Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

DALILI ZA KUKOMA UTUME

0 Voti 00.0 / 5

DALILI ZA KUKOMA UTUME

Utangulizi

Imani juu ya mitume wote na kukubali risala zao ni jambo la dharura,na kwa kumpinga mmoja kati yao au kupinga moja kati ya risala zao ni sawa na kupinga uungu wa Mungu na inakuwa  ni sawa na kufru aliyofanya iblisi. Kwa hivyo  risala ya mtume wa uislamu, pamoja na kumuamini na kuamini aya alizoteremshiwa,ikiwa ni hukmu na kanuni toka kwa muumba ni jambo la dharura.

Lakini kuwaamini mitume hakuendi sambamba na kufuata sheria zao,mfano; waislamu wanaamini mitume wote na vitabu vyao, lakini kwa hali hiyo hawatakiwi na wala si sheria kwao  kufuata sheria za mitume waliotangulia. Hivyo ni wadhifa wa kila umma kufauta sheria za mtume aliyetumwa kwao. Kwa kuwa mtume hakuja kwa ajili ya baadhi ya watu(waarabu), na baada yake hakuna mtume mwengine aliyekuja kufuta mafundisho yake,basi kwa hali hio dini aliyokuja nayo yaani uislamu ni dini ya ulimwengu mzima.

kwa minajili hiyo, ni lazima tulithibitishe swala hili, kisha tuliangalie swala la kukoma  utume na sababu zake,kwa kuwa uislamu ni dini ya milele,kunafuata hoja ya kuwepo mtume mwingine atakayefuta sheria za kiislamu.

Dalili katika Qur’an:

Qur’an ndio njia sahihi na bora zaidi katika kuthibitisha jambo hili,na mtu akipitia kitabu hiki hata kwa haraka haraka atagundua kuwa wito uliomo ndani ya kitabu ni wito wa kila mtu,yaani wa jumla na kamwe haukukomea kwa watu mahususi,aya nyengine zinaanza kwa kusema; “Enyi watu”1 , “Enyi wana Adamu”2

Na uongofu wake umeenea kwa wote kama itumikavyo lafdhi ya “watu”3 au “ulimwengu”4    na vile vile inapozungumzia wafuasi wa dini nyingine hutumika lafdhi ya “Ahli kitaab”5 yaani watu wa kitabu,na has kama tujuavyo lengo la kushuka Qur’an ni kushika hatamu kwa dini ya kiislamu dhidi ya dini nyinginezo. 6 aya hizi zinaondoa shaka juu ya kuwa uislamu ni dini ya daima nay a ulimwengu na kadhailka kitabu kitabu cha Qur’an ni kwa ajili ya watu wote.

Uislamu ni wa daima.

Aya tulizotaja zinathibitisha jambo hili kwa kuwa mara zote zinazungumzia juu  ya watu na wana wa Adamu na ziwazungumziapo wasio waislamu zinaanza na ahlul kitaab,hii ni dalili ya wazi ya kuthibitisha kuwa uisalmu ni wa dunia nzima na ndio wenye kudumu,na vile vile aya isemayo  liyudh-hirahu alaa diini kullihi “ili ishinde dini zote”. Ili idhihiri juu ya dini zote , iwe na (khatamu). Hakuna tena shaka itakayobaki juu yake,pia tunaweza kutumia dalili ya aya isemayo;

“bila shaka ni kitabu chenye kuheshimika. Hautafikia upotevu mbele yake wala nyuma yake,kimeteremshwa na mwenye hekima,mwenye kuhidimiwa”

Hiki ni kitabu ambacho katu hakina shaka ndani yake,hakuna batili itakayoingia ndani yake si zamani wala sasa.

Na ni dalili kuwa Qur’an katu haitaweza kupoteza ukweli iliyonao ,na pia inaondoa uwezekano wa kuwa na mtume mwingine atakayekuja kufuta sheria za uislamu nakuja na sheria mpya. Na hatimae ikawa ni kukoma kwa utume kwa mtume Muhammad. Pia zimepokewa haditi nyingi kuhusiana na suala hili isemavyo moja ya hadithi kuwa:

“Halali  ya Muhammad ni halali tu mpaka siku ya kiyama na haramu yake ni haramu mpaka siku ya kiyama”. Jambo aliloliharamisha yeye ni haramu mutlaq mpaka siku ya kiyama,na pia jambo alilolihalalisha yeye ni halali mpaka siku ya kiyama. Mitume wengine waliopita  walikuwa wanakutana katika zama moja mfano wa Nabii Lut aliteuliwa katika zama za Nabi Ibrahim ingawa hakuw na sheria na alifuata sheria za Nabii Ibrahim na mara nyingen baada ya mtume aliyepewa sheria waliteuliwa mitume wengine na kufuata sheria zile zile,kutokana na hali hii inatulazimu suala la kukoma kwa utume kuwa kwa Nabii Muhammad(saw) lazima tulizungumze kwa peke yake ili kusibaki wasi wasi wa kutokea mtume atakayefuata sheria za Muhammad(saw).

Ushahidi wa Qur’an na suala la kukoma kwa Utume.

Misingi ya kiislamu inatuonyesha kuwa utume unakomea kwa mtume Muhammad(saw) na hakuna tena mtume atakaye kuja baada yake,na hata wasio waislamu wanajua kuwa huu ni mmoja katika misingi ya uislamu kama dharura nyingine za dini ni suala lililohitaji dalili za kina,kwa hiyo tunaweza kutumia Qur’an na hadithi katika kulizungumzia suala hili. Qur’an inasema;

“Na Muhammad si baba katika ya wanaume wenu bali ni mtume wa mwenyezi Mungu na mwisho wa mitume”,baadhi ya maadui wa uislamu ayah ii wameishakia katika Nyanja mbili; Nyanja ya kwanza neno khatim Neno Khatam  ni neno la kiarabu lenye maana ya pete, na katika ayah ii limetumika kwa maana io hio. Nyanja ya pili; kama ikiwa khatam imetumika hapa ikiwa na maana ya kufunga,lengo ni kuwa Mtume Muhammad ni kifuungfa cha mitume wote na hapatakuwa na mtume mwengine baada yake. Majibu ya hoja ya kwanza ni kuwa khatam inamaana ya kufunga kitu.

“kama inavyotumika kufunga kitu”

Pete iliitwa khatam kwa sababu ilikuwa ikitumika barua na vitu mfano wa hivyo. Na katika Nyanja ya pili ni kwamba kila mtume aliyekuwa ni Rasuli basi pia ni Nabii ingawa mafhum ya neno Nabii  ni kubwa kuliko neno Rasul.

Ushahidi wa Hadithi na Suala la kukoma Utume.

Suala la kukoma utume limezungumziwa sana katika hadithi ikiwemo hadithi ya manzila ambayo ni miongoni mwa hadithi zisizokuwa na shaka na zimepokelewa kwa sanad ya mutawaatir toka kwa mtume akisema wakati akielekwa katika vita vya Tabuuk,alimuacha imam Ali Madina ili asimamie mambo ya waislamu wakati wa kutokuwapo kwake,wakati ikimkabidhi jukumu hilo la kusimamia mambo ya waislamu akasema:

“Je! Huridhiki kuwa daraja yako kwangu ni kama Harun kwa Musa ila hakuna nabii baada yangu”11. Na katika riwaya nyingine bwana mtume alisema:

“Enyi watu,juweni kuwa kwa hakika hakuna mtume baada yangu na wala hakuna umma baada yenu”12

Vile vile katika hadithi nyengine asema: “Na wala hakuna sunna baada ya sunna yangu”13

Mara nyingi tusomapo katika dua na ziara za Maimamu tunakuta hali hii inajionyesha kwa uwazi na suala hili linazungumziwa kwa urefu zadi.

Siri ya Kukoma Utume.

Kuna hekima nyingi katika kuwa mitume wengi kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu kama tutakavyoona baadhi ya hekima za kuwapo na mitume wengi na wanaofuatana,kwanza ilikuwa ni taabu kwa mtum mmoja kuweza kueneza mafunzo ya mwenyezi Mungu katika maeneo yote.

Pili kwa kubadilika kwa mazingira kwa mambo mbalimbali yalilazimu pia kwa kanuni kubadilika au kuletwa upya,pia kutokana na watu majahili kuingilia katika swala la mafunzo yalitokea mabadiliko katika sheria za muumba ambapo yalilazimu awepo mtu sahihi wa kuweza kuyarekebisha na kuondoa yale yote yaliyoongezwa au kupunguzwakatika sheria za Allah(swt). Kwa hivyo ikiwa hali halisi ya kimazingira inaruhusu mtu mmoja kuweza kusambaza hukumu za Allah(swt) katika kila kona ya dunia akisaidiwa na wafuasi na viongozi baada yake,na kanuni alizonazo zikaweza kumaliza na kutatua matatizo yaliyopo katika zama za sasa na zinazokuja,na kukawa na umakini katika kutatua mambo yanayojitokeza katika zama zijazo na pia kukawa na uhakika wa kuhifadhika kwa kitabu na sheria hizo hakutakuwa tena na haja ya kuletwa mtume mwingine. Amma kwa kuwa elimu ya kawaida ya mwanadamu haiwezi kubainisha yote haya,na ni mola pekee ajuwaye ni zama gani zinafaa kuwa na mtume wa aina hii kutokana na elimu yake isiyo na mwisho na ndiye pekee awezae kubainisha suala la kukoma kwa mtume. Lakini kukoma kwa utume haina maana ya kukoma kwa uhusiano baina ya muumba na viumbe wake. Mwenyezi Mungu huwa na na mawasiliano na viumbe wake kwa wakati wowote atakao kwa kutumia elimu ya ghaibu hata kama si kwa njia ya wahyi kama aliyokuwa akiwaleta mitume,elimu ambayo hata maimamu maasumina walikuwa nayo.

Kutokana Na maelezo haya tumepata natija kwamba:

Mtume wa uislamu kwa kusaidiwa na wafuasi na viongozi baada yake umeweza kuenea ujumbe wake  katika kila kona ya dunia,kitabu alichonacho kimelindwa kutokana na kila aina ya upotevu na iwe kwa kupunguza yaliyomo au kuzidisha  lisilokuwamo, na tatu kitabu chake kinauwezo wa kutatua matatizo ya sasa nay a baadaye ya kilimwengu. Lakini yawezekana mtu akatoa hoja kwa njia kama hii;kama ilivyokuwa zama zilizopita mabadiliko mbalimbali yalijitokeza  katika Nyanja za kijamii,uchumi yalihitaji kupatikana kwa hukmu mpya au kurekebisha zilizopo, na kwa sababu hii waliletwa mtume wengine, na tangu kuja kwa uislamu yameshatokea mabadiliko mengi katika Nyanja mbalimbali,je iweje mabadiliko haya yasiambatane na sheria mpya? Tunaweza kutoa majibu kwa kusema kwamba;kama ilivyoonyeshwa,suala la kubadilika kwa kanuni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi ni suala ambalo haliendani na akili ya mwanadamu wa kawaida,kwa kuwa sisi hatuna ujuzi na maarifa juu ya utoaji wa kanuni ila kutokana na kuwa uislamu ni wa milele na wa dunia nzima tunaweza kusema kutokana na hali hii hakuna haja ya kuwa na mabadiliko katika kanuni zake. Hatupingani na madiliko yanayojitokeza siku hadi siku  bali uislamu tayari ulishaweza kanuni na sheria za jinsi ya kutatua hali hizo pindi zinapojitokeza, na haya yameelezwa wazi katika vitabbu vya Fiqhi na vile vinavyozungumizia maswala ya wilayat faqiih.

 

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini