Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

FALSAFA YA DINI NO.1

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

FALSAFA YA DINI NO.1

Ikiwa walimwengu watafahamu na kuelewa falsafa na umuhimu wa dini hapana shaka kila mwanaadamu mwenye akili salama atafuata dini na kutekeleza maamrisho yake, kwa sababu dini ni nyenzo inayomtekelezea mwanaadamu mahitajio yake ya kila siku. katika makala hii tutaelezea miongozo ya dini ambayo inaweza kumuongoza mwanaadamu katika njia iliyo sahihi. Miongoni mwa miongozo hiyo ni hii ifuatayo:-

A:Amri na hukumu za dini ni zenye kuwafunga watu katika mlolongo wenye kuleta maendeleo, maendeleo ambayo hupatikana baada ya utekelezwaji wa matendo na amri, au pale wanaadamu wanaposhikamana na ule mfumo wa amri na matendo yanapotakiwa kutendeka. Hukumu na desturi zimejengeka katika njia mbili:-

1. Ni pale iwapo matendo yatatendeka natija itapatikana.

2. Matendo hutendeka baada ya kuzikubali amri, katika njia hii pia natija itapatikana.

Kanuni na desturi ambazo ndani yake hazina hata chembe ya rangi inayoweza kutoa maendeleo ya wanaadamu huwa hazielekezwi kwa wanaadamu kupitia dini, lakini kunaweza kupatikana misingi ambayo kiudhahiri wake haimuelekezi mtu moja kwa moja kufikia malengo fulani, hiyo haimaanishi ya kuwa misingi hiyo haina maana , kwa kuzingatia kwa makini utaelewa kuwa misingi hiyo inaweza kukufikisha katika malengo yanayokusudiwa.

B: Dini ni mabainisho ya haki yaliyofungamana na malengo ya wanaadamu, katika kipindi chote cha tarehe, dini ina dhamini na kukidhi mahitajio ya wanaadamu, na Mwenyeezi Mungu amewateremshia waja wake dini ambayo mwanaadamu ana uwezo wa kuifahamu, na kwa sababu dini ni haki, basi humpa mwanaadamu muongozo, saada na yale yote anayoyahitajia katika maisha yake.

Mahitajio ya mwanaadamu yamegawika katika sehemu mbali mbali, baadhi ya wakati mwanaadamu anahitajia mahitajio yake mwenyewe binafsi, baadhi ya wakati anahitajia mahitajio katika jamii n.k. (mahitajio hayo yanaweza kuwa ya dhati, au yanayotokana na nafsi, au yanayotokana na fitra ya mwanaadamu n.k). Imam Sadiqi (a.s) kuhusiana na hayo anasema hivi:-

قال الصادق علیه السلام:" والله انی لاعلم کتاب الله من اوله الی اخره کانی فی کفی فیه خبر السماء وخبر الارض وخبر ما کان و خبر ما یکون وکائن قال الله عز و جل:

Imam Saadiqi (a.s) amesema:-

Naapa kwa jina la Mola wangu, mimi ninakijua kitabu cha Mwenyeezi Mungu kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake kama kwamba katika kiganja changu kumewekwa habari zote za mbinguni na ardhini, ziliopo, zilizopita, na zijazo. Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِى كُلِّ اُمَّةٍ شَهِيداً عَلَيْهِم مِّنْ اَنفُسِهِمْ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيداً عَلـٰي هَـؤُلاء وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَاناً لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَي لِلْمُسْلِمِينَ[1]

Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Maelezo kuhusiana na Aya.

Hapa zinabainishwa baadhi ya nafuu zilizopatikanwa kwa kuteremshwa Qur-ani.

 Ni jambo lililo sahihi kuwa maudhui ya dini ni mwanaadamu, lakini mwanaadamu ni kiumbe bora na ni alama kamili yenye kuashiria uhakika wake Allah (s.w), mwanaadamu akiwa ni ashirio kamili katika ulimwengu huu yeye ndiye muhusika mkuu wa dini, na kwa upande wa pili ni khalifa wa Mwenyeezi Mungu, na yeye anatakiwa kuzifanya amri zote alizoamrishwa na Mola wake, na kumpa kila mja majukumu yake kwa jinsi ya mamlaka yake yalivyo, na yeye ndiye mwenye kutekeleza matakwa ya Allah (s.w). Maelezo hayo yana maana ya kuwa; dini haimuhusu mwanaadamu peke yake tu, kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka ya kugawa majukumu ya viumbe wengine, bali dini inahusu viumbe vyote duniani, vilivyo na uhai na visivyo na uhai. (miti, wanyama na mimea). Kila kiumbe kina wadhifa wake katika dini kulingana na mahitajio yake, na daraja iliyonayo kiumbe hicho.

Kwa hiyo uhakika wote wa dini sio kwa ajili ya binaadamu tu, bali ni kwa ajili ya viumbe vyote duniani, na Mitume ya Mwenyeezi Mungu na Ahlulbayt (a.s) ndio misingi asili ya dini ya kila haki kijumla jamala, (haki zinazotambulika na zisizotambulika), na hao ndio vigezo bora vya uongofu, wanaweza kuwaongoza na kuwaongoa watu wote hata muovu aliyebobea katika maovu.

[1] Surat An-Nahl Aya ya 89

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini