Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA SITA) B

0 Voti 00.0 / 5

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA SITA) B
MATENDO YASIYOSHAURIWA KUFANYWA
Ni muhimu kufahamu kwamba vingi ya vitendo vilivyotajwa katika sehemu hii vinafanana na vile vilivyoelezwa kwenye mlango wa Adabu za mahusiano ya kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi vinavyoathiri mtoto anayezaliwa.
VITENDO VYA MAKRUHU (VYA KARAHA)
Kwa vile vitendo vingine vina athari hasi, mbaya juu ya mtoto kama vile chuki dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s.),1 inashauriwa kwamba vitendo vilivy- otajwa hapa chini viwe vinaepukwa:
1. Kuangalia kwenye sehemu nyeti za siri za mwanamke wakati wa kitendo chenyewe hasa, kwani hili linapelekea kwenye upofu wa mtoto atakayezaliwa.2
2. Kuzungumza wakati wa kitendo chenyewe (isipokuwa kwa kudhukuru Allah (s.w.t.).), kwani hili linapelekea kwenye ububu wa mtoto atakayezaliwa.3
3. Kuwa na hinna juu ya mwanaume, kwa vile hili husababisha ukhuntha wa mtoto anayezaliwa (yaani, msichana anakuwa na tabia za kiume na kinyume chake).4
4. Kufikiria au kutamani mwanamke mwingine wakati wa kitendo, kwa vile hili linapelekea kwenye wenda wazimu wa mtoto atakayezaliwa.5
5. Kufanya mapenzi mbele ya mtoto, ambaye ama anaweza kuona au kusikia sauti za kitendo hicho, kwani hili linaleta matokeo ya mtoto huyo kutokuja kuokolewa (kutoka kwenye moto wa Jahannam) na kuwa mzinifu.6
6. Kufanya mapenzi wakati ambapo kuna mtu aliyeko macho ndani ya nyumba, ambaye anaweza kuona au kusikia sauti za kitendo hicho, kwani hili linaleta matokeo ya mtoto kutokuja kuokolewa (kutoka kwenye moto wa Jahannam) na kuja kuwa mzinifu.7
7. Kufanya mapenzi kwa kusimama wima, kwani hili linapelekea mtoto kuwa na tatizo la kukojoa kitandani.8
8. Kufanya mapenzi juu ya paa la nyumba, kwani hili linaishia kwenye mtoto kuwa mnafiki, na mmbea (mzushi).9
9. Kufanya mapenzi chini ya mti wa matunda, kwani hili linapelekea mtoto kuwa muuaji na kiongozi wa udhalimu.10
10. Kufanya mapenzi chini wa mwanga wa moja kwa moja wa jua, kwani hili linapelekea mtoto kuwa masikini, hata mpaka kifo chake.11
11. Kufanya mapenzi wakati mwanaume yuko katika hali ya Muhtalim (yaani, anapokuwa na hali ya janaba kwa ndoto usingizini mwake) na kabla ya kuchukua Wudhuu au Josho, kwani hili linasababisha mtoto kuja kuwa mwendawazimu.12
Ni muhimu vilevile kuzingatia akilini vitendo vinginevyo vile vyenye karaha – Makruh – wakati wa taratibu za kawaida za mahusiano ya kujamiiana (kama zilivyoelezwa kwenye Mlango wa 2: Adabu za Mahusiano ya Kujamiiana). Hivi ni vifuatavyo:
1. Kuwa na Qur’ani au Majina ya Allah (s.w.t.). mwilini mwako.
2. Kufanya mapenzi ukiwa uchi kabisa (bila cha kujifunika).
3. Kufanya mapenzi barabarani au ndani ya boti.
4. Kuelekea au kukipa mgongo Qibla.
5. Kukataa kujamiiana (kwa sababu mbalimbali – za visingizio).
Kiangalizo: Mara mwanamke anapokuwa kaishapata ujauzito, inashauri- wa kujiepusha kutokana na kufanya mapenzi bila ya Wudhuu, kwani hili linasababisha mtoto kuwa masikini na upofu wa ndani13
NYAKATI ZINAZOSHAURIWA
Ni muhimu kutambua kwamba nyingi ya nyakati zilizotajwa katika mlan- go huu ni sawasawa na zile zilizotajwa kwenye mlango wa Taratibu za Kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi zinavyomuathiri mtoto anayezaliwa.
NYAKATI ZINAZOFAA (MUSTAHAB)
1. Usiku wa Jumapili (kuchea Jumatatu). Mtoto anayetungwa kwenye mimba usiku huu atakuwa mwenye kuridhika na chochote Mwenyezi Mungu Mtukufu atakachomjaalia nacho, atakuwa na kumbukumbu nzuri na atakuwa Hafidh (mwenye kuhifadhi) wa Qur’ani Tukufu.14
2. Usiku wa Jumatatu (kuchea Jumanne). Mtoto anayetungiwa mimba kwenye usiku huu atakuwa na ustawi au neema ya Uislamu, na fursa ya Shahadat na hatoadhibiwa pamoja na washirikina. Atakuwa na kinywa kilicho na harufu nzuri na moyo wa huruma. Atakuwa ni mtu mwenye kutoa sadaka na ulimi wake utasalimika na kusema uongo, kusengenya au kutoa shutuma za uongo.15
3. Usiku wa Jumatano (kuamkia Alhamisi) Mtoto anayetungwa mimbani kwenye usiku huu atakuwa mtawala miongoni mwa watawala wa Shari’ah, au mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni
wa kidini.16
4. Mchana wa Alhamisi, wakati wa kumalizika kwa mchana. Huu ndio muda muafaka, bora kabisa na umependekezwa sana kwa ajili ya utun- gaji mimba. Shetani hatasogea karibu na mtoto anayetungwa kwenye mimba usiku huu mpaka anapokuja kuzeeka na usalama wa dini na dunia utakuwa wake.17
5. Usiku wa Alhamisi (kuchea Ijumaa). Mtoto anayetungwa mimbani kwenye usiku huu atakuja kuwa mubalighin, msemaji fasaha na msomaji wa Qur’ani.18
6. Siku ya Ijumaa, baada ya wakati wa Alasiri. Mtoto atakayetungwa mimbani wakati huo atajulikana sana miongoni mwa watu wenye busara na wanachuoni wakubwa.19
7. Siku ya Ijumaa, baada ya wakati wa swala Isha. Mtoto atakayetungwa kwenye mimba wakati huo atakuwa anatokana na watu wema na wanaofaa.20
8. Usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani.21
NYAKATI ZISIZOPENDEKEZWA
Ni muhimu kutambua kwamba nyingi ya nyakati zilizotajwa katika mlango huu ni sawasawa na zile zilizotajwa katika mlango wa Taratibu za Kujamiiana, pamoja na nyongeza ya jinsi zinavyoathiri mtoto anayezaliwa.
NYAKATI HARAMU
1. Wakati wa kipindi cha hedhi ya mwanamke, hata katika ile siku ya mwisho, mpaka tone la mwisho la damu litakapodondoka. Ujauzito bado unawezekana, na mtoto atakayetungwa mimbani atasumbuliwa na (phagedemic ulcers) – aina ya vidonda vya tumbo na ukoma.22
Imesimuliwa vile vile kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.) kwamba: “Hakuna adui kwetu sisi Ahlul-Bayt, isipokuwa yule ambaye amezaliwa kwa njia ya haramu na yule ambaye alitungwa mimbani wakati wa hedhi.23
Ni muhimu vile vile kuzingatia akilini vitendo vingine haramu wakati wa taratibu za kawaida za kujamiiana (kama zilivyotajwa katika Mlango wa 2: Taratibu za Kujamiiana): Hizi ni:
1. Wakati wa Nifaas
2. Wakati wa saumu katika mwezi wa Ramadhani
3. Wakati katika hali ya Ihraam
4. Wakati ambapo inaweza kusababisha madhara makubwa ama kwa mume au kwa mke.
NYAKATI ZA KARAHA (MAKRUH)
1. Kati ya asubuhi sadiki (Adhana ya swala ya al-Fajr) na kuchomoza kwa jua.24
2. Kati ya kuzama kwa jua mpaka kupotea kwa wekundu wa angani.25
3. Usiku wa kupatwa kwa mwezi.26
4. Mchana wa kupatwa kwa jua.27
5. Wakati wa tetemeko la ardhi (au matukio mengine yanayolazimu Swala – Salat al-Ayat).28
Kama atatungwa kwenye mimba katika nyakati hizo hapo juu, wazazi hawataona sifa yoyote wanayoipenda kwa mtoto wao, kwa sababu hawakuziona hizi ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa za muhimu.29
6. Katika tarehe ya mwanzo wa mwezi (isipokuwa mwezi mosi ya Ramadhani, ambapo ni mustahab), katikati ya mwezi (unapoonekana mwezi kamili) na mwishoni mwa mwezi (kunapokuwa hakuna mwezi), kwani itakuwa ni chanzo cha hali ya wendawazimu, ukoma mweusi na kupooza kwa mama na mtoto.30
Hadithi nyingine inasimulia kwamba kutunga mimba wakati wa mwanzo wa mwezi na katikati ya mwezi kunapelekea kwenye wendawazimu na mtoto kutawaliwa na Jinni,31 na kutunga mimba wakati wa mwisho wa mwezi kunaongezea uwezekano wa kuharibika kwa mimba.32
7. Baada ya swala ya Adhuhuri (mpaka takriban karibu na wakati wa Asr), kwani hii inapelekea mtoto kuwa na makengeza.33
8. Kati ya Adhana na Iqaamah kwani hii inapelekea kwa mtoto kuwa shauku ya kuua.34
9. Usiku wa Eid al-Fitr, kwani hii inasababisha katika mtoto kuwa chanzo cha maovu.35
10. Usiku wa Eid al-Udh’haa, kwani hilo linapelekea kwa mtoto kuwa na vidole (sita) 6 au (vinne) 4.36
11. Usiku wa nusu ya Shaaban (mwezi 15), kwani hili linapelekea kwenye mtoto kuwa na hali ya ndege mbaya (nuksi au kisirani) na alama nyeusi usoni mwake.37
12. Siku ya mwisho ya mwezi wa Sha’ban, kwani hii inapelekea kwa mtoto kuwa msaidizi na mkusanyaji kodi wa madhalimu.38
13. Usiku wa Ashuraa’.
KUPANGA MIMBA
Tunaweza kuhitimisha kutokana na yote hayo hapo juu kwamba lengo la mahusiano ya kijinsia ni la njia mara mbili: kuridhisha haja ya mtu ya kimaumbile na kuzaa.
Miongozo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.) kwa wazi kabisa inaonyesha urefu wa muda ambao mtu anaweza kuchukua ili kupata mtoto anayefaa. Mahusiano ya kijinsia kwa ajili ya utungaji mimba yanapaswa kufanywa kwa tofauti kabisa, vyote kiakili na kivitendo.
Wakati mwingine, inaweza kutokea kwamba kutokana na ukosefu wa taar- ifa au sababu nyinginezo, mazingira ya upatikanaji wa mimba ya mtoto yanakuwa hayakupangwa. Taarifa hiyo hapo juu inaweza kwa hiyo kuwa chanzo cha wasiwasi kwa ajili ya wazazi kuhusu matokeo yanayowezekana ya utungaji wa mimba katika nyakati na kwa vitendo visivyopendeza.
Ni muhimu kuzingatia akilini kwamba kuna mambo mengi yanayochangia katika utengenezaji wa mtoto, kama vile hali asili ya kurithi (genetics), lishe, hali ya kijamii, na kadhalika.
Taarifa zilizotajwa hapo juu ni baadhi tu ya haya mambo ambayo yanaweza kuathiri mtoto aliyezaliwa.
Kwa nyongeza, inawezekana kuyakinga matokeo ya kijyume yanay- owezekana kutokea kwa vitendo kama vile sadaka, kusoma Qur’ani na kutafuta tawasali (uombezi mtukufu) kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s.).39
REJEA:
•    1. Biharul-Anwar, Jz. 39, uk. 278, Hadithi ya 87
•    2. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 122, Hadithi ya 25197
•    3. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 121, Hadithi ya 25195
•    4. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 125, Hadithi ya 25205
•    5. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    6. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, uk. 133, Hadithi ya 25223
•    7. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, Uk. 64
•    8. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    9. Ibid. (Hilliyatul Muttaqiin, uk. 112-114)
•    10. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    11. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    12. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20 Uk . 148, Hadithi ya 25271
•    13. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 148
•    14. Hilliyatul Muttaqiin, Uk k. 112-114
•    15. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    16. Hilliyatul Muttaqiin Uk. 112-114
•    17. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    18. Hilliyatul Muttaqiin Uk. 112-114
•    19. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    20. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    21. Hilliyatul Muttaqiin, Uk. 112-114
•    22. Hilliyatul Muttaqiin, Uk 110
•    23. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, uk. 69
•    24. Wasa’ilush-Shi’ah, Jz. 20, Uk. 126-127, Hadihi ya 25207
•    25. Ibid
•    26. Ibid
•    27. Ibid
•    28. Ibid
•    29. Niyaazhaa wa Rawaabith Jinsii was Zanaashuii, uk. 59
•    30. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk 129, hadithi ya 25214
•    31. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk. 129, hadithi ya 25212
•    32. Wasa’ilush-Shi’ah, Juz. 20, Uk. 129, hadithi ya 25208
•    33. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    34. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    35. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    36. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    37. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    38. Hilliyatul Muttaqin, Uk. 112-114
•    39. Imethibitishwa na ofisi ya Ayatullah Sistanii, Qum.

ITAENDELEA MAKALA IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini