Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

IMAM RIZA (A.S)

0 Voti 00.0 / 5

IMAM RIDHWA (A.S), MUHSTASARI WA MAISHA YAKE

Jina: Ali bin Musa.

Majina: Ridha, Zamin -e- Thamin , Gharibul Ghuraba , Alim e Ale Muhammad.

Kuniyya: Abul Hasan.

Tarehe ya Kuzaliwa: 11 Dhul Qaada .

Mama: Bibi Suttana (au Najma au Ummulbanin).

Baba: Imam Musa Al- Kadhim (a.s.)

Kifo: 29 Safar 203 Baada ya Hijira (kwa kupewa Sumu na Maamun Rashid).

Alikozikwa: Mashhad, Iran.

Wazazi wake & Uzazi

Mama: Alikuwa mtumwa wa Ummu Hamida (Mke wa Imam wa sita). Wakati Imam wa Saba (7) alipokwenda kumnunua kutoka kwa mfanyabiashara wa watumwa, wakati yeye alikuwa anakuja Madina akitokea Marrakesh mwanamke Mkristo mchamungu alimwambia kuwa; Bibi Suttana alikuwa mtumwa wa pekee sana ambaye atakuja kuzaa mtoto ambaye ataeneza neno la kweli kutoka Mashariki kwenda Magharibi.

Ummu Hamida alimuota Mtume (SAWW), katika ndoto  akimwambia amtoe mwanae  Bibi Suttana kwa Imam Musa Kadhim (as) na ndivyo alifanya. Imamu wa Sita (6) alikuwa akiwaambia wafuasi wake wasubirie kuzaliwa kwa mjukuu wake ambaye alikuwa kimtambulisha kwa jina la  Alim (Mwanchuoni) wa nyumba ya Muhammad. Yeye Imam Ridwa alikuwa mmoja katika Maimamu watatu ambao walifanya Jihad kwa elimu na maarifa yao. (Wengine wawili walikuwa Imamu wa Tano (5) na 6). Imam Ali Ridhwa (as) alizaliwa mwezi mmoja baada ya mauaji ya babu yake Imam Jaffar Sadiq (as) alizaliwa wakati wa utawala wa Harun Rashid ambaye alimuua kwa sumu baba yake.

Baba: Imam Musa Al- Kadhim (a.s.)

Majina yake mengine; Ridhwa, Malaika, Nabii, Aimma , Muumini na hata maadui wa Ahlul- Bayt walimkubali kwa kiasi kwamba Mamun Rashid alikubali na kumtaka yeye kuwa mrithi dhahiri (kwa kuwa kiongozi baada yake). Na miongoni mwa majina yake ni Imamu Zamin-e-Thamin maana nane. Zamin maana Ulinzi na usalama. Moja ya matukio ya kuhusishwa na jina hili ni kwamba siku moja Imamu alikuwa anapita katika soko na wafuasi wake wachache alipoona mwindaji akitaka kumuua paa wakike aliyekuwa akitaka kujinasua katika mateso ya mtego. Imamu alimwambia Muwindaji basi muachia paa huyu kwani anataka kwenda kuwalisha watoto wake wawili waliopo porini na kisha akishawalisha atakurudia na wewe utamuua. Wawindaji walidhani anafanya mzaha. lakini Imamu alisimama kidete mpaka wakamuachia, kisha punde kidogo Paa alirudi akiwa na watoto wake wawili na kuwakabidhi kwa Imamu akimtaka awaangalie. Sisi tunaamini kwamba kama kuna mtu ambaye ana kwenda katika safari chini ya ulinzi wa Imamu yeye atakwenda na kurudi salama.

Jina jingine ni Gharibul Ghurabaa (Mmoja ambaye ni mgeni yaani yeye yu mbali na mji wake). Imamu alikuwa mbali na nyumbani kwake na familia na ni yeye Imamu pekee ambaye alizikwa nje ya Iraq na Hijaz (Saudi Arabia).  Jina lingine ni Alim Aali Muhammad (Mwanzuoni katika watu wa  Muhammad). Jina hili alipewa na babu yake (Imam Jaffar Sadiq (as ).

Maisha na Kazi: Imamu alitekeleza jukumu muhimu kabisa la kuelimisha Waislamu. Kuweka mifano ya elimu kupitia mwenendo wa tabia yake mwenyewe .

Alishuhudia kipindi kifupi cha utawala wa Harun Rashid ambaye alimuua baba yake. Harun Rashid pia alijaribu kumuua Imamu Ali Ridha (as) lakini hakufaulu. Baada ya kifo cha Harun wanawe, Amin na Mamun walipigana kwa kutaka utawala kwa nguvu. Mamun alishinda kwa kumuua nduguye Amin.

Mara baada ya Mamun kuwa Khalifa, kulingana na mila iliyoanzishwa na Muawiya, alitakiwa kutaja jina la mrithi (mrithi dhahiri). Mamun alimwita Imamu kuja mji wake mkuu Marw kwa kutuma mjumbe kwenda Madina kumleta Imamu na hata kubainisha njia fulani itakayotumika kupita na kutuma kikosi cha wanausalama. Njia aliyochagua haikuwa njia ya kawaida ambayo Mashia mengi walikuwa wakiishi. Wakiwa njiani waliingia mji uitwao Nishapur. Hapo wasomi na watu walimtaka Imam kuwasomea hadithi. Imamu aliwasomea Hadith ifuatayo ambayo inajulikana kama hadithi ya mnyororo wa dhahabu.

“Baba yangu Musa Kadhim amenisimulia mimi kutoka kwa baba yake Jaffari Sadiq kutoka kwa baba yake Mohammed Baqir kutoka kwa baba yake Ali Zaynul Abedeen kutoka kwa baba yake, shahidi wa Karbala kutoka kwa baba yake Ali bin Abu Talib amesema : ” Ewe kipenzi changu, na radhi ya macho yangu, Mtume wa Mungu (amani iwe juu yake na familia yake) aliniambia wakati fulani, kwamba Jibril alimwambia kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu ” Kalima ya la ilaha Illallah ni ngome yangu, na yeyote anaye itamka kaingia katika ngome yangu, na yeyote aliyeingia katika ngome yangu atakuwa salama kutokana na adhabu yangu. “

Wale ambao waliandika hadithi hii hesabu yao ni ishirini elfu. Hapo watu walianza kuisoma Kalima ndipo Imamu aliponyanyua mkono wake juu na kuendelea : ” Ndiyo, Kalima ni ngome ya Mwenyezi Mungu itakuhakikishia usalama wa hakika lakini kwa sharti moja tu ni kwamba ni wewe kutii na kutufuata sisi Maimamu Watakatifu katika kizazi cha Mtume (SAW na nyumba yake). Alipofika Mji wa Marw Mamun akamlazimisha Imamu kukubali kuwa mrithi wa wazi (Kwa kuwa kiongozi baada yake) Imamu akakubali shingo upande.

Kwa nini Mamun alitaka Imamu kuwa mrithi wake dhahiri ?

1)     Ili kuridhisha maoni ya umma wa Mashia katika mji wa Khurasan na maeneo ya jirani kwani hilo litafanya kuwa rahisi kwa Mamun kukubaliwa na watu wa hapo na kuridhiwa ushindi wake juu ya ndugu yake Amin .

2)     Ili kuepuka mapigano na watu kama Alawids ambao walikuwa daima wakitisha tawala za Abbasia na misukosuko mbalimbali.

Mamun alisherehekea sana tukio la Imamu kukubalika kuwa mrithi wake, wakati huo kwa upande wake imamu alitoa hutuba fupi tu akisema baada ya kumsifia Mwenyezi Mungu.” Tuna haki zaidi juu yako ya kuteuliwa na Mtume, na una haki juu yetu vile vile, hivyo kama wewe utatimiza wajibu wako kwetu , sisi tutalazimika kutekeleza wajibu wetu kwako “.

Mamun akaamuru sarafu mpya kuchongwa jina la Imamu Ridha juu yake lakini Imamu hata hivyo alijua kwamba hii bila shaka ni mbinu itakayoisha muda mfupi.

Punde kidogo Mamun akaanza kumuweka imam chini ya ulinzi na uangalizi wa hali ya juu. Imamu aliitumia nafasi yake kueneza mafundisho sahihi ya uislamu. Na wakati wote Mahakama ya Mamun ilikuwa ikitembelewa na watu kwa maelfu na Imamu alifanya athari kubwa katika mawazo yao. Kwani ni katika wakati huo Hadith zake nyingi zilikuwa zikihifadhiwa sana katika kumbukumbu. Mamun ambaye alikuwa mpenzi wa majadiliano ya kitaalamu mara kwa mara akiwapanga wasomi kutoka Ugiriki, Italia, India nk kuja mahakamani kwake kuendesha majadiliano na Imamu.

Siku moja msomi wa Kiyahudi aliletwa na Mamun kujadiliana na Imamu. Msomi aliuliza: “Jinsi gani unaweza kukubali Muhammad kuwa ni nabii wa Mungu wakati yeye hakuwa na miujiza?” Imamu alijibu: “Muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu ni akili ya binadamu. Inaruhusu dhana mbalimbali kuwazika na kupatiwa busara ndani yake. Uislamu umeapa na kuitukuza Akili. Mwanaadamu lazima amkubali mungu kwa kupitia busara za Akili na sio kupitia Miujiza”

Msomi hakuwa na mengi ya kusema baada ya jibu hilo.

Imamu pia amesisitiza kwa mapana sana juu ya umuhimu wa kumkumbuka Imam Husein (as). Maamuni alikuwa kamwe si mkweli wa tabia zake kwa Imam. Kwa Kuona umaarufu wa Imamu unaongezeka kila uchao hilo lilikuwa likimsumbua sana na hasa baada ya tukio wakati yeye alipomuomba Imamu kuongoza sala ya Idd alipokuwa hajisikii vizuri. Alishuhudia hata kabla ya imamu kufika msikitini watu walikuwa wamejipanga mistari mitaani na walikuwa wakisoma Takbir na ilionekana kwamba hata kuta za mji wa Marw walikuwa kufanya Vivyo hivyo. Ilibidi Mamun amzuie na amtake imam arudi nyumbani kwake siku hiyo.

Kuna maelezo mbalimbali yanayosimulia jinsi Imam Ali Ridha (as) alivyouwawa na Mamun. Mmoja wapo ya simulizi ni kuwa, Imamu alikuwa akipenda sana zabibu na hivyo Mamun alimuandalia na kumpa Imamu zabibu zenye sumu. Imamu akapatwa na Maradhi na alikufa baada ya siku mbili tarehe 29 Safar Mwaka wa 203 Baada ya hijira.

Simulizi nyingine ni kuwa Imamu Ali Ridwa (as) alikufa huko Toos katika kijiji kiitwacho Sanabad akiwa na mtoto mmoja tu, Imam Muhammad Taqi (as), ambaye alimrithi kama Imamu wa Tisa (9).

Mamun aliamuru kaburi la Imamu lazima lichimbwe karibu na baba yake Harun na wakati lilipokuwa likichimbwa akasema kuwa Imam alimwambia wakati kaburi lake litakapokuwa likichimbwa Maji na Samaki wataonekana chini. Na kama alivyotabiri Imamu wakati walipomaliza kuchimba chemuchemu ya maji ilionekana na samaki ndani yake na kisha kutoweka. Imamu alizikwa hapo sehemu ambayo leo inatambulika kwa jina la Mashhad katika Nchi ya Iran.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini