Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 2

0 Voti 00.0 / 5

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA

WAJIBU WA MWANAMUME

Sehemu ya pili

UTUNZAJI WA MKE WAKO

Siri ya ustawi wa familia inategemea na jinsi mtu anavyomtunza mke wake, na hii ni kama ilivyo wajibu wa mke kwa mume wake ambao unaeleweka kuwa katika kiwango sawa na jihadi, pia unatambua kama tendo jema na lenye thamani sana. Lakini mwanaume ajifunze namna ya kumshughulisha mke wake, katika namna ambayo atageuka kuwa na tabia kama Malaika.

Kuhusu jambo hili, mwanaume lazima atafiti kuhusu tabia na matakwa ya mke wake. Lazima apange maisha yake kufuatana na matakwa ya mke wake na mahitaji Sahihi. Mwanaume anaweza kwa tabia na msimamo wake kumshawishi mke wake katika njia ambayo inampendeza yeye (mke wake), kwake yeye mume na nyumba yake.

Hili ni somo ambalo linahitaji maelezo zaidi na mazungumzo ya kina yatawasilishwa baadaye kwenye makala hii maridhawa.

                   MPENDE MKEO

Mwanamke ni kituo cha wema na ni kiumbe chenye hisia kubwa sana. Kuwepo kwake hutegemea huruma na upendo. Huwa na shauku ya kupendwa na wengine na jinsi anavyopendwa zaidi ndivyo anavyofurahi zaidi.

Hujitolea sana ili apendwe na wengi. Tabia hii ina nguvu sana ndani mwake hivyo kwamba akigundua kwamba hakuna mtu anayempenda, basi atajitambua kama ameshindwa. Atakasirika na atahisi kuvunjika moyo. Kwa hiyo, kwa hakika mtu anaweza kudai kwamba siri ya mwanaume aliyefuzu katika maisha ya furaha ya ndoa ni jinsi anavyoonesha mapenzi kwa mke wake.

Bwana mpendwa! Mke wako kabla ya kuolewa na wewe, alikuwa anafaidi mapenzi ya wazazi wake na wema wa wazazi wake. Sasa ameingia kwenye mkataba wa ndoa na wewe na sasa amechagua kuishi na wewe katika maisha yake yote, anatarajia wewe umtimizie matakwa yake ya mapenzi na huba. Anatazamia wewe Kuonyesha mapenzi zaidi kwake kuliko alivyopokea kutoka kwa wazazi wake na marafiki zake. Amekuamini wewe sana na ndiyo sababu amekupa udhamini wa maisha yake.

Siri ya ndoa yenye furaha hutegemea jinsi unavyodhihirisha mapenzi yako kwa mkeo.

Ukitaka kuuvutia moyo wake, ukitaka awe mtiifu kuhusu matakwa yako kama kuimarisha ndoa yenu, ukitaka mkeo akupende wewe, au adumishe uaminifu kuliko au... Basi lazima kila mara uoneshe mapenzi na huba yako kwake.

Usipokuwa mwema kwa mke wako, basi anaweza kupoteza mvuto kwenye nyumba yake, halikadhalika na watoto pia. Na zaidi ya yote kwako wewe mwenyewe. Wakati wote nyumba yako itakuwa katika hali machafuko. Hatakuwa tayari kufanya juhudi kwa ajili ya mtu asiyempenda.

Nyumba ambayo ndani yake haina mapenzi, hufanana na Jahannamu inayowaka moto, hata kama ni nadhifu sana na iliyojaa vitu vya anasa.

Mke wako anaweza kuugua au kupatwa na mfadhaiko. Anaweza kutafuta kupendwa na wengine kama hatoshelezwi na wewe. Anaweza asikuthamini wewe na nyumba yako pia, kiasi kwamba anaweza hata kuomba talaka!

Unawajibika kwa yote haya kwa sababu umeshindwa kumtosheleza mkeo. Kwa hakika ni kweli kwamba taratibu zingine za kutalikiana hutokea kwa sababu ya ukatili wa mume au ukatili wa mke.

Fuatana nami Sehemu ya tatu kanuni za ndoa na maadili ya familia mpende mkeo 2.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini