Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

IMAMU WA KUMI NA MOJA.

0 Voti 00.0 / 5

IMAM WA KUMI NA MOJA: IMAM ASKARIY (A.S)

Yeye ni Imam Hassan bin Ali Al-askariy (a.s) na mama yake ni Sayyidah Hadiitha. Alizaliwa katika mji wa Madinatul-munawwarah siku ya Ijumaa tarhe nane (8) mwezi wa Rabiul-aakhir, na inasemekana kuwa amezaliwa tarehe kumi na mbili (12) Rabiul-aakhir [29] mwaka (232) hijiria na kufa shahidi kwa Sumu siku ya Ijumaa tarehe nane (8) mwezi wa Rabiul-awwal mwaka (206) hijiria, na mwanae Imam Hujjatul-muntadhar (mwenye kungojewa) ndie alie simamia maandalizi ya mazishi yake na kumzika karibu na kaburi la baba yake Imam Al-hadiy (a.s) katika mji wa Samarra, mahala ambapo ndipo lilipo kaburi lake kwa hivi sasa.

Na Imam (a.s) alikuwa ni mfano wa juu kabisa katika ubora, elimu, utoaji, sharafu, furaha na ukarimu, ibada, unyenyekevu na tabia zingine nyingi njema, na alikuwa ni mfano wa kuigwa na kigezo chema kwa wengine, na alikuwa ni mwenye urefu wa wastani na mzuri wa umbile, mwenye uso mzuri na kiwiliwili cha wastani, mwenye heshima na hadhi kubwa kwenye nyoyo na mwenye nafasi ya juu na tukufu katika nafsi za watu, na Imam (a.s) alikuwa akimfanana sana babu yake Mtume (s.a.w) katika tabia zake na mwendo wake mwema na uzuri wa kuishi vema na watu.

 Na miongoni mwa visa vya ukarimu wake ni kisa kilicho pokelewa na Ismail kisemacho: Nilimkalia na kumsubiri Imam (a.s) katikati ya njia, alipo fika na kupita mahala nilipo kuwa nikamueleza ufukara wangu. Imam akasema (a.s): Unaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo kwani umefukia Dinari miambili  chini ya Ardhi na kusema kwangu maneno haya si kwa sababu ya kuto taka kukupa, ewe ghulam (Mhudumu) mpatie ulicho nacho, akasema: Yule mhudumu akanipatia Dinari mia moja.[30]

Na kuna mtu mwingine alimwendea Imam-alipo sikia ukunjufu wake na ukarimu wake-na alikuwa akihitaji Dirhamu mia tano, Imam (a.s) akampatia Dirham mia tano na kumuongezea Dirhamu zingine mia tatu.[31]

Na kwa hakika watu wote walitoa ushahidi na kuthibitisha ubora wake na ukarimu wake, hata wakiristo walimshuhudia (a.s) ya kuwa yeye anafanana na masihi (Yesu) katika ubora, elimu, ukarimu na miujiza yake, na Imam (a.s) alikuwa ni mwenye kufanya sana ibada, akisali sala za usiku (tahajjud) daiama na alikuwa ni mwenye mandhari ya wema, na mwenye heba kubwa

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini