Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Kusoma Qurani

ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN

ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN

ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN Wasomaji na wanaoishughulikia Quraan wana mtizamo maalum katika dini yao na wana haki ya kufanyiwa hivyo, kwani amana walioibeba ni kubwa ukilinganisha na kitu chengine chochote lau kama tunazingatia. Katika jumla ya matukufu wanayoyopata ni: " Kuhusishwa moja kwa moja na Allah(S.W) wake na ndio watu aliokhusisha nao(yeye). " Idadi ya aya za peponi ni kwa mujibu wa aya alizozihifadhi msomaji na kuwa watakao ingia katika waliohifadhi hawapindukiwi na mtu yeyote. " Malipo ya wasomao Quraan ni kila herufi moja kwa jema moja na jema moja kwa thawabu kumi. " Mwenye kushikamana kikweli na Quraan hapotei milele. " Mbora na mtukufu wa watu ni yule aliyejifunza Quraan na kuifundisha. " Wanaokusanyika na kusoma na kuidurusu Quraan hufunikwa na malaika na kupata rehma na utulivu wa nafsi na Mwenye-ezi-Mungu anajifakharisha kwa watu hao juu ya malaika wake na wanakuwa wageni wa Mwenye-enzi-Mungu muda wa kuwa wapo katika mkusanyiko huo.

Ufafanuzi

SABABU 7 ZA KUSOMA QURANI

SABABU 7 ZA KUSOMA QURANI SABABU 7 ZA KUSOMA QURANI HAKIPINGIKI Qurani imesimama madhubuti kwenye majaribio na utafiti mwingi. Na hakuna aliekuja na sababu madhubuti za kuipinga ukweli uliomo ndani yake. Qurani inazungumzia mambo yaliopita na kinaonekana kinaeleza ukweli. Kimeeleza kuhusu Manabii waliotangulia na kimeonekana ukweli wake na kinachambua na kueleza mambo ya kuustajibisha ambayo yalikuwa hayajulikani na watu katika wakati huo. Na bado mambo ya uchunguzi na utafiti wa Sayansi umegundua na kuthibitisha ya kwamba Quran ishaeleza mambo hayo zamani kabisa. Kila kitabu huwa kinahitaji mapitio kuhakikisha kinakwenda na mahitaji ya wakati uliopo. Qurani ni kitabu pekee ambacho hakihitaji kupitiwa ili kukidhi mahitaji ya wakati ulipo, Qurani ipo imara na ipo kwa Wakati. (up to date).

Ufafanuzi

FADHILA ZA QURANI

FADHILA ZA QURANI FADHILA ZA QURANI MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir kutoka kwa Ali bin Hussen (a.s) na ameipokea hadithi hii kutoka kwa Abi Abdillah (a.s) amesema: Mwenye kusikiliza herufi moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya kusoma, Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja na kumfutia kosa moja na kuinuliwa daraja moja, na mwenye kusoma kwa kuangalia bila ya kusali Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi jema moja na kumfutia kosa moja na huinuliwa daraja moja, na mwenye kujifunza herufi moja ya dhahiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humuandikia mema kumi na kumfutia makosa kumi na kuinuliwa daraja kumi, akasema: Si semi kwa kila aya lakini kwa kila herufi sawa iwe baa au faa au mfano wa hizo, akasema: Na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amekaa kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi hiyo mema khamsini, na kumfutia makosa khamsini, na kumuinua daraja khamsini, na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia mema mia moja na kumfutia makosa mia moja na kumuinua daraja mia moja, na mwenye kuihitimisha, maombi yake ni yenye kukubaliwa, sawa yachelewe au yawahi akasema: Nikasema: Niwe fidia yako mwenye kuihitimisha yote? Akasema: Mwenye kuihitimisha yote.

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.5

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.5 DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO.5 Katika makala iliyopita, (makala ya nne inayohusiana na dini ya haki ya Kiislamu) tulielezea kuwa dini ya haki ni dini ya Kiislamu pekee, lakini baadhi ya wafuasi wa dini nyengine kama Mayahudi na Manasara walidai kuwa dini zote ni haki, na mfuasi wa dini yoyote ile atapata saada na ujira mwema kutoka kwa Mola wake, na watu hao wamethibitisha madai yao hayo kupitia dalili za Qur-ani takatifu, hivyo katika makala hii tutaelezea baadhi ya madai ya watu hao na kuyapatia majibu yake inshaallah. suala liko hapa hivi kweli dini za Mayahudi na Manasara ni dini za haki ? kwani dini za Mayahudi na Manasara zote hazikuteremshwa na Mola Mtakatifu? basi hivi kweli madai hayo ni sahihi? Madai ya watu hao ni haya yafuatayo:- Katika Aya ya 62 ya Suratul Baqarah Allah (s.w) anasema: إِنَّ الَّذِينَ آمَنُواْ وَالَّذِينَ هَادُواْ وَالنَّصَارَي وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحاً فَلَهُمْ اَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ Kupitia Aya hiyo wamethibitisha kuwa:- 1. Aya hiyo inatoa himaya kwa dini tofauti na watu tofauti, na sio Dini ya Kiislamu tu, au kwa wafuasi wa dini ya Kiislamu. 2. Aya hiyo inawapa himaya na kuwalingania watu wa dini tofauti, kumuamini Mwenyeezi Mungu, kuamini siku ya Kiyama, na kufanya amali njema. 3. Aya hiyo inaunga mkono dini tofauti. Na sio dini ya Kiislamu tu. Bali watu wa dini zote watapata saada na ujira mzuri kutoka kwa Mola wao. 4. aya hiyo imeelezea sifa tatu zitakazowafanya watu wa dini tofauti kupata saada.

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.4

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.4 DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO.4 Ni sahihi kuwa neno “Dini” kwa mtazamo wa wanalugha ni neno lililozoeleka, na kila mmoja analifahamu neno hilo, lakini maana hasa ya dini si ile maana ambayo kila mmoja wetu amezoea kuisikia. Dini katika mtazamo wa kitaalamu (kiistilaha) lina maana pana zaidi. Dini sio neno kuu lililokusanya ndani yake aina au maana zote za dini kiasi ya kwamba wakati lisilikapo liwe linamaanisha aina yoyote ile ya dini, ufafanuzi wa dini unaokubalika unatakiwa uwe umepatikana katika dini yenyewe, yaani katika vitabu vya dini. Kwa hiyo maana asili ya neno hilo inayokusudiwa hapa, ni dini ya Kiisalamu. Ndio, neno hilo lina maana maalumu, na linatumika katika dini ya Kiislamu tu.

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.3

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.3 DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO 3 Maana maalumu ya neno “dini”. Maana maalumu ya neno dini sio kitu chengine isipokuwa “dini ya haki ya kiislamu” kama anavyosema Allah (s.w) :- إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللهِ الإِسْلاَمُ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ اُوْتُواْ الْكِتَابَ إِلاَّ مِن بَعْدِ مَا جَاءهُمُ الْعِلْمُ بَغْياً بَيْنَهُمْ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللهِ فَإِنَّ اللهِ سَرِيعُ الْحِسَابِ[1] Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. Nguo ya dini inaendana sawa na Uislamu, na Uislamu unawafunga watu katika mfumo mmoja. Na kwa sababu neno “ISLAM” kijumla lina maana ya kusalimu amri (kusarenda) katika amri, sheria, kanuni na hukumu zote alizoamrisha Mwenyeezi Mungu. (hukumu za kimaumbile na hukumu za kisheria) . Kwa hiyo, kwa kuzingatia maana ya neno Islam,ni lazima maana ya neno dini liwiane na maana hiyo. Ni jambo lililowazi kabisa kuwa, haiwezekani kulitumia neno dini katika maana yake ya kijumla, na kulitumia neno hilo kwa kulipa maana maalumu, kwa sababu neno dini limetumika katika sehemu tofauti likiwa na maana tofauti. maana ya kijumla ya neno dini inaweza kutafsiriwa katika mambo mbali mbali, kwa mfano, tunaweza kusema dini ya kikafiri, au dini ya washirikina, n.k. hiyo ni kwa mtazamo wa kijumla, lakini neno dini katika maana yake maalumu inakusudiwa dini ya Kiislamu, na hii ndio maana sahihi.

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.2

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.2 DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO2 Katika Qur-ani, neno Dini limekuja na maana mbili, maana ya kijumla, na maana maalumu. Kwa mtazamo wa Qur-ani, neno dini kwa maana ya kijumla limekuja likiwa na maana ya akida na madhehebu, katika maana hiyo, neno hilo limekusanya akida na dini tofauti na sio dini ya Mwenyeezi Mungu, kwa sababu kuna aina mbili za dini. Dini za Nabii Ibrahimu (a.s) (ambazo ndio dini za Mwenyeezi Mungu) na dini zinazotokana au zilizoundwa kutokana na tamaduni za watu. (dini za Makafiri, washirikina.nk.) katika paragrafu hii natushuhudie baadhi ya Aya ambazo ndani yake neno Dini limetumika. Allah (s.w) anasema:- وَكَذٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ اَوْلاَدِهِمْ شُرَكَآؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُواْ عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ[1] A: Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwauwa watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua. *Maelezo kuhusiana na Aya:- Makafiri walikuwa wakuwatoa mihanga watoto wao kuwapa masanamu yao, wakiona ni kheri hivyo wanavyofanya.

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.6

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI No.6 DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO.6 Katika makala iliyopita tulielezea madai yaliyotolewa na baadhi ya wafuasi wa dini tofauti, miongoni mwa hao ni wafuasi wa dini ya kiyahudi na Manasara, watu hao wanadai kuwa dini zote ni haki na Mola (s.w) atawalipa waja wake wote ujira mwema na kuwaongoza katika njia ya saada. tuliyajibu madai ya watu hao kwa kutoa dalili za Qur-ani takatifu kuwa dini ya haki ni dini ya Kiislamu tu, katika makala hii tutaendelea kuyajibu madai hayo kwa dalili mbali mbali inshaallah. tuliyajibu madai hayo na tukafikia kifungu cha tatu, na sasa hivi tutkielezea kifungu cha nne kwa kusema:- Nne: Katika Qur-ani takatifu kuna Aya nyingi zinazoelezea kwa uwazi kabisa kuhusiana na akida za Mayahudi na Manasara, na Mwenyeezi Mungu amezichukia na kubainisha kuwa akida hizo sio sahihi.

Ufafanuzi

HATARI ZA BID_A

HATARI ZA BID_A HATARI ZA BID_A Katika makala iliyopita (makala namba 2), tulielezea maudhua yanayohusiana na sifa tukufu za Mitume, na tukabainisha sifa mbili ambazo wanatakiwa Mitume kuwa nazo, sifa hizo zilikuwa ni elimu, na kuwa Maasumu, katika makala namba mbili tulifikia sehemu inayosema kuwa, "kama angelizua juu yetu baadhi ya maneno" ambayo ni tarajama ya Aya ya 44 ya Surat Haaqqah, basi tukapata maelezo na maudhui yanayohusiana na Aya hiyo, maudhui hayo yalikuwa ni Bid-a, katika makala hii tutaelezea kwa kina kuhusiana na maudhui hayo. UFAFANUZI WA NENO BID_A. Neno "Bid-a kilugha ni: lina maana ya Lenye kuzuka" ikiwa ni zuri au baya. Ama "Bid-a kitaalamu (kiistilaha) ni hivi asemavyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) "kila lenye kuzuka ni upotovu, na upotovu wote utatupwa motoni" "Yatakapotokeza yenye kuzuka katika umati wangu basi mwanachuoni aonyeshe elimu yake (kwa kukanya hayo) na yeyote asiyefanya (hilo) basi laana ya Mwenyeezi Mungu iko juu yake."

Ufafanuzi

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI

DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO 1 UFAFANUZI WA NENO DINI KILUGHA NA KISHERIA Ufafanuzi wa neno “dini” kilugha na kisheria ndani ya historia ya mwanaadamu. Chanzo na asili ya neno dini, kwa mtazamo wa wana lugha; wao wamesema kuwa, dini ni neno wanalotumia waajemi wa kizamani (persian) linalotokana na neno – Daena – likiwa na maana ya johari, hisia na dhati ya mwanaadamu, na baadhi ya watu wamesema kuwa asili ya neno –Daena – lina maana ya kutafakari na kutambua, na wanaamini kuwa neno hilo ni miongoni mwa maandishi maalumu ya sanskrit dehi, Sanskrit ni lugha ya zamani ya india na nchi za mashariki ya kati kwa ujumla, kwa mfano,Irani, Palestina n.k. Wafuasi wa dini ya Zartushti walijiita “Behdiyn” wakiwa na maana ya watu waumini, na katika kitabu cha Zartushti neno “dini” limekuja likiwa na maana ya kishi, akida, dhati ya mwanaadamu,tabia za kiroho, haiba ya kibinaadamu na hisia za ndani za mwanaadamu.

Ufafanuzi

MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU

MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU Mwenyeezi Mungu Mtakatifu katika Surat Al-Imrani Aya ya 28 anasema hivi:- لاَّ يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ اَوْلِيَاء مِن دُوْنِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللهِ فِى شَيْءٍ إِلاَّ اَن تَتَّقُواْ مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللّهُ نَفْسَهُ وَإِلَي اللهِ الْمَصِيرُ[1] Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. Katika aya hiyo limekuja neon “Tuqaata” yaani taqiyya, likiwa na maana ya kuficha imani ndani ya moyo, na kutamka yaliyo kinyume na hayo. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. Katika aya hiyo limekuja neon “Tuqaata” yaani taqiyya, likiwa na maana ya kuficha imani ndani ya moyo, na kutamka yaliyo kinyume na hayo.

Ufafanuzi

MAYAHUDI NDANI YA QUR_ANI

MAYAHUDI NDANI YA QUR_ANI MAYAHUDI NDANI YA QURANI Mwenyeezi Mungu Mtukufu ndani ya Kitabu chake kitakatifu (Qur-ani) Suratul-Baqarah Aya ya 85 anasema hivi:- ثُمَّ اَنتُمْ هَـؤُلاء تَقْتُلُونَ اَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقاً مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَاتُوكُمْ  اُسَارَي تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ اَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاء مَن يَفْعَلُ ذٰلِكَ مِنكُمْ إِلاَّ خِزْيٌ فِى الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَي اَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ. Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda. Maelezo kuhusiana na Aya: Madina kulikuwa na makabila mawili: Aws na khazraj. Watu wa makabila haya kabla ya kusilimu walikuwa mara kwa mara wakipigana, Mayahudi wa madina waligawanyika makundi mawili,wengine wakaunga mkono upande wa Aws, na wengine upande wa Khazraj. Kwa hivyo wakati yanapopigana makabila mawili haya, Mayahudi wa upande mmoja walikuwa wakiua Mayahudi wenzao wa upande mwengine

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO7

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO7 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaendelea na mada yetu ile ile inayohusiana na malengo ya Mitume. 5. KUWALINGANIA WATU KUHUSU SIKU YA KIAMA Mitume, baada ya kuwalingania watu tawhiyd, na kuwataka wamuabudu Mola mmoja, ujumbe mwengine muhimu waliokuja nao ni kuwafunza na kuilea jamii, kuwapa wanaadamu habari kuhusu siku ya Kiama, na kuwataka wajiepushe na anasa za dunia, kwani zinaweza zikawapeleka pabaya, vile vile Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliwatia mori na shauku watu ili wapigane jihadi, na wawe madhubuti katika hukumu za dini yao.

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.6

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.6 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.6 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaendelea na mada yetu ile ile inayohusiana na malengo ya Mitume. 4. KUPIGANIA HAKI ZA WATU DHAIFU NA KUPIGANA NA MADHALIMU Watu dhaifu ni wale watu ambao kutokana na hukuma za madhalimu, hawawezi kupigania haki zao, na wameharamika katika kuhifadhi tamaduni zao, na kwa sababu hizo basi hawapati kuamua mambo yao, vile ambavyo inawapasa kuayaamua, watu hao ndani ya Qur-ani wamesifiwa hivi :- إِلاَّ الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ لاَ يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلاَ يَهْتَدُونَ سَبِيلاً[1] Isipo kuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama.

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.5

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.5 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.5 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaendelea na mada yetu ile ile inayohusiana na malengo ya Mitume. 3. KUTIMIZA UADILIFU Pindi jamii ya wanaadamu ikiwa katika hali ya usalama, hapana shaka italeta athari kubwa miongoni mwa wanaadamu, na ni kwa sababu hiyo basi Mitume yote imefanya jitihada katika kuhukumu kanuni za Mwenyeezi Mungu, na kuwafanya wanaadamu kunufaika na haki zao binafsi, na vile vile haki zao katika jamii, hakuna mtu mwenye haki ya kudhulumu, wala hakuna mwenye kudhulumiwa.

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.4

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.4 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.4 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, na tukafikia sehemu ambayo ilitulazimu kuelezea maana ya neno Tawhiyd, katika makala hii tutendelea kufafanua kuhusu neno hilo na kuthibitisha hayo kwa mujibu wa Aya za Qur-ani takatifu. Maana nyengine ya neno Tawhiyd : Ni kuwa, maisha na rizki zote za wanaadamu zinakuja kutokana na mapendeleo yake Mwenyeezi Mungu.

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.3

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.3 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.3 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala iliyopita tulielezea lengo moja miongoni mwa malengo ya Mitume, nalo lilikuwa ni kutumia akili na kupinga kukalidi bila ya kuwa na dalili au elimu yoyote.  katika makala hii tunaendelea na lengo jengine nalo ni kuwalingania watu kumuabudu Mola mmoja na kupingana na wafanyao shirki. MITUME (A.S) IMESHIRIKIANA KATIKA MALENGO YAO. Tukitupilia macho elimu ya Tarekhe tutafahamu kuwa katika kipindi chote kilichopita elimu ya Tarekhe inathibitisha kuwa Mitume yote imekuja ikiwa na malengo mamoja, nayo ni kuwalingania wanaadamu kwa kuwataka wamuabudu Mola mmoja.

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.2

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.2 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.2 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?.katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutabainisha malengo hayo muhimu moja baada ya mengine. Tukitupilia macho elimu ya Tarekhe tutafahamu kuwa katika kipindi chote kilichopita elimu ya Tarekhe inathibitisha kuwa Mitume yote imekuja ikiwa na malengo mamoja, nayo ni kuwalingania wanaadamu kwa kuwataka wamuabudu Mola mmoja. Miongoni mwa malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni haya yafuatayo:- 1. KUTUMIA AKILI NA KUPINGANA NA KUKALIDI Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu imewalingania watu kutumia akili na kupigana na kukalidi mambo ya wengine bila ya kuwa na dalili nayo,Kuwalingania watu kutumia akili na dalili na kujikinga na dhana ni miongoni mwa malengo waliyoshirikiana Mitume katika kuwalingania wanaadamu, kwa sababu akili ni nyenzo ya kukubali wahyi, Mitume imekuja kwa ajili ya kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka. kwa hiyo, njia ya Mitume ndio njia bora inayopambanua maarifa ya Mwenyeezi Mungu,

Ufafanuzi

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.1

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.1 MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.1 * Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?. MITUME (A.S) IMESHIRIKIANA KATIKA MALENGO YAO. Tukitupilia macho elimu ya Tarekhe tutafahamu kuwa katika kipindi chote kilichopita elimu ya Tarekhe inathibitisha kuwa Mitume yote imekuja ikiwa na malengo mamoja, nayo ni kuwalingania wanaadamu kwa kuwataka wamuabudu Mola mmoja, na hii ni katika sunna zake Allah (s.w). kama alivyosema:- إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ وَتِلْكَ الايَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاء وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ الظَّالِمِينَ[1] Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu.

Ufafanuzi

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.4

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.4 SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 4. USHAHIDI WA MITUME KWA UMATI WAO Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu sifa tukufu za Mitume (s.a), na tukaelezea miongoni mwa sifa hizo kuwa ni elimu, Maasumu na kuweza kuleta miujiza. katika makala hii tutaendelea na mada hiyo kwa kuelezea kuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu inashuhudia amali na matendo ya umma zao. Mitume inashuhudia amali na matendo ya umati wao. Miongoni mwa sifa nyengine za Mitume, sifa ambazo zitadhihirika siku ya Kiama, ni kwamba kila Mtume ataona amali za umma wake, na siku ya Kiama atatoa shahada ya amali zao. Kama anavyosema Allah (s.w):- Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Ufafanuzi

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini