KUFUNGUA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA 4
KUFUNGUA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNAH HADITHI
Sehemu ya nne
UPEMBUZI KUHUSU KINACHOPATIKANA NDANI YA AYA HIZI TATU 2:183-184-185 KATIKA MAKUNDI MANNE YA WATU
KUNDI LA KWANZA: MTU MZIMA MWENYE AFYA.
Hakika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi mwenye kushuhudia mwezi huu na aufunge." Inabaainisha wazi ulazima wa kufunga saumu kwa mwenye kuushuhudia mwezi, bila kutofautisha Tafsiri ya kushuhudia mwezi, kati ya kuwemo ndani ya mji wa makazi bila ya safari au kuona mwezi muandamo. Mwenye kushuhudia hana jukumu isipokuwa moja tu nalo ni kufunga mwezi mzima iwapo atatimiza shart zote.
KUNDI LA PILI NA TATU: MGONJWA NA MSAFIRI
Hakika Mwenyezi Mungu amebainisha hukumu ya mgonjwa na msafiri katika Sehemu mbili:
¹. Na ambaye alikuwa katika nyinyi ni mgonjwa au yuko safarini basi yampasa alipe idadi yake katika siku nyingine." 2:184
². Na ambaye alikuwa mgonjwa au yuko safarini basi itampasa idadi katika siku nyingine." 2:185.
Na Makusudio ni kufahamu hukumu ya jukumu la mgonjwa na msafiri ndani ya sentence katika Sehemu hizo mbili. Je ni maana dhahiri inayoonyesha kuwa kufungua ni lazima au ni ruhusa ya hiyari.
Na kuzama ndani ya Aya kunathibitisha kuwa kufungua ni lazima, hilo ni kwa vigezo vinne:
KIGEZO CHA KWANZA: KUWEPO WAJIBU WA KUFUNGA KATIKA SIKU NYINGINE NI ALAMA YA ULAZIMA WA KUFUNGUA MGONJWA AU MSAFIRI.
Hakika maana ya Kauli ya Mwenyezi Mungu:" "Basi itampasa idadi katika siku nyingine" maana yake ni "Wajibu juu yake Saumu katika siku nyingine" au "Inamlazimikia Saumu katika siku hizo."
Hilo ndilo linaloonekana toka kwa wafasiri wengi kwani baada ya sentence "Basi itampasa idadi katika siku nyingine" wanasema: "Ni wajibu juu yake Saumu siku nyingine.' Hivyo maana inayojulikana haraka toka kwenye Aya ni kuwa analazimikiwa kufunga katika siku hizo nyingine, au ana dhima ya kufunga. Huu ni upande mmoja.
Upande mwingine ni kuwa ikiwajibika kufunga siku hizo nyingine bila shart lolote basi inakuwa kufungua ndani ya mwezi wa Ramadhani ni wajibu. Kwa sababu laiti ingekuwa ni ruhusa ya hiyari kufunga basi isingekuwa ni wajibu kufunga siku hizo nyingine bila kuwekewa sharti lolote. Hivyo wajibu huo wa kufunga nao pia ni alama ya wajibu wa kufungua mgonjwa na msafiri katika mwezi wa Ramadhani.
KIGEZO CHA PILI: MUKABALA KATI YA SENTENCE MBILI NI DALILI YA UHARAMU WA KUFUNGA, (mgonjwa na msafiri).
Ni wazi kuwa ikiwa ndani ya maneno kuna sentence mbili zilizo Mukabala basi hali ya kujulikana maana ya moja kati ya sentence mbili huondoka kwa kujulikana maana dhahiri ya sentence nyingine. Kutokana na hayo tunaondoa hali ya kutojulikana maana ya Kauli "Au yuko safarini" kwa kutumia sentence nyingine Mukabala, hivyo tunasema:
Mwenyezi Mungu kasema kuhusu atakayeshuhudia mwezi kuwa: "Basi mwenye kushuhudia mwezi huu na aufunge."
Kisha akasema kuhusu yule asiyeshuhudia mwezi: "Na ambaye alikuwa mgonjwa au yuko safarini basi yampasa alipe idadi yake katika siku nyingine.'
Hivyo ikiwa maana ya sentence ya kwanza ni kuwa mwenye kushuhudia mwezi afunge kwa mujibu wa hukumu ya Mukabala itakuwa maana ya sentence ya pili ni kuwa msafiri hafungi. Hivyo kama amri ya kutenda iliyopo sentence ya kwanza inaonyesha wajibu basi amri ya kukataza iliyopo sentence ya pili itakuwa inaonyesha uharamu.
Imepokewa kutoka kwa Ubaydu bin Zurara toka kwa Imamu Ja'afar Sadiq as kwamba amesema: "Nilimwambia: "Basi mwenye kushuhudia mwezi huu na aufunge." Akasema: "Ni hili ninalolibainisha:
Mwenye kushuhudia mwezi afunge na atakayesafiri asifunge"'.
fuatana nami Sehemu ya tano kuona kigezo cha tatu upembuzi kuhusu Aya hizo tatu 2:183-184-185.
REJEA:
Wasailu UK 7, hadithi ya 8, mlango wa 1 mlango wa anayepaswa kufunga.
Tafsiri Tabar Jz 2 UK 77.