Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UFAFANUZI WA DINI NO.4

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UFAFANUZI WA DINI NO.4

Ufafanuzi wa dini:-

Dini ni udadisi na utafutaji wa mwanaadamu kwa ajili ya kumfikia na kumtambua Mola wake, siku zote, hatima ya udadisi na utafutaji huo humalizikia kwa Mola Mtakatifu, kwa hiyo udadisi na utafutaji huo ni lazima ufanywe kwa mujibu wa mapendekezo ya mwanaadamu mwenyewe.

Ufafanuzi huo wa dini ulioelezewa hapo juu hautoshelezi, kwa sababu, (ingawa) Mwenyeezi Mungu anayekusudiwa ni yule Mwenyeezi Mungu aliye katika nyoyo za wanaadamu, na hii inaonyesha nafasi ya mwanaadamu katika dini, hali ya kwamba maudhui ya dini ni mwanaadamu, na nafasi ya dini kwa mwanaadamu sio Mwenyeezi Mungu tu, bali kuna mambo mbali mbali yaliyo muhimu kwa mwanaadamu.

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu ufafanuzi wa dini , na tukaashiria baadhi ya vidokezo ambavyo vinahusiana na mada hiyo ya dini katika makala hii vile vile tutaendelea kuelezea nadharia za watu tofauti zilizotolewa kuhusiana na ufafanuzi wa dini

Baadhi ya watu wameifafanua dini kwa mtindo huu:-

Dini ni kuwa na imani na yale ambayo elimu inajizuilia kuyakubali.[1]

Kwa sababu dini haina hofu na tajiriba, na nafasi ya tajiriba haiwezi kuitoa dini katika nafasi yake (ambayo haina upeo) na dini inaendana sambamba na fikra kiakili, ufahamu wake na tajiriba ya taaluma zake, kwa maelezo zaidi tunaweza kusema hivi:-

1. Ikiwa mwanaadamu ni mtiifu (mwenye kutii) wa amri za Mola wake, na ikiwa utii fu huo ndio unaompatia yeye uongofu na saada, na ikiwa utiifu huo hauwezi kupatikana wala kukubalika bila bila ya kuwa na uwezo kielimu, basi dini ni lazima iweze kudhamini mambo ya elimu yanayoendana na nguvu za utiifu wa mwanaadamu, na hii ina maana ya kuwa, elimu yenyewe ni sehemu ya dini, na sio nyenzo kwa ajili ya dini au inatengana na dini.(yaani elimu tukijaalia kuwa ni nyenzo ya dini (hali ya kwamba sio nyenzo) basi haitengani na dini).

2.Ikiwa mwanaadamu ni kiumbe mwenye uhakika aliye na uhusiano na kila kiumbe, na ikiwa nafsi ya mwanaadamu ni yenye kunufaika na mambo mbali mbali maishani mwake, na kila jambo likiwa na elimu yake mahasusi, basi elimu ya mwanaadamu kwa namna fulani ina uhusiano na inasaidiana na mambo ya elimu nyengine.

3.Ikiwa dini mbali ya mabainisho ya sheria na hukumu za dini ina wadhifa wa kubainisha haki na uhakika, na ikiwa kila uhakika ni sadikisho la elimu, basi mabainisho yoyote yale ya dini kwa hakika ni mabainisho ya elimu ya dini yaliyoelezewa kupitia elimu, kwa hiyo dini na elimu ni vitu viwili visivyo tengana, kwa sababu elimu ni sehemu ya dini.

A:Kuifafanua dini kwa mtindo kama huo, kwa hakika ni kuitoa dini thamani, na kuifanya dini hiyo iwe iko katika milki ya mwanaadamu, (na sio milki ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu), kwa sababu dini ambayo ina upeo wa hali ya juu na iliyokusanya uhakika wa kila kitu, hukumu, maamrisho, makatazo, n.k. sio jambo la kawaida kwa dini ambayo ina sifa kama hizo kuwa katika uwezo au milki ya mwanaadamu, Hivyo maelezo hayo yaliyoelezewa kuhusu dini sio sahihi bali ni jitihada zilizofanywa na baadhi ya wanaadamu waliokuwa wana makusudio ya kuipotosha na kuiharifu dini tukufu ya Mwenyeezi Mungu, na hizo ni fikra potofu zilizotolewa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuitoa thamani dini, na kufanya hivyo ni kuitenganisha dini na elimu, na kuibagua elimu na dini, na hilo sio jambo linalowezekana na haliko katika uwezo wa wanaadamu.

B: Dini ambayo haina elimu wala haina nafasi yoyote katika taaluma au elimu tofauti kwa hakika hiyo sio dini, kwa hiyo dini ambazo hazina uwezo wa kubainisha haki au uhakika wa mambo na zikitizamwa katika udhahiri wake hufikiriwa kuwa ni dini kwa hakika hizo sio dini, dini ya haki na yenye uhakika ni dini ya Mwenyeezi Mungu tu, dini ambayo inaweza kuwakidhi na kuwatimizia wanaadamu katika mahitajio yao yote.

C: Ingawaje kwa upande mmoja, dalili zinazosimamishwa kuhusiana na Imamu Mahdi Ajjala llahu Taala Sharifu kuwa nje ya jamii ni kule watu (wanajamii) kuwa bado hawako tayari kukabiliana na mfumo wa serikali kamili ya Kiislamu, au vile vile wao kutokana na baadhi ya ubedui wa watu, Imamu (a.s) anaweza akazuriwa ikiwa ataingia katika jamii, lakini vile vile kuna dalili nyingi za kiakili na kielimu kuhusiana na hilo zinazothibitisha kuwa Imamu ni lazima awe nje ya jamii, kwa mtazamo wa baadhi ya watu, Imamu ni lazima awe hai (awepo) na karibu ya wanaadamu ili atimize wadhifa wake wa kuwaongoa na kuwaonyesha wao njia ya haki itakayowafikisha katika saada, na hii ni kwa sababu mwanaadamu anahitajia nyenzo ambazo zitamfikisha yeye katika daraja ya juu, (kumtambua Mola wake mtakatifu), daraja ambayo ndio nyenzo ya kumletea yeye saada na mafanikio ya duniani na akhera. Kutokuwa na imani au akida na Maimamu (a.s) katika kuwatii na kuukubali muongozo wao katika jamii ni madhara na dharari kubwa inayowafika wanaadamu na jamii kwa ujumla, na kuwaondoa Maimamu (a.s) katika jamii kunaleta madhara kielimu,kwa sababu ikiwa mwanaadamu hatonufaika na elimu ya Maimamu hao, basi mwanaadamu huyo hataweza kuongoka wala kufikia katika saada, na elimu ya Maimamu (a.s) ndiyo nyenzo pekee inayomsaidia mwanaadamu katika kumtekelezea mahitajio yake, kumuongoza na kumfikisha katika saada ya duniani na akhera.

D: Maimamu na Ahlulbayt (a.s) wana majukumu mengi katika jamii, miongoni mwa majukumu hayo ni kwamba; iwapo wataulizwa masuala na wanajamii, wana wadhifa wa kuyajibu masuala hayo kutokana na elimu waliyonayo, (elimu ambayo wamepewa kutoka kwake Yeye Mola Mtakatifu), na mwanaadamu anapohitajia kupata ufumbuzi wa mambo Fulani kuhusiana na dini yake au mambo mengine tofauti, ni lazima asikilize na apate jawabu ya haki na ya uhakika, na baada ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni Maimamu (a.s) pekee ndio waliyo na elimu hiyo ya haki, hivyo ni lazima kwa mwanaadamu kuitambua haki, kwa sababu iwapo hataitambua haki au kupata majibu na mabainisho ya masuala yake kupitia mtu mwengine hataweza kupata natija yoyote mbali ya shaka itakayokuwa inamuadhibi au kumuudhi katika nafsi na akili yake (kwa sababu ya wasiwasi atakaokuwa nao, ya kuwa hivi kweli jawabu aliyolipata ni sahihi na ina uhakika au vipi)?.

E: Katika kipindi cha ughaibu wa Imamu (a.s), (kutokuwepo Imamu (a.s)), wanaadamu wameachiwa rasilimali na urithi wenye thamani ya juu, urithi huo ni elimu ya dini na matini za kidini, kwa hiyo mwanaadamu anapohitajia au anapotaka kunufaika na elimu hizo, ni lazima kufanya jitihada ili kuzipata na baadae kuzitumia kwa mujibu inavyotakiwa, au kuzifanyia tajiriba ili kuona mafanikio yake.


[1] Uhusiano wa elimu na dini, doctor Bahnar, uk 10.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini