KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 4
KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA
WAJIBU WA MWANAMUME
Sehemu ya nne
MSIMAMI WA FAMILIA
MWANAUME MHESHIMU MKE WAKO
Mwanamke hujivunia utu wake kama ilivyo kwa mwanaume. Anapenda kuheshimiwa na watu wengine. Ataumia sana kimawazo kama akitukanwa au kudhalilishwa. Hufurahi anapoheshimiwa na huchukia wale wanaojaribu kushusha hadhi yake.
Bwana mpendwa kwa hakika mke wako anatarajia kuheshimiwa na wewe zaidi kuliko watu wengine. Anayo haki kumtarajia mpenzi wake wa maisha na rafiki mzuri zaidi ya wote kumtunza yeye.
Mke wako kufanya kazi kwa ajili ya faraja yako na watoto wenu na kwa hiyo anakutarajia wewe kumthamini yeye na juhudi zake.
Kumheshimu mkeo si jambo la kukushusha hadhi yako ila ni kweli itakuwa ni uthibitisho wa mapenzi na huba yako kwake. Kwa hiyo, mheshimu mkeo zaidi ya mwingine na sema naye kwa upole. Usiingilie kati au kumkemea anapozungumza. Mwite kwa majina ya heshima na uadilifu. Onyesha heshima yako anapotaka kuketi chini.
Unapoingia nyumbani, akisahau kusema "Salamu alayk" ( yaani kukusalimia), basi anza wewe kumsalimia kwa kusema "Salamu alayk (amani iwe juu yako)."
Sema "kwa heri" unapoondoka nyumbani. Usiache kuwasiliana naye unaposafiri au unapokuwa haupo nyumbani. Mwandikie barua (massage).
Dhihirisha heshima yako kwake unapokuwa kwenye mikusanyiko. Usitumie lugha chafu au hata kumchokoza kwa kumtania. Usidhani ya kwamba kwa sababu upo karibu naye sana kwa hiyo hatojali ukimtania. Kinyume chake ni kwamba atachukia msimamo wa aina hiyo bila kukuonesha ishara yoyote.
Mwanamke mwenye hadhi mwenye umri wa miaka 35, anasema kuhusu ombi lake la talaka: Ni miaka 12 tangu nimeolewa. Mume wangu ni mwanaume mwema na zipo tabia nyingi za mtu mwema na mpole ndani mwake. Lakini kamwe hajataka kutambua kwamba mimi ni mke wake na mama watoto wake.
Yeye anadhani kwamba ni mtu anayeweza kuchanganyikana na kuzoeana na watu bila taabu, lakini maonesho yake hayo huyafanya kwa kunitania na kunidhalilisha. Huwezi kuamini ni kiasi gani nimeumia katika hisia zangu. Neva zangu zimeathiriwa sana hivyo kwamba imenibidi niende kupata ushauri kutoka kwa bingwa wa maradhi ya akili ili nipate tiba. Nimezungumza na mume wangu kuhusu jambo hili mara nyingi.
Nimemuomba asinifanyie hivyo. Nimemkumbusha kuhusu nafasi yangu kama "mke wake" na umri wangu na kwamba si stahili yake kunitania mimi mbele ya watu wengine hadi wanacheka au wanafurahia kitendo hicho. Nina hisi kuaibika mbele ya kila mtu na kwa sababu sijawahi hata wakati mmoja kuwa mcheshi, siwezi kushindana naye. Kwa kuwa matakwa yangu hayatekelezwi na mume wangu, ninataka kutengana naye. Ninajua sitakuwa na furaha nikibaki peke yangu, lakini siwezi kuishi na mwanaume ambaye hushusha hadhi yangu kila wakati.."
Wanawake wote huwa na matamanio ya kuheshimiwa na waume zao na wote huchukia fedheha. Kama wanawake wengine hunyamaza wakati waume zao wanawadhalilisha huo si uthibitisho wa kuridhika kwao na tabia hiyo.
Ukimheshimu mke wako, na yeye atafanya hivyo kwako na uhusiano wenu utazidi kuimarika. Wewe pia utapata heshima zaidi kutoka kwa watu wengine. Kama ukimtendea vibaya mke wako na yeye alipe kisasi, hili tena si kosa lake ni kosa lako.
Bwana mpendwa ! Kuoa si sawa na kupata mtumwa. Huwezi kumtendea mtu aliye huru kama mtumwa. Mke wako amekubali kuolewa na wewe ili aishi na wewe na kugawana maisha yake na mtu ambaye anampenda.
Anatazamia mambo kama hayo kutoka kwako kama vile unavyotarajia kutoka kwake. Kwa hiyo, mtendee kwa namna ambavyo wewe ungependa kutendewa.
Imamu Ja'afar Sadiq as akimnukuu Baba yake, alisema: "Yeyote anayeoa, lazima amheshimu mke wake."
Mtukufu Mtume saww alisema: "Mtu yeyote anayemheshimu Mwislamu, Mwenyezi Mungu atampa heshima yake mwenyewe."
Mtukufu Mtume saww pia alisema: "Hapana yeyote ambaye angewaheshimu wanawake isipokuwa watu wakarimu. Mtukufu Mtume saww akaongeza kwa kusema: "Mtu yeyote anayetukana familia yake, atapoteza furaha katika maisha yake.
Rejea: Wasailu Shi'ah
Fuatana nami Sehemu ya tano kujifunza kanuni za ndoa na maadili ya familia.