Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.3

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO 3

Maana maalumu ya neno “dini”.

Maana maalumu ya neno dini sio kitu chengine isipokuwa “dini ya haki ya kiislamu” kama anavyosema Allah (s.w) :-

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللهِ الإِسْلاَمُ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ اُوْتُواْ الْكِتَابَ إِلاَّ مِن بَعْدِ مَا جَاءهُمُ الْعِلْمُ بَغْياً بَيْنَهُمْ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللهِ فَإِنَّ اللهِ سَرِيعُ الْحِسَابِ[1]

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

Nguo ya dini inaendana sawa na Uislamu, na Uislamu unawafunga watu katika mfumo mmoja. Na kwa sababu neno “ISLAM” kijumla lina maana ya kusalimu amri (kusarenda) katika amri, sheria, kanuni na hukumu zote alizoamrisha Mwenyeezi Mungu. (hukumu za kimaumbile na hukumu za kisheria) . Kwa hiyo, kwa kuzingatia maana ya neno Islam,ni lazima maana ya neno dini liwiane na maana hiyo.

Ni jambo lililowazi kabisa kuwa, haiwezekani kulitumia neno dini katika maana yake ya kijumla, na kulitumia neno hilo kwa kulipa maana maalumu, kwa sababu neno dini limetumika katika sehemu tofauti likiwa na maana tofauti. maana ya kijumla ya neno dini inaweza kutafsiriwa katika mambo mbali mbali, kwa mfano, tunaweza kusema dini ya kikafiri, au dini ya washirikina, n.k. hiyo ni kwa mtazamo wa kijumla, lakini neno dini katika maana yake maalumu inakusudiwa dini ya Kiislamu, na hii ndio maana sahihi.

Neno dini, na neno Islam, linashabihiana na kuwiana katika maana zake, tukijaalia kuwa sadikisho la dini ni Islam, basi tunaweza kulifafanua neno dini katika mtazamo wa kitaalamu kwa kusemaDini ni mkusanyiko wa desturi, mabainisho, maamrisho ya kimaumbile na ya kisheria, yanayowafungamanisha watu katika mfumo mmoja kulingana na mahitajio ya vitu vyote ulimwenguni,wanaadamu, mimea, wanyama n.k. yote hayo yametumwa na Mwenyeezi Mungu kupitia Mitume na Ahlulbayt wake kwa ajili ya kuwapelekea wanaadamu na viumbe vyote kijumla .ili waifikie saada katika maisha yao ya  duniani na Akhera .

[1] Surat Al-Imrani Aya ya 19

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini