KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 1
KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA
WAJIBU WA MWANAMUME
Sehemu ya kwanza
MSIMAMIZI WA FAMILIA
Mwanaume na Mwanamke ni nguzo mbili za msingi wa familia, lakini kwa kuwa wanaume wamepewa sifa maalumu kwa amri ya Muumbaji na kwa sababu ya kuwa uwezo wao wa mantiki ni imara zaidi ya ule wa wanawake, wao huchukuliwa kama wasimamizi wa familia zao.
Mwenyezi Mungu Muweza wa yote amewaweka wanaume kuwa walezi wa familia zao na anasema kwenye Qur-ani Tukufu:
الرجال قوامون على النساء بما فضل الله بعضهم على بعض
"Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi. 4:34
Kwa hiyo, wanaume wanajukumu kubwa na zito zaidi katika kuzisaidia familia zao.
Ni mwanaume ambaye kwa kutumia busara yake, anaweza kuisaidia familia yake na kutayarisha mazingira kwa ajili ya furaha yao, na ni yeye ambaye anayeweza kuigeuza nyumba kuwa pepo na mke wake kuwa kama Malaika.
Mtukufu Mtume saww alisema: "Mwanaume ni mlinzi wa familia yake na kila mlezi anao wajibu kwa hao waliopo kwenye ulinzi wake."
Mwanaume ambaye anaisaidia familia yake, lazima atambue kwamba mwanamke pia ni binadamu kama mwanaume. Pia mwanamke anayo matamanio na haki ya uhuru na maisha. Kumuoa mwanamke si kukodisha mtumishi, lakini ni chaguo la mwenza na rafiki ambaye atakuwa tayari kuishi pamoja katika maisha yote. Mwanaume lazima amtunze na amtimizie matakwa yake. Mwanaume si mmiliki wa mke wake, kwa kweli mwanamke anazo haki fulani kwa mume wake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwenye Qur-an Tukufu:
ولهن مثل الذي عليهن بالمعروف ولرجال عليهن درجة والله عزيز حكيم
"..... Na wanawake wanayo haki kwa Sheriah kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. 2:228
Kwamujibu wa Aya hii ni kuwa Mwanamke Ana haki kwa Mume wake Kama Ambavyo Mwanamume Anahaki kwa Mke wake, kinacho paswa kuzingatiwa zaidi katika Maisha ya Ndoa na Ili kustawisha Maisha yenu ya Ndoa, ni Kila Mmoja kuzingatia haki za Mwenziwe.
Ama ni zipi haki za wana ndoa ambazo za paswa kuzingatiwa, ufanunuzi wake utakujia katika Makala zifuatazo.
Fuatana nami Sehemu ya pili katika somo hili la kanuni za ndoa na maadili ya familia, kwa muda huu nitakuwa mkunga na nitajikita kwanza kuwafunda wanaume njoo karibu yangu.