USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA QURAN
USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KUPITIA QURAN
Ayatul Wilayah ni aya nyingine ya Qur'an inayothibitisha Ukhalifa wa Ali bin Abitalib (a.s), Aya hii ipo katika Suratul Maidah (5:55) ambayo inasema: "Walii wenu ni Allah, Mtume wake na waumini wanaosimamisha sala na wanaotoa zakat huku wakiwa katika hali ya rukuu". Maulamaa wote wa Tafsiir na Hadith, wa Kishia na Kisunni, wanakubali kwamba aya hii iliteremka kwa ajili ya Imam Ali bin AbiiTaalib (a.s), baadhi ya maelezo ya wasimuliaji wa hadithi wa upande wa Kisunni ni kama ifuatayo:
A - Suyuti amesimulia katika tafsiir yake katika kitabu chake Tafsiir Durrul Manthur kwamba Ali bin AbiiTalib alitoa pete yake sadaka na kummpa masikini alipokuwa katika sala akirukuu; hivyo Allah akateremsha Aya hii ya Al maaida (5:55). B - Mwanazuoni wa Kisuni Tabrani katika kitabu chake "Awsat" amesimulia kuwa: "Siku moja maskini mmoja alisimama pembeni ya Ali ambaye alikuwa katika sala akirukuu (Sunnah) na akaomba chochote, hivyo Ali akampa pete yake kutoka kidole chake alipokuwa katika Rukuu. Mtume (s.a.w.w) alipokuja msikitini Imam Ali alimuarifu Mtume juu ya tukio hilo na hapo hapo ikashuka aya ya Suratul Maaida (5:55). Mtume aliisoma aya hii kwa sabaha zake na akasema:
"MAN KUNTU MAWLAHU FAALLIYUN MAWLAHU. ALLAHUMMA WAALI MAN WAALAAHU, WA AADI MAN AADAAHU". Yaani: "Kwa yeyote ambaye anaamini kua mimi ni kiongozi wake, basi Ali ni kiongozi wake (baada yangu), Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa pmoja naye yule atakayekua pamoja na Ali na kuwa adui wa yule anayeonyesha uadui kwa Ali".
USHAHIDI NA UTHIBITISHO KWA KPITIA QURAN

C - Fakhruddin Raazi katika Tafsiir yake amesema kuwa Abudhar Al-Ghaffari alisimulia kuwa: Siku moja Mtume alimuomba Allah kwa kusema : "Ewe Allah, ndugu yangu Nabii Musa alikuomba kwa kusema: kipanue kifua changu, irahisishe kazi yangu na ondoa uzito katika kauli yangu, ili waelewe wake ninaowalingania kile ninachokisema na nipatie Wazir (msaidizi) kutoka katika familia yangu, Haruun ndugu yangu, na nizidishie nguvu kupitia kwake na mfanye awe mshirika wangu katika kazi yangu ----". (Taha 20:25-32)
"Ewe Allah, mimi ni Muhammad, Mtume wako na mjumbe wako Mpendwa, hivyo ninakuomba ukipanue kifua changu, uirahisishe kazi yangu na unipe Wazir (msaidizi) kutoka katika familia yangu, Ali ndugu yangu na niongezee nguvu kupitia kwake ----". Abudhar anaendelea kwa kusema : "Wallah, Mtume hakumaliza hata kumaliza dua yake, Jibriil akaja na kuteremsha Aya ya (5:55) ya Suratul Maaida, ambapo Ali alitoa pete yake kama sadaka kwa masikini alipokuwa akirukuu". Maulamaa wengine wa kisunni waliosimulia tukio hili ni : Al-Ganji Shafii katika Kifayat Al- Talib, Shablanji katika Noorul Absaar, Al-Waahidi katika Asbaabun Nuzul, Zamakhshari katika Tafsirul Kashshaf, Ibn Hajr Asqalani katika Al-Kafi Ash-Shafi, Abubakar Ahmed bin Ali Ar-Razi Al-Hanafi katika Ahkamul Qur'an, Al -Qurtubi Al-Undulusi katika Al-Jami' Li Ahkamil Qur'an, Shahabuddin Al-Aluusi katika Ruuhul Ma'aani, Sibt ibn Al-Jawzi katika Tadhkirah, na waandishi wengine wengi wa Kissuni.
Watafiti wa ukweli wanatakiwa warejee vitabu hivyo hapo juu ili waupate ukweli kuwa Ali bin Abitalib ni Walii, Imam, Khalifa na Wasii baada ya Mtume kama ilivyo katika aya hii ya (5:55) ya Suratul Maaida. Qur'an tukufu inaendelea katika aya inayofuata kwa kusema: "Na kwa wale walioukubali Uwalii wa Allah na Mtume wake na wale walioamini (Imam Ali bin AbiiTaalib), basi kwa hakika kundi la Allah (Shia wa Imam Ali) ndio wenye kufaulu". (MAIDAH 5:56). Aya hii inafuatia baada tu ya aya ya (5:55) ya Suratul Maaida. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu wanakana Uwalii na Ukhalifa wa Imam Ali bin Abii Taalib (a.s) mara tu baada ya Mtume (s.a.w.w). Juu yao Qur'an inasema : "Wanazitambua neema za Allah, kisha wanazikataa, na wengi wao hawana shukrani". (Nahl 16:83).