Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UFAFANUZI WA DINI NO.1

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UFAFANUZI WA DINI NO.1

Ufafanuzi wa dini:-

Dini ni udadisi na utafutaji wa mwanaadamu kwa ajili ya kumfikia na kumtambua Mola wake, siku zote, hatima ya udadisi na utafutaji huo humalizikia kwa Mola Mtakatifu, kwa hiyo udadisi na utafutaji huo ni lazima ufanywe kwa mujibu wa mapendekezo ya mwanaadamu mwenyewe.

Ufafanuzi huo wa dini ulioelezewa hapo juu hautoshelezi, kwa sababu, (ingawa) Mwenyeezi Mungu anayekusudiwa ni yule Mwenyeezi Mungu aliye katika nyoyo za wanaadamu, na hii inaonyesha nafasi ya mwanaadamu katika dini, hali ya kwamba maudhui ya dini ni mwanaadamu, na nafasi ya dini kwa mwanaadamu sio Mwenyeezi Mungu tu, bali kuna mambo mbali mbali yaliyo muhimu kwa mwanaadamu.

Ili kutambua umuhimu wa dini ni vyema tukaashiria baadhi ya vidokezo vinavyohusiana na ufafanuzi na umuhimu wa dini kwa walimwengu na jamii kwa ujumla.

Vidokezo kuhusiana na ufafanuzi wa dini.

Vidokezo vya mwisho:

Kidokezo ni habari au jambo linalosaidia kutoa fununu au njia ya kufumbua tatizo fulani.

 Kidokezo cha kwanza:

Maelezo na ufafanuzi huo wa dini ulioelezewa, ni ufafanuzi uliochopolewa kupitia chungu za riwaya, hadithi, nyanzo za dini, vitabu vya dini, na juhudi za kiakili. Kwa hiyo, ufafanuzi huo umetolewa katika matini za dini, na umepatikana baada ya kutafakariwa kwa fikra zilizo salama.

Ni sahihi kuwa , ufafanuzi huo (kijumla jamala) haukupatikana katika matini zozote za dini, (kwa mfano,(hadithi na riwaya)) au katika maelezo maalumu, lakini masharti na taaluma yote hiyo iliyotumiwa katika kuifafanua dini imechukuliwa katika matini za dini.

Kidokezo cha pili:

Kama ilivyokwisha ashiriwa hapo mwanzo; kuwa dini sio mabainisho ya yaliyofungika katika mfumo maalumu tu, bali mbali ya mfumo huo ulio na fungamano maalumu na matakwa ya binaadamu, vile vile unabainisha taaluma nyengine nyingi zinazohusiana na mambo mbali mbali, kama anavyosema Alameh Tabatabai anasema:-

“Mfumo huu, ni mfumo ule ule ambao Qur-ani takatifu umeubainisha au kuutambulisha kwa jina la dini, na mfumo huo utakuwa ni ule mfumo asili unaotokana na chanzo cha nguvu za muumbaji”.

Mbali ya kuwa dini anaelezea mfumo maalumu, vile vile inaelezea elimu nyengine ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na namna ya utekelezwaji wake, kwa hiyo kuifunga dini katika mfumo maalumu ni kuiwekea dini mipaka katika fikra na kimitazamo, hali ya kwamba dini vile vile ina nafasi nyingi katika mitazamo ya kidunia, mitazamo ambayo baadhi ya wakati ina uhusiano wa moja kwa moja na nafasi ya utendaji wake.

Kidokezo cha tatu:

Ni jambo lililo sahihi kuwa, miongoni mwa mielekeo ya mwanaadamu ni mwelekeo wake wa kijamii, lakini maisha yote ya mwanaadamu hayamaliziki katika mwelekeo wa jamii tu, mpaka ifafanuliwe kuwa “dini” kwa mtazamo wa qur-ani, ni mfumo maalumu wa maisha ya kijamii ya mwanaadamu, ambapo mwanaadamu huchagua mfumo huo kwa ajili ya kudhamini saada ya maisha yake[1]. Mwanaadamu ni kiumbe mwenye mielekeo miwili, na ni kwa sababu hiyo basi, hukumu na taaluma za dini baadhi ya wakati ni za kijamii na baadhi ya wakati ni za mtu binafsi. Hivyo kuifunga dini katika muelekeo wa kijamii tu sio jambo lenye kukubalika.

Kidokezo cha nne:

Dini sio kuwa na itikadi peke yake tu, kwa sababu, mabainisho na maamrisho ya Mwenyeezi Mungu kuhusiana na dini baadhi ya wakati ni mabainisho ya kiakida, na baadhi ya wakati sio ya kiakida. Kwa hiyo, kutokana na maelezo hayo tunaweza kuifafanua dini hivi:-

Kidokezo cha tano:

Dini, ni kuwa na imani na akida na Mola Muumba, (Mola ambaye amemuumba mwanaadamu, dunia, na kila kilichomo) ili kuyatekeleza maamrisho yake kiamali na kimatendo kwa mujibu yanavyowiana na itikadi yake.

Ufafanuzi huo wa dini ni kwa mujibu wa natija zilizopatikana kwa mawafikiano, na ufafanuzi huo sio natija kamili inayotokana na uhakiki wa dini?

Kidokezo cha sita:

Dini ya haki na ya kweli ni ile dini ambayo inawafunga watu katika fungamano na mfumo mmoja, na inawalazimu wao kuitii dini hiyo. fungamano hilo linatokana na kitu zaidi ya fikra na zaidi ya hisia, fungamano ambalo natija yake ni kuwa na imani na dini, kwa hiyo dini sio kuwa na ufahamu au hisia za hali ya juu kabisa tu, bali mbali ya vitu hivyo viwili ni lazima mwanaadamu aifikie daraja ya kuwa na imani ya kimoyo ya dini hiyo. (dhahiri na batini).

Kidokezo cha saba:
Kuwa na dini sio kumtambua Mwenyeezi Mungu tu, kwa maelezo mengine, kutafuta dini kwa mwanaadamu kutoka kwa Mola wake, sio kwa ajili ya kumfikia Mola wake tu,( bali, baada ya kumtambua Mwenyeezi Mungu kuna mambo mengine pia yanayotakiwa kutekelezwa), Kwa sababu kumtambua Mwenyeezi Mungu ni sehemu ya dini, na sio dini yote, kwa maelezo mengine, kila mwenye kumtambua Mwenyeezi Mungu haimaanishi kama yeye ana dini, Mwenye dini ni yule mtu ambaye anamkubali Mwenyeezi Mungu katika nyanja zote na kwa matakwa yake yote,maamrisho yake, hali halisi ya uumbaji wake, daraja ya utukufu wake n.k. Awe ni mwenye kumkubali Mwenyeezi Mungu kifikra, kiamali kimwenendo na kimatendo.

[1] Rejea katika feheresi ya makala iliyopita.

 

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini