Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UFAFANUZI WA DINI NO.3

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UFAFANUZI WA DINI NO.3
Ufafanuzi wa dini:-
Dini ni udadisi na utafutaji wa mwanaadamu kwa ajili ya kumfikia na kumtambua Mola wake, siku zote, hatima ya udadisi na utafutaji huo humalizikia kwa Mola Mtakatifu, kwa hiyo udadisi na utafutaji huo ni lazima ufanywe kwa mujibu wa mapendekezo ya mwanaadamu mwenyewe.
Ufafanuzi huo wa dini ulioelezewa hapo juu hautoshelezi, kwa sababu, (ingawa) Mwenyeezi Mungu anayekusudiwa ni yule Mwenyeezi Mungu aliye katika nyoyo za wanaadamu, na hii inaonyesha nafasi ya mwanaadamu katika dini, hali ya kwamba maudhui ya dini ni mwanaadamu, na nafasi ya dini kwa mwanaadamu sio Mwenyeezi Mungu tu, bali kuna mambo mbali mbali yaliyo muhimu kwa mwanaadamu.

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu ufafanuzi wa dini , na tukaashiria baadhi ya vidokezo ambavyo vinahusiana na mada hiyo ya dini katika makala hii vile vile tutaendelea kuelezea vidokezo hivyo vinavyohusiana na umuhimu wa dini katika jamii ya wanaadamu.
Ili kutambua umuhimu wa dini ni vyema tukaashiria baadhi ya vidokezo vinavyohusiana na ufafanuzi na umuhimu wa dini kwa walimwengu na jamii kwa ujumla.
Vidokezo kuhusiana na ufafanuzi wa dini.
Kidokezo cha kumi:

Uhusiano unaopatikana katika dini sio uhusiano baina ya mwanaadamu na Mwenyeezi Mungu tu, bali katika dini kuna uhusiano mbali mbali, uhusiano wa mwanaadamu mwenyewe na nafsi yake,uhusiano wa mwanaadamu na mwanaadamu, uhusiano wa mwanaadamu na jamii, binaadamu na ulimwengu, binaadamu na hali halisi ya duniani na Akhera, mwanaadamu na walimwengu tofauti,mwanaadamu na hali halisi kuhusiana na ukweli, uhakika, na haki ya dini, na hatimae uhusiano wa mwanaadamu na Mwenyeezi Mungu, yote hayo yamezunguka taaluma na hukumu za dini. Kwa sababu uongofu na saada ya kila mwanaadamu inatokana na nidhamu ya mambo hayo, hivyo kama hapakuzingatiwa mambo hayo hapatakuwa na uwezekano wa kupata saada na uongofu.

Ufafanuzi wa dini kwa mtazamo wa John Lark:

Dini ni amri inayohusiana na hisia za dhati za nafsi ya mwanaadamu, na uhusiano wake baina yake na Mola muumba. Ufafanuzi huo pia sio sahihi na haukubaliki. Kwa sababu; dini sio uhusiano baina ya mwanaadamu na Mwenyeezi Mungu tu, bali katika dini mbali ya uhusiano huo kuna uhusiano na mambo mengine mbali mbali yanayoleta uhusiano ndani ya dini. Hivyo ufafanuzi huo sio sahihi kwani umetolewa kutokana na mabainisho mbali mbali yanayohusiana na dini, na haujatolewa kutokana na mabainisho ya haki na ya uhakika ya dini.

Kidokezo cha kumi na moja:-

Ikiwa dini ni mfumo na muongozo kwa ajili ya kuwaletea wanaadamu saada na uongofu, basi ni lazima iwe na nafasi kubwa katika kudhamini na kutekeleza mahitajio ya wanaadamu na viumbe vyote kwa ujumla, ni dini peke yake ndiyo inayoweza kudhamini kwa kumuelewesha na kumridhisha mwanaadamu katika nyanja zote maishani mwake, kielimu, kifikra, kiitikadi n.k. tukisema kuwa ni dini peke yake ndiyo inaweza kumuelewesha mwanaadamu maamrisho ya Mola wake haimaanishi kuwa uhakika na hali halisi yote ya dini ni yenye kuhisiwa. Na tukisema kuwa akili na nafsi ya mwanaadamu inaweza kufahamu hali halisi ya dini, haimaanishi kuwa wanaadamu hawana uwezo wa kufahamu hukumu na maamrisho ya dini ya Mwenyeezi Mungu.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini