Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

BIBI FATIMAH ZAHARA (A.S) 4

0 Voti 00.0 / 5

HISTORIA YA MA'ASUMIN (A.S).

MA'ASUMAH WA PILI

 BIBI FATIMAH ZAHARA AS 4

Sehemu ya nne

FATIMAH ZAHARA (S.A) NDANI YA

HADITH ZA MTUKUFU MTUME (s.a.w.w).

1. Mtu yeyote atakaye mpenda Fatimah (a.s) atapendwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

2. Siku zote Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa akisema: Ewe Mwenyezi Mungu! Kuwa rafiki na watu wanaompenda Fatimah as na uwe adui na wale wanaomchukia Fatimah (a.s).

3. Mara nyingi Malaika walikuwa wakifanya safari kuja kumsalimia Fatimah (a.s) na walikuwa hawachoki kumtazama na ilikuwa ni Ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

4. Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema: Ewe Fatimah! Furahia hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuchagua uwe kiongozi wa wanawake wa ulimwengu na wanawake wa Kiislamu na uislamu ndio bora ya dini zote.

5. Mtukufu Mtume saww anasema katika hadithi ndefu aliyoeleza Dhulma zitakazowapata Ahlubaiti (a.s) akasema: ama mtoto wangu Fatimah Hakika yeye ni Kiongozi wa wanawake wa ulimwengu wa mwanzo na wa Mwisho.

6. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) anasema kumwambia Fatimah: Hakika Jibrilu as amenipa habari kuwa katika wanawake wa kiislam hakuna mwanamke mwenye misiba (matatizo) mikubwa kuliko wewe (kuwa mwenye subira) usije ukawa ni mwanamke duni kuliko wanawake wengine katika kuwa na subira.

7. Mtukufu Mtume saww anasema :. Alinijia Malaika akanisalimu huyu Malaika alishuka toka mbinguni hajawahi kushuka kabla ya hapo akaniambia: Hakika Hassan na Hussein ni mabwana wawili wa vijana wa watu peponi na hakika Fatimah ni Kiongozi wa wanawake peponi.

8. Mtukufu Mtume Muhammad saww alisema: Hakika ilivyo Fatimah ni sehemu ya mwili wangu huniudhi linalomuudhi.

9. Mtukufu Mtume Muhammad saww alisema kumwambia Fatima (a.s): Hakika Mwenyezi Mungu hukasirika kwa lile lilokukasirisha, na anaridhia kwa lile uliloridhia.

10. Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alisema: Ewe Fatimah je, huridhii kuwa umekuwa kiongozi wa wanawake wa ulimwengu na kiongozi wa wanawake wa ummah huu na kiongozi wa wanawake waumini?

11. Kutoka kwa Ibn Abbasi anasema: Siku moja Mtukufu Mtume saww alichora mistari minne kisha akasema: Mnajua nini maana yake? Wakasema Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuao: Mtukufu Mtume saww akasema: Hakika wanawake bora peponi ni Khadija bint Khuwaylid (a.s) Fatimah bint Muhammad (s.a.w.w), Mariamu bint Imran na Asia bint Mzahimah.

12. Kutoka kwa Abi Ja'far kutoka kwa baba zake anasema: Hakika Fatimah bint Muhammad Anaitwa twahirah kwa sababu ya kutoharika kwake kuepukana na kila aina ya uchafu na kutoharika kwake kuepukana na upuuzi wa aina yoyote, hajawahi kuona wekundu (hedhi) hata siku moja wala nifasi.

13. Abu Abdullah as anasema :. Kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu:

مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ ﴿١٩﴾ بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ ﴿٢٠﴾ فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢١﴾ يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٢٢﴾.

Anaziendesha bahari mbili zenye kukutana, baina yao kipo kizuizi, hazibughudhiani. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. 55:19-22.

Abu Abdillah anasema: Ally na bi Fatumah ndio bahari mbili za elimu zenye kina kirefu hawabughudhiani, kizuizi kilicho kati yao ni Mtume Muhammad saww zinatoka katika bahari hizo lulu na marijani yaani Hassan na Hussein (a.s).

14. Kutoka kwa Ally (a.s) anasema: Nimemsikia Mtume (s.a.w.w) anasema: Kitakaposimama kiyama ataita mwitaji kwa nyuma ya pazia akisema: Enyi mliokusanyika (katika uwanja huu) inamisheni macho yenu (msimwangalie) Fatimah bint Muhammad (s.a.w.w) hadi apite (kuingia peponi maana baada ya Mtukufu Mtume Muhammad saww kuingia peponi atakaye fuata ni Ally bin Abi Twalib (a.s) na Fatimah bint Muhammad (s.a.w.w).

15. Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasema: Wanawake waliobora katika watu wa peponi ni Khadija bint Khuwaylid (a.s) Fatimah bint Muhammad (s.a.w.w), Mariamu bint Imran na Asia bint Mzahimah.

Huyo ndiye Fatimah Zahara katika hadithi za mtukufu Mtume (s.a.w.w).

Rejea:

 sahihi Bukhari Jz 3 UK 21

Sahihi Muslim Jz 5 UK 57 hadithi 99 babu fadhail Fatimah UK 628

Mustadrakul Jz 2 UK 539 hadithi 3836 na UK 166 hadithi 4728

Rawdhwatul waidhina UK 148

Biharul anuwari Jz 43 UK 19

Fuatana nami sehemu ya tano historia ya Maasumah Fatimah bint Muhammad (s.a.w.w).

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini