Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MALINGANIO YA MITUME NO.2

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALINGANIO YA MITUME YA ALLAH (S.W) NO.2

*Namna ya kuwalingania watu ni maneno mazuri yenye hekima yanayoweza kumtoa nyoka pangoni, seuze yawe ni ya akili pia.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu ilitumia njia mbali mbali katika kufikisha ujumbe wa Mola wao. miongoni mwa hizo ni:-

 a) KUONYA NA KUTOA HABARI NJEMA.

Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu iliwalingania watu na kufikisha ujumbe wao kwa kuwaonya na kuwabashiria habari njema, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلاَّ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ وَاتَّخَذُوا آيَاتِى وَمَا اُنذِرُوا هُزُواً[1]

Na hatuwatumi Mitume ila wawe wabashiri na waonyaji. Na walio kufuru wanabishana kwa uwongo, ili kwa uwongo huo waivunje kweli. Na wanazifanya Ishara zangu na yale waliyo onywa kuwa ni mzaha.

Wanaadamu wana hadafu na madhumuni yao katika kutafuta maendeleo ya maisha yao ya kila siku, Kwa sababu  hiyo basi tunaweza kufupisha madhumuni ya wanaadamu katika sentensi mbili fupi zifutazo:-

1)kutafuta manufaa.

2)kujikinga na madhara.

Kwa hiyo hofu aliyonayo mwanaadamu ndiyo inayomuonya, na mategemeo aliyonayo mwanaadamu ndiyo yanayompongeza, na kumpa utulivu na mafanikio katika maisha yake ya duniani na Akhera, na faida na athari zote hizo humletea baraka kutokana na hofu na mabashirio mema aliyonayo mwanaadamu huyo, katika sehemu hii tutaelezea vipengele viwili hivyo, kila kimoja kwa upande wake.

1. KUONYA.

Neno (inzaar) lina maana ya kuonya, yaani kuonya na kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu, pamoja na kuwahofisha kutokana na adhabu ya siku ya kiama,  kwa sababu madhara humfanya mwanaadamu ahisi hatari katika maisha yake, basi hii ni dalili bora itakayomfanya mwanaadamu huyo awe makini katika kutimiza wajibu wake aliyopewa na Mola wake, na kwa sababu hiyo basi Mitume ilifikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa watu kwa kuwabashiria habari njema na kuwatahadharisha na kuwatia hofu kutokana na adhabu kali ya Mwenyeezi Mungu, adhabu ambayo wataipata kutokana na kufuru au madhambi waliyoyafanya, kama tunavyoona katika Surat Muddathir:-

يَا اَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ. قُمْ فَاَنذِرْ[2]

Ewe uliye jigubika! . Simama uonye! .

Kwa kuzingatia aya hiyo, tutafahamu kuwa hadafu ya mwanzo ambayo Qur-ani imebainisha ni kuonya na kuzindua kutokana na kughafilika usingizini, kama inavyosema Qur-ani:-

قُلْ اَيُّ شَيْءٍ اَكْبَرُ شَهَادةً قُلِ اللهِ شَهِيدٌ بِيْنِى وَبَيْنَكُمْ وَاُوحِيَ إِلَيَّ هَذَا الْقُرْآنُ لاُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ اَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ اَنَّ مَعَ اللهِ آلِهَةً اُخْرَي قُل لاَّ اَشْهَدُ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِى بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ[3]

Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia.

Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha.

[1] Suratul-Kahf Aya ya 56

[2] Surat Muddathir Aya ya 1-2

[3] Surat Al-An-aam Aya ya 19

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini