USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI)
USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI)
5- USHAHIDI WAHADITHI YA SAFINA (JAHAZI)
Katika kitabu cha Kisunni : kiitwacho Mustadrak Sahihein kimeeleza kua imesimuliwa na Hakim kupitia kwa Hanash Al- Kanani ambaye alisema: Nimemsikia Abudhar Al-Ghafari akisema wakati ambapo alikuwa ameushika mlango wa Ka'ba Tukufu: "Enyi watu, wale wanaonijua mimi ni nani hawanahaja ya kupewa habari kwa wao wananijua, lakini wale wasionijua na wajue kuwa mimi ni Abudhar (Sahaba wa Mtume). Nimemsikia Mtume (s.a.w.w) akisema: "Mathalu AHLULBAYTII FIIKUM MATHALI SAFIINATIN NUUH, MAN RAKIBAHA NAJAA, WA MAN TAKHALLAFA ANHA GHARIKA". - "Mfano wa Ahlul Bayt wangu ni kama Jahazi ya Nuuh (a.s). Kila aliyeipanda aliokoka, na kila aliyejiepusha nayo aligharikishwa (alizama)".
Mwanachuoni wa Kisunni Hakim amesema kwamba hadithi hii ni Sahihi. Pia hadithi hii ya Safiina imesimuliwa na mamia ya wanazuoni wa Kisunni katika vitabu vyao. Umewahi kumsikia mwanazuoni yeyote wa Kisunni akiizungumzia hadithi hii kwenye hotuba yake? Kama hujawahi , basi wanazuoni hao wanaificha. Lakini unaweza kurejea vitabu vifuatavyo vya Kisunni na utaipata hadithi hii: • Al-Haakim katika kitabu chake Mustadrak, Juz. 2, Uk. 343. Sawaiq Muhriqah, Uk. 153. Faraid Simtein, Juz.4,Uk. 149. Mustadrak Sahihein, Juz.3, Uk. 343. Nuurul Absaar, Uk. 126, na vitabu vingine vingi tu.
Waislamu waliotaka kunusurika na moto wa Jahanamu siku ya Kiyama waliwafuata Ahlul Bayt - Imam Ali (a.s), baada ya kuondoka kwa Mtume. Ni sababu gani inayotufanya tusiwafuate Ahlul Bayt baada ya Mtume na hali ya kuwa Ahlul Bayt ni safina ya Nuuh (a.s)? Kwa hakika, hatutaki kuwa kama mtoto wa Nuuh (a.s) ambaye juu yake Qur'an inasema: " ---- na Nuuh alimwita mwanawe, na alikuwa peke yake. Ewe mwanangu! ingia (ndani ya Jahazi) ili uwe pamoja nasi na usiwe miongoni mwa makafiri (wasio amini). Alisema nitakimbilia mlimani, mlima ambao utanilinda dhidi ya maji. Nuuh akasema hakuna mlinzi leo atakayekulinda dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule mwenye kurehemewa (ndiye atakaye epukana na adhabu). Kisha wimbi likapita kati yao, hivyo akawa ni miongoni mwa waliogharikishwa (waliozamishwa)". Rejea Surat (Huud 11:41-43).
Ni nani atakayetuokoa dhidi ya gharika ikiwa hatutoingia katika jahazi / safina ya Ahlul Bayt? Tunamuomba Allah (swt) atunusuru na gharika tusiwe kama alivyokuwa mtoto wa Nuuh. Amin
MWISHO