Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MALINGANIO YA MITUME NO.1

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALINGANIO YA MITUME YA ALLAH (S.W)

*Namna ya kuwalingania watu ni maneno mazuri yenye hekima yanayoweza kumtoa nyoka pangoni, seuze yawe ni ya akili pia, na imeelezewa katika Aya ya 253 ya suratul-baqarah, na katika Aya ya 90 ya Surat Al-An-aam namna gani Mwenyeezi Mungu anavyowafadhilisha hao Mitume waliokuwa kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w.w.).

تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلـٰي بَعْضٍ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللّهُ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ وَآتَيْنَا عِيسَي ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَاَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـكِنِ اخْتَلَفُواْ فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا اقْتَتَلُواْ وَلَـكِنَّ اللّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ[1]

MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.

*Aya hii inaonyesha kuwa Mitume, daraja zao ni mbali mbali kwa Mwenyeezi Mungu, kama binaadamu wengine na Malaika na Majini na vinginevyo, wanazidiana kwa fadhila za Mwenyeezi Mungu na kwa amali zao, walizofanya ambazo si sawa sawa, za wengine ni kubwa zaidi au nyingi zaidi kuliko za wenziwao. Na hapa Mwenyeezi Mungu amewataja watatu katika hao Mitume wakubwa kabisa, naye ni huyo aliyesemezwa na Mwenyeezi Mungu, naye ni Nabii Mussa (a.s), aliyepewa hoja zilizo wazi,.. naye ni Nabii Issa (a.s) Aliyepandishwa vyeo vikubwa kabisa, Naye ni Nabii Muhammad (s.a.w.w). na vile vile katika hao wakubwa kabisa ni Nabii Ibrahimu na Nabii Nuhu (a.s) kama ilivyofahamishwa katika Aya nyenginezo kama aya ya 7 ya surat Ahzaab inavyosema. Na anayewekwa mbele katika hao ni Nabii Muhammad, kisha Nabii Ibrahimu, Nabii Mussa, Nabii Issa, na hatimae Nabii Nuhu (a.s). Na huyo roho mtakatifu ni Jibraiyl anayewaletea Wahyi Mitume.

Na aliposema Mwenyeezi Mungu, na kama Mungu angalitaka, ni kuonyesha kuwa Mwenyeezi Mungu hakuumba wanaadamu umbo la Malaika, na kama angelitaka angeliwaumba hivyo(Kimalaika), wakawa wanakwenda mwendo ule ule waliowekewa, hawakhalifu hata kidogo, ikawa wanafanya mema tu. Lakini binaadamu kawaumba akawapa uhuru wa kufanya jema na baya,na angelitaka kuwaumba kimalaika asingelishindwa, lakini Mwenyewe Mwenyeezi Mungu katafautisha baina ya viumbe vyake- Malaika kawaumba wana akili na hawana matamanio, akawaumba wanyama kuwa wana matamanio lakini hawana akili, (wana utambuzi mdogo tu), na akawaumba wanaadamu nayote mawili, wana matamanio na akili ya kupima baina ya jema na baya, na baina ya jema na jema zaidi, na baina ya baya baya zadi,- wafanye wanalolitaka, bila ya kufungika kwa moja wapo, na hayo matamanio yao ndiyo yanayowapelekea kutowafikiana, na angelitaka Mwenyeezi Mungu asingeliwaumba hivi, basi mwanaadamu akapigana na matamanio yake akafika katika utakatifu unaokurubia wa kimalaika, hua bora kuliko hao Malaika, na akitawaliwa na matamanio yake anakuwa kama mnyama, au zaidi kuliko mnyama, kwani yeye ana hatamu ya akili, naye hataki kuzuilia kasi zake kwa hatamu hizo.

Na katika Surat Al-An-aam anasema:-

اُوْلَـئِكَ الَّذِينَ هَدَي اللّهُ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ قُل لاَّ اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ اَجْراً إِنْ هُوَ إِلاَّ ذِكْرَي لِلْعَالَمِينَ[2]

Na waheshimiwa walio kufuru katika kaumu yake wakasema: Mkimfuata Shua'ib, basi hakika hapo nyinyi mtakuwa mlio khasiri.

Katika sehemu hii tutabainisha baadhi ya njia walizotumia Mitume katika kuufikisha ujumbe wa Mola wao.

[1] Suratul-Baqarah Aya ya 253

[2] Surat Al-An-aam Aya ya 90

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini