Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA SABA) C

0 Voti 00.0 / 5

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA SABA) C
MLANGO WA 6: MIMBA (C)
KUUMBWA KWA MTOTO KWA MUJIBU WA QUR’ANI TUKUFU
VITENDO VINAVYOPENDEKEZWA
Kwa ajili ya watoto wenye sifa njema na maumbo kamilifu, akina mama wanashauriwa kufanya kwa wingi zaidi ya vitendo vifuatavyo kiasi iwezekanavyo:
VITENDO VYA KAWAIDA
Vitendo Vya Kawaida 1
1. Wakati wote jaribu kuwa katika hali ya wudhuu, hasa wakati wa kula chakula.
2. Wakati wote jaribu kuelekea Qibla wakati unapofanya matendo ya kila siku, hususan kula na kunywa.
3. Toa sadaka kila siku kwa ajili ya ulinzi wa mtoto.
4. Usijiangalie kwenye kioo wakati wa usiku.
5. Jihadhari na aina zote za dhambi, hususan kusengenya na uongo.
6. Tekeleza vitendo vyote vya wajibu na jaribu kufanya vitendo vingi mus- tahabu vilivyopendekezwa kwa kiasi kinachowezekana.
7. Jaribu kuwa umetulia na kuwa na mawazo yenye kusaidia wakati wote, na usiwe mwenye hasira.
8. Zuia mawazo ya wasiwasi wowote unaowezekana kuhusu makuzi na maendeleo ya mtoto au mimba kwa kupata taarifa zote muhimu, na zaidi ya yote hasa, kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu
9. Sikiliza, na soma Qur’ani kwa wingi iwezekanavyo, na hivyo kusaidia mtoto wako kuwa hafidh wa Qur’ani kuanzia akiwa tumboni.
10. Sikiliza hotuba kutoka kwa wanavyuoni.
11. Fanya josho la Ijumaa – Sunnat Ghusli-Jumu’ah – kwa Ijumaa 40 (tafadhali kumbuka kwamba mimba kwa kawaidi ni majuma 40. Kwa nyongeza, imesimuliwa katika hadith kwamba mtu anayechukua Ghuslul-Jumu’ah kwa wiki 40 mfululizo, mtu huyo hatakabiliwa na mbinyo wa kaburini).
12. Swali swala ya usiku Salatul-Layl mara 40 kwa kima cha chini kabisa.
Kama mtu hawezi kuamka kabla ya Swala ya al-Fajr na kuswali, basi inawezekana kuiswali baada ya Swala ya Isha.2 Kama hili pia hali- wezekani, inashauriwa kuswali Qadhaa.
13. Kula zabibu kubwa kwa siku arobaini kwenye tumbo tupu lenye njaa, kila siku vipande 21, kila kipande kuliwa baada ya kusoma Bismillah.
14. Mkumbuke Mwenyezi Mungu Mtukufu (sina dhikri ya Allah) wakati wote.
15. Saidia watu wengine katika matatizo yao.
16. Kuangalia nyuso za watu wachamungu na mandhari nzuri za kimaum- bile.
17. Usijichanganye na watu wenye tabia mbaya.
18. Nenda ukafanye Ziyaarat.
19. Tekeleza Swala zako kwa wakati wake uliopangwa.
20. Mpe mtoto jina akiwa tumboni, na chagua majina mazuri kama Muhammad, Ali, Fatimah na umuite kwa jina hili.
21. Zungumza na mtoto akiwa tumboni, kwani hili linaongeza ukaribu wa wazazi na mtoto huyo. Hili linabakia katika kumbukumbu ya mtoto, hata baada ya kuzaliwa. 3
VITENDO MAALUM KWA AJILI YA KILA MMOJAWA MIEZI ILE 9 YA UJAUZITO.
MWEZI WA 1:
Soma Surat Yaasin (36) na al-Saffaat (37) siku ya Alhamisi na Ijumaa na kasha pulizia kwenye tumbo.
Kula tufaha tamu wakati wa asubuhi
Kula komamanga kabla ya kifungua kinywa siku za Ijumaa.
Kula kiasi kidogo cha Khakhe Shafaa 4 (kipimo cha mbegu ya dengu) kabla ya kuchomoza kwa jua.
Swali swala zako za kila siku katika nyakati fadhilah.
Soma Adhana/Iqamah kabla ya swala na mkono wako juu ya tumbo.
Soma Surat al-Qadr (97) ukiwa na tende mbili kila siku na kuzila ukiwa na tumbo tupu.
MWEZI WA 2:
Soma Surat al-Mulk (67) siku ya Alhamisi na Ijumaa.
Soma Swalawat – Swala ya Mtume (pamoja na Wa Ajjil Farajahum ikiongezwa mwishoni) siku ya Alhamisi mara 140 na siku ya Ijumaa mara 100: “Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad, Wa Ajjil Farajahum.”
Soma Swalawat hii ndefu ifuatayo pamoja na mkono wako juu ya tumbo: “Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad, Wa Ajjil Farajahum wa ahlik ‘aduwwahum minal-jinna wal-insi minal awwalina wal aakhirina.”
“Ewe Mola! Wape rehma na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad, na harakisha kuondolewa kwao kutoka kwenye mateso, na waangamize maadui zao, na walaani maadui zao miongoni mwa majinni na watu kuanzia mwanzo hadi mwisho (wa wakati).5
Kula nyama na tuhafa tamu na kiasi cha maziwa kila wiki.
Soma Surat al-Tawhiid (112) juu ya jujube 2 (tunda la rangi nyekundu nzito; pia linajulikana kama tende ya Kichina) kila siku na uzile kwenye tumbo tupu.
MWEZI WA 3:
Soma Surat Aali Imraan (3) katika siku za Alhamisi na Ijumaa. Soma Swalawat (pamoja na Wa Ajjil Farajahum) mara 140.
Soma ile Swalawat ndefu kabla ya kila swala ukiweka mkono juu ya tumbo: “Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad, Wa Ajjil Farajahum wa ahlik ‘aduwwahum minal-jinni wal-insi minal awwalina wal aakhirina.”
“Ewe Mola! Wape rehma na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad, na harakisha kuondolewa kwao kutoka kwenye mateso, na waangamize maadui zao, na walaani maadui zao miongoni mwa majinni na watu kuanzia mwanzo hadi mwisho (wa wakati).” 6
Kula ngano na nyama na kunywa maziwa kila wiki. Kunywa asali kila asubuhi.
Soma Ayat al-Kursi (Surat al-Baqarah; 2:255) juu ya tuhafa kila siku na kula tunda hili kwenye tumbo tupu. Kula kiasi kidogo sana cha Ubani Makkah (kipimo cha mbegu moja ya dengu) kwenye tumbo tupu.7
MWEZI WA 4:
Soma Surat ad-Dahr/al-Insaan (76) mnamo siku Alhamisi na Ijumaa. Soma Surat al-Qadr (97) katika rakaa moja ya kila Swala yako.
Baada ya swala za kila siku, soma Suratul-Kawthar (108), Suratul-Qadr (97) na ile Swalawat ndefu pamoja na kuweka mkono juu ya tumbo: “Allahumma swali ‘alaa Muhammadin wa aali Muhammad, Wa Ajjil Farajahum wa ahlik ‘aduwwahum minal-jinna wal-insi minal awwalina wal aakhirina.”
“Ewe Mola! Wape rehma na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad, na harakisha kuondolewa kwao kutoka kwenye mate- so, na waangamize maadui zao, na walaani maadui zao miongoni mwa majinni na watu kuanzia mwanzo hadi mwisho (wa wakati).”8
Soma:
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا {74}
“…..Mola wetu! Utupe katika wake zetu na watoto wetu yaburud- ishayo macho, na utujaalie kuwa viongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu.” (Al-Furqaan, 25:74).
Soma: Astaghfirullaha Rabbi wa Atuubu Ilaik. (Ninaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na natubia Kwako) mara saba (7).
Soma Swalawat mara 140 baada ya kumaliza Swala.
Kula tuhafa tamu, asali na komamanga.
Anza kuswali Salatul-Layl (kama huwezi hili kwa wakati wake, basi swali qadhaa).
Soma Suratut-Tiin (95) juu ya tiini mbili kila siku na uzile kwenye tumbo tupu.
Chagua jina la mtoto kabla haijatimia miezi 4 na siku 10 ya umri wa mimba.
MWEZI WA 5:
Soma Surat al-Fath (48) katika siku za Alhamisi na Ijumaa.
Soma Surat an-Nasr (110) katika swala ya kila siku.
Sugua Khakhe Shafaa juu ya tumbo.
Kula tende moja kila siku asubuhi.
Kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa tano, wakati wa Swala, anza kusoma Adhana na Iqama ukiwa na mkono wako juu ya tumbo.
Soma Surat al-Hamd (1) juu ya yai moja kila siku na ulile yai kwenye tumbo tupu lenye njaa.
MWEZI WA 6:
Soma Surat al-Waqiah (56) siku za Alhamisi na Ijumaa.
Soma Suratut-Tiin (95) katika moja ya rakaa za Swala za Magharibi na Isha.
Paka Khakhe shafaa juu ya tumbo, baada ya kila swala.
Kula tiini na zeituni baada ya kifungua kinywa.
Imma wakati wa asubuhi au usiku, jaribu kula uboho wa mfupa,9 na jiweke mbali na vyakula vya mafuta.
Soma Surat al-Fath (48) juu ya komamanga kila siku na ulile wakati ukiwa na tumbo tupu.
MWEZI WA 7:
Kuanzia kwenye mwezi wa 7, kwa siku 40 baada ya Swala ya al-Fajr soma Surat al-An’aam (6) juu ya malozi na kisha ule matunda hayo.
Kuanzia mwezi wa 7 na kuendelea, kula lozi moja kwa siku.
Soma Surat al-Nahl (16) siku ya Jumatatu.
Soma Surat Yaasiin (36) na Surat al-Mulk (67) siku za Alhamisi na Ijumaa.
Kuanzia mwezi huu na kuendelea, soma Surat an-Nuur (24) mara kwa mara.
Kuanzia mwezi huu na kuendelea, baada ya tasbihi, soma mara tano Sura hizi: Surat al-Hadiid (57), Suratul-Hashr (59), Suratul-Saff (61), Suratul- Jumu’ah (62) na Suratut-Taghabun (64) mara kwa mara.
Soma Surat al-Qadr (97) na Surat at-Tawhiid (112) katika Swala za kila siku.
Soma Swalawaat mara 140 kila siku.
Kula tikiti maji kiasi kidogo baada ya chakula (usinywe maji kabla au baada).
Soma Surat Yaasiin (36) juu ya quince (tunda aina ya pera) kila siku na ule tunda hilo kwenye tumbo tupu.
MWEZI WA 8:
Soma Surat al-Qadr (97) mara 10 katika siku za Jumamosi baada ya Swala ya al-Fajr.
Soma Suratut-Tiin (95) mara mbili katika siku za Jumapili baada ya swalat Subhi.
Soma Surat-Yaasiin (36) kwenye siku za Jumatatu.
Soma Suratul-Furqaan (25) siku ya Jumanne.
Soma Surat ad-Dahr/al-Insaan (76) kwenye siku ya Jumatano.
Soma Surat-Muhammad (47) mnamo siku ya Alhamisi.
Soma Suratus-Saffaat (37) siku ya Ijumaa.
Kula mtindi mtamu kwa asali.
Kula komamanga tamu kwenye siku ya Ijumaa ukiwa na tumbo tupu.
Kama hakuna hofu ya madhara, tumia siki (katika chakula chako) mara moja kwa wiki.
MWEZI WA 9:
Usitumie kula garam masala.10
Chinja kondoo wa kafara kwa ajili ya Imam Mahdi (a.s.) na kisha kula kutoka humo kiasi.
Kula tende na kabaab. Kuhusu kula tende, imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Katika mwezi ambamo wanawake wajawazito hujifungua watoto, walisheni tende kwani watoto wao watakuwa wavumilivu na waadilifu.”11
Soma Suratul-‘Asr (103) na Suratu-Dhaariyaat (51) ndani ya swala za Dhuhuri na Al-‘Asr.
Soma Surat al-Hajj (22) kwenye siku ya Alhamisi na Surat al-Faatir (35) kwenye siku ya Ijumaa usiku.
Soma Suratul-Insaan/al-Dahr (76) juu ya kiasi fulani cha tende na maziwa kila siku na kula kwenye tumbo tupu.
Jaribu kujiepusha kuangalia picha na kujitazama kwenye kioo.
Fanya matembezi ya kila siku kwa hatua za taratibu.
DUA NA MAOMBI YANAYOPENDEKEZWA
Dua za kawaida katika kipindi chote cha ujauzito.12
1. Soma Surat Mariam (19) kila siku kwa ajili ya mtoto mwadilifu na mchamungu.
2. Soma Surat Yaasiin (36) mara 40 (kila mara moja ipulize kwenye koma- manga na kisha ulile tunda hilo)
3. Soma Surat Yusuf (12) mara arobaini (kila mara moja ipulize kwenye tuhafa na kisha ulile tunda hilo).
4. Soma Sura hizi: al-Hadid (57), al-Hashr (59), at-Taghabun (64), al- Jumu’ah (62), na as-Saff (61)
mara arobaini (40) kabla ya kulala siku ya Alhamisi usiku au usiku wowote ule.
5. Soma Surat at-Tawhiid (112) mara 50 kila siku baada ya swalat Subhi.
6. Soma Suratul-Qadr (97) mara 50 kila siku baada ya swala ya al-Fajr.
7. Soma Suratul-Anbiyaa (21) mfululizo (angalau mara moja kwa wiki) kwa ajili ya mtoto mchamungu.
8. Kwa ajili ya mtoto mwenye subira, soma Surat al-‘Asr (103) ukiwa na mkono wako juu ya tumbo lako.
9. Soma Ziyaarat al-Jam’iah mara 40.
10. Soma Ziyaarat Aale Yaasiin (na ile Dua inayoifuatia) kwa mara 40.
11. Soma mara arobaini (40) Ziyaarat ‘Ashuuraa (pamoja na laana 100 na salaam na Dua Alqamah 100, kama laana hizo 100 na salaam hazi- wezekani, basi hata mara 10 itatosheleza.).
12. Soma Ziyaarat al-Imaam al-Mahdii (a.s.) mara 40.
13. Soma Hadith al-Kisaa mara 40.
14. Soma Duaul-Tawassul mara 40.
15. Soma Duaa Kumail siku ya Alhamisi usiku mara 40.
16. Soma Dua an-Nudba kwenye asubuhi ya siku ya Ijumaa (kabla ya Dhuhr) mara 40.
17. Soma Dua as-Samaat kwenye mchana wa siku ya Ijumaa mara 40.
18. Soma Dua al-‘Ahd mara 40 mfululizo baada ya Swalat al-Fajr.
19. Mswalie Bwana Mtume – Swalawaat 140 kwa siku.
20. Soma Istighfaar mara 70 baada ya swalaa.
21. Soma Tasbih al-Hadhrat Fatimah (a.s.) baada ya kila swala, na kila usiku kabla ya kulala.
22. Soma Qur’ani Tukufu yote mara moja (na uziwasilishe thawabu zake kwa Imam al-Mahdi a.s.).
23. Wakati wa kuhisi mtisiko wa mtoto, weka mkono wako juu ya tumbo na soma Swalawaat na Surat al-Tawhiid (112).
Kiangalizo: Ni muhimu kutambua kwamba kwa ajili ya zile Dua za kila wiki 40 zilizopendekezwa (kama vile Dua al-Kumail), kwamba kuna takriban wiki 40 katika ujauzito.
DUA ZA KI-QUR’ANI KWA AJILI YA WATOTO WANYOFU
1. Dua ya Nabii Ibrahim (a.s.):
رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ {100
فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ {101}
“Ewe Mola Wangu! Nipe (mtoto) miongoni mwa watendao wema. Ndipo tukampa habari njema ya mwana mpole.” (As-Saffaat; 37:100- 101)
2. Dua nyingine ya Nabii Ibrahim (a.s.):
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِنْ ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ {40}
“Mola Wangu! Nijaalie niwe msimamishaji swala na kizazi change (pia) Mola Wetu! Na uyapokee maombi yetu. (Al-Ibrahim; 14:40)
3. Dua ya Nabii Zakariya
رَبِّ هَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ {38}
“Pale pale Zakariya akamwomba Mola Wake, akasema: Mola Wangu! Umpe kutoka Kwako kizazi kizuri, hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia maombi.” (Al-Imraan; 3:38)
4. Dua ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ {15}
“….. Na unitengenezee watoto wangu, kwa hakika ninatubu Kwako na hakika mimi ni miongoni mwa walionyenyekea.” (Al-Ahqaf; 46:15)
6. Dua nyingine ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا {74}
“….. Mola Wetu! Utupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho, na utujaalie kuwa viongozi kwa wamchao Mungu.” (Al- Furqaan 25:74)
Dua ya Imam Zainul-Abidiin kwa ajili ya watoto kama ilivyosimuliwa ndani ya Sahifatul–Sajjadiya, ni Dua inayoshauriwa sana kusomwa katika wakati wa ujauzito na baada ya hapo:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma. Mwenye kurehemu.”
“Allahumma wa munna ‘alaiyya bibaqaai wuldiy wa bi-iswlaahihim liy wa bi imtaa‘i bihim.
“Ewe Mola! Kuwa na huruma juu yangu kupitia uhai wa watoto wangu, ukiwaongoza katika njia iliyonyooka kwa ajili yangu, na ukiniwezesha kuwafaidi!”
“Ilaahiy amdudliy fiy a’amaarihim, wa zidliy fiy aajaalihim, wa rabbi liy swaghiirahum, wa qawwi liy dhwa’iyfahum, wa aswihha liy abdaanahum wa adyaanahum wa akhlaaqahum, wa ‘afihim fiy anfusihim wa fiy jawaar- ihihim wa fiy kulli maa ‘uniytubihi min amrihim, wa adrir liy wa ‘alaa yadiy arzaaqahum. Waj’alhum abraaran atqiyaa buswaraaa sami’iyna mutwi’iyna laka, wa liawliyaaika muhiybiina munaaswihiyna, walijamiy’i a’adaaika mu’aanidiyna wa munghidhwiyna, aamiina.”
“Mola Wangu! Yafanye maisha yao kuwa marefu kwa ajili yangu, waongezee vipindi vyao, zidisha kilicho kidogo kwa ajili yangu, wape nguvu wanyonge kwa ajili yangu, warekebishie miili yao kwa ajili yangu, kujitolea kwao kidini, na akhlaq zao, wape afya katika nafsi zao, viungo vyao, na kila kitu ambacho kinanihusu mimi katika mambo yao, na uni- jaalie mimi na juu ya mikono yangu riziki yao! Wafanye wawe wanyofu, wenye kuhofia, wenye busara, wasikivu na watiifu Kwako, wenye mahaba na mwelekeo mwema kwa marafiki Zako, na wapinzani sana na wenye chuki kubwa kwa maadui Zako wote! Amiina!”
“Allahumma sh’dud bihim ‘adhwudiy, wa aqim bihim awadiy, wa kathir bihim ‘adadiy, wa zayyin bihim mahdhwariy, wa ahyi bihim dhikriy, waak- finiy bihim fiy ghaybatiy, wa a’inniy bihim ‘alaa haajatiy, waj’alhum liy muhibiyyna, wa ‘alaiyya hadibiyna muqbiliyna mustaqimiina liy, mutwiy’iyna, ghayra ‘aaswiyna wa laa ‘aaqqiyna wa laa mukhalifiyna wa laa khatwii’yna.
“Ewe Mungu, kupitia kwao niimarishie mkono wangu, ninyooshee mgon- go wangu uliolemewa na unizidishie idadi yangu, na uupambe uwepo wangu, na uhuishe kumbukumbu yangu, nitoshelezee kupitia kwao pale ninapokuwa sipo, na unisaidie katika haja zangu, na uwajaalie mahaba juu yangu na upendo, kuwaendea, waadilifu, watiifu, kamwe wasiofanya maasi, wasiokhalifu au wenye kufanya hatiauonevu!”
“Wa a’inniy ‘alaa tarbiyatihim wa ta-adiybihim, wa birrihim, wahabliy min ladunka ma’ahum aulaadan dhukuuran wa-j’al dhaalika khairaan liy, wa aj‘alhum liy ‘awnaan ‘alaa maa sa-altuka.”
“Nisaidie katika malezi yao, elimu yao, na utii wangu kwao, nijaalie mion- goni mwao kutoka Kwako mtoto wa kiume, na umfanye mwema kwangu, na uwafanye wao wawe msaada kwangu katika lile ninaloliomba kutoka Kwako!”
“wa a’izaniy wa dhuriyatiy min shaytwaani rajiymi, fainnaka khalaqtanaa wa amartanaa wa nahaytanaa waraghabtanaa fiy thawaabi maa amar- tanaa wa rahhabtanaa ‘iqaabahu, wa ja’alta lanaa ‘a duwaan yakiy- dunaa, sallatw’tahu minnaa ‘alaa maa lam tusallitw’naa ‘alayhi minhu, askantahu swuduuranaa, wa ajraytahu majaariyaa, laa ya ghfulu in ghafalnaa, wa laa yansaa in nasiynaa, yu-uminunaa ‘iqaabika, yukhawfu- naa bighayrika.”
“Nipatie mimi na kizazi changu hifadhi kutokana na Shetan aliyelaaniwa, kwani Wewe umetuumba sisi, umetuamuru sisi, na umetukataza sisi, na umetufanya sisi tuwe na tamaa juu ya thawabu za yale uliyotuamrisha, na hofu juu adhabu yake! Umetujaalia sisi adui ambaye anapanga mipango dhidi yetu, ukampa mamlaka juu yetu, ukamruhusu kukaa ndani ya vifua vyetu na ukamfanya atembee ndani ya mishipa ya damu zetu, yeye hajali japo sisi tuzembee, yeye hasahau, ingawa sisi tunasahau; anatufanya sisi tujihisi tuko salama kutokana na adhabu Zako na anatujaza hofu kwa mwingine asiyekuwa Wewe!”
“In hamamnaa bi faahishatin shaja’aanaa ‘alayhaa, wa in hamamnaa bi ‘amali swaalihin thabatwanaa ‘anhu, yata’aaradhu lanaa bilshshahawaati, wayanswibu lanaa bilsh-shubhaati,
in wa’aadanaa kadhabanaa, wa in mannanaa akhlafanaa, wa illa taswrif ‘annaa kaydahu yud- hwilnaa,wa illa taqinaa khabblahu yastazilanaa.”
“Kama tukikaribia kufanya maovu, yeye anatutia moyo kufanya hivyo, na kama tunataka kufanya amali njema, yeye anatuzuia kufanya hivyo. Anatupinga sisi kupitia hisia, na anatujengea mashaka na wasiwasi. Kama akituahidi sisi, anatudanganya, na endapo akinyanyua matumaini yetu, anashindwa kuyatimiza. Kama hutazigeuza hila zake juu yetu, yeye atatupotosha, na kama hutatulinda kutokana na udhalimu wake, atatufanya sisi tuteleze.”
“Allahumma faaqhar sultanaahu ‘annaa bisultaanika hattaa tahbisahu ‘annaa bikathratid-du’aai laka fanuswbiha min kaydihi fiy al-ma’asuw miyna bika.”
“Ewe Mungu, hivyo uyashinde mamlaka yake juu yetu kwa mamlaka Yako, kiasi kwamba unamrudisha nyuma kutoka kwetu kupitia wingi wa du’a zetu Kwako na sisi tunaziacha hila zake na kuamka miongoni mwa wale waliolindwa Nawe kutokana na dhambi!”
“Allahumma a’atwiniy kulla suwliy, wa-aqdhwi liy hawaaijiy, wa laa tamna’aniy l-ijaabata wa qad dhwamintahaa liy, wa laa tahjub du’aaiy ‘anka wa qad amartaniy bihi, waamnun ‘alayyaa bikulli maa yuslihuniy fiy dunyaaya wa aakhiratiy maa dhakartu minhu wa maa nasiytu,
aw adh-hartu aw akhfaytu aw a’alantu aw asrartu.”
“Ewe Mungu, nijibu kila ombi, nijaalie juu yangu haja zangu, usizuilie kutoka kwangu majibu Yako unapokuwa umekadiria majibu, usiyawekee pazia maombi yangu kutoka Kwako, wakati Wewe ukiwa umeniamuru kuyafanya, na unineemeshe kupitia kila kitu ambacho kitaniweka sawa katika dunia hii na ile ijayo ya akhera, katika kila kitu ambacho ninakikum- buka au kukisahau, ninachokionyesha au kukificha, ninachofanya hadharani au ninachokifanya siri!”
“Wa-j’alniy fiy jami’yi dhaalika minal-muswalihiyn bi suwliy innaaka, al- munjihiyna bi-twalabi ilayka ghayril-mamnuw’iyna bi tawakkuli ‘alaykal- mu’awwadhiyna bi tta’awwudhiyna bika, ar-raabihiyna fiy tijaarati ‘alayka, mujaariyna bi’izzaka, muwassa’i ‘alayhim ar-rizkul-halaalu min fad- hilika, al-waasi’i bijuwdika wa karamika, al-mu’azziyna minal-dh-dhula bika, wal-mujaariyna minadh-dhulmi bi’adlika, wal-mu’aafiyna minal- balaai bi-rahmatika, wal-mughniyna minal-faqri bighinaaka, wal-ma’a- suwmiyna minadh-dhunuwbi waz-zalali wal-khatwaai bitaqwaaka, wal- muwafiqiyna lilkhaiyri war-rushdi wa swawaabi bitwa’atika, wa muhaali baynahum wa baynadh-dhunuwbi biqudratika, at-taarikiyna likulli ma’aswiyatika, saakiniyna fiy jiwaarika.”
“Nijaalie (katika yote haya, kupitia maombi yangu) kuwa miongoni mwa wenye kuweka mambo sawa (swalihiin), wale wanaojibiwa vyema wanapoomba kutoka Kwako na ambao hawanyimwi wanapoweka mategemeo yao Kwako, wale ambao wenye mazoea ya kuomba hifadhi Kwako, wale wanaonufaika kwa biashara pamoja Nawe, wale waliopata kimbilio kwa nguvu Zako, wale ambao wanaopewa riziki halali kwa wingi kutoka Kwako, neema isiyo na mipaka kupitia upaji na ukarimu Wako, wale wanaofikia daraja ya juu baada ya unyonge, kupitia Kwako, wale wanaookoka na dhulma kwa uadilifu Wako, wale wanaondolewa kwenye mateso kwa rehma Zako, wale wanaookolewa kwenye dhiki baada ya umasikini kwa ukwasi Wako, wale waliokingwa na madhambi, kuteleza na mahatia kwa uchamungu wao na hofu juu Yako, wale waliofanikiwa katika wema, na wongofu na usahihi kupitia utii juu Yako na wale waliokingwa dhidi dhambi kwa uwezo Wako, wanaojizuia na kila tendo baya la kufru juu Yako, wale wakaazi wa jirani Yako.”
“Allahumma a’atwinaa jamiy’a dhaalika bi-tawfiyqika wa rahmatika, wa a’idhnaa min ‘adhaabis-sa’iyri, wa a‘atwi jamiy’al-muslimiyna wal-mus- limaati wal-mu’minina wal-mu’minaati mithlal-ladhiy sa-altuka linafsiywa liwuldiy fiy ‘aajilid-dun’yaa wa ajilil-aakhirati, innaka qariybun mujiybun samiy’un ‘aliymun ‘afuwun ghafuwrun raawfun rahiymun. Wa aatinaa fiy ad-dun’yaa hasanatan, wa fiyl-aakhirati hasanatan wa qinaa ‘adhaaban-naari.”
“Ewe Mungu, nipatie yote hayo kutokana na utoaji wako wa mafanikio na rehma Zako, tujaalie kinga kutokana na adhabu ya kuungua, na utupe Waislam wote, waume kwa wake, na waumini wote wanaume kwa wanawake, kama kile nilichoomba kwa ajili yangu na wanangu, katika ukaribu wa dunia hii na ya akhera! Hakika Wewe ni Mkaribu, Mwenye kujibu, Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote, Mwenye kuridhia, Msamehevu, Mpole, Mwenye huruma! Na utupatie mema katika dunia hii, na mema katika akhera, na utukinge na adhabu ya Moto!”
REJEA:
•    1. Zaidi vinapatikana kutoka Rayhaaney-e Beheshti, uk. 103 - 106
•    2. Imethibitishwa na ofisi ya Ayatullah Sistaanii, Qum.
•    3. Fasalnaameye Shir Maadar, namba 9.
•    4. Udongo wa ardhi tukufu ya Karbala, Iraqi.
•    5. Biharul-Anwar, Jz. 86, Uk. 289
•    6. Biharul-Anwar, Jz. 86, Uk. 289
•    7. Hili halishauriwi kwa wale wanaishi kwenye nchi kame na zenye chumvichumvi (majangwa).
•    8. Biharul-Anwar, Jz. 86, Uk. 289
•    9. Pia unajulikana kama ‘bongo’ kwa ki-Gujarati
•    10. Mchanganyiko fulani wa viungo wenye asili ya India
•    11. Mustadrak al-Wasaa’il, Jz. 3, Uk. 112
•    12. Nyingi zinapatikana kutoka kwenye Rayhaaney-e Beheshti, Uk. 103-106
ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini