Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

NDOA YA MTUKUFU FATIMAH ZAHRAA (A.S) 4

0 Voti 00.0 / 5

NDOA YA MTUKUFU FATIMAH ZAHARA AS, KUTOKA NYUMBA YA MTUKUFU MTUME SAWW, NA MTUKUFU IMAMU ALLY BIN ABI TWALIB AS, MZALIWA KATIKA NYUMBA YA MWENYEZI MUNGU MTUKUFU. 01 Dhul Hijja mwaka wa 2 hijiria

MATAKWA YA KHADIJA (A.S)

Katika ule usiku wa harusi ya Bibi Fatimah Zahraa as, Asmaa binti Umais (au Ummu Salama) ambaye alikuwa miongoni mwa wanawake hao, aliomba ruhusa kutoka kwa Mtukufu Mtume saww kama angeweza kukaa karibu na Bibi Fatimah Zahraa as ili aweze kutekeleza mahitaji yoyote atakayoweza kuwa nayo. Alimwambia Mtukufu Mtume saww. Wakati wa kifo cha Bibi Khadija ulipofika  hapo Makkah, mimi nilikuwa karibu naye na niliona kwamba Khadija alikuwa analia. Nilimuuliza: "Wewe ni Bibi wa wanawake dunia yote' na ni mke wa Mtukufu Mtume saww na licha ya yote hayo bado unalia ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupa habari njema za (kufaulu kuingia) peponi?

Bibi Khadija alijibu: Silii kwa sababu ya (kuogopa) kifo; bali mimi ninalia kwa ajili ya Fatimah ambaye ni Msichana mdogo, na mwanamke katika usiku wa harusi wanahitaji mwanamke kutokana na ndugu zao na wale wa karibu (maharimu) watakaoweza kuwaambia wao siri zao zilizofichika, na ninahofia kwamba usiku huo, kipenzi changu Fatimah hatakuwa na mmojawapo."

Kisha nilimwambia Khadija kwamba: "Ninaapa kwa Mola wangu kwamba kama nitabaki kuwa hai mpaka siku hiyo, usiku huo mimi nitakaa ndani ya nyumba hiyo mahala pako (badala yako). Sasa ningeomba ruhusa kutoka kwako kwamba unisamehe ili niweze kutimiza ahadi yangu.""

Baada ya kuyasikia haya, Mtukufu Mtume saww alianza kulia na akanipa ruhusa kubaki na akaniombea Du'a.[1]

SUTI YA HARUSI YENYEWE

Katika usiku ule wa harusi ya Bibi Fatimah Zahraa as na Imamu Ally as, Mtukufu Mtume saww alimpa binti yake suti (vazi) ya harusi ya kuvaa usiku ule. Wakati Bibi Fatimah Zahraa as alipokuwa amekwenda kule kwenye nyumba ya harusi na pale alipokuwa ameketi kwenye mkeka wa kuswalia ili kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu mara akatokea mtu mweye shida kwenye mlango wa nyumba ya Bibi Fatimah Zahraa as na kwa sauti kubwa akasema: "Kutoka kwenye mlango wa nyumba ya Utume,mimi ninaomba suti ya zamani, chakavu."

Kwa wakati ule, Bibi Fatimah Zahraa as alikuwa na suti mbili, moja iliyochakaa na nyingine bado mpya yeye alitaka kutoa ile suti ya zamani kulingana na maombi ya yule mtu mwenye haja, ghafla wakati alipokumbuka Aya inayosema: "Hamtapata uchamungu mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda, na chochote mnachokitoa, basi Mwenyezi Mungu hakika anakijua. 3:92

لن تنالوا البر حتى تنفقوا مما تحبون، وما تنفقوا من شيء فأن لله به عليم.

Bibi Fatimah Zahraa as ambaye alijua kwamba anaipenda ile suti mpya zaidi, alifanya kulingana na Aya hii na kutoa ile suti mpya kumpa yule mtu mwenye haja.

Siku iliyofuata, wakati Mtukufu Mtume saww alipoiona ile suti ya zamani mwilini mwa Bibi Fatimah Zahraa as, yeye alimuuliza: "kwa nini hakuvaa ile suti mpya?

Bibi Fatimah Zahraa as akajibu: "Niliitoa kumpa mtu mwenye haja." Mtukufu Mtume saww akasema: "Kama ungevaa ile suti mpya kwa ajili ya mumeo ingekuwa vizuri na yenye kufaa sana." Bibi Fatimah Zahraa as alijibu akasema: "Hili nimejifunza kutoka kwako. Wakati mama yangu Khadija alipokuja kuwa mke wako, alitoa utajiri wake wote kwenye mkono mtupu uliokuwa kwenye njia yako, ilikuwa haina kitu, hadi ikafikia mahali wakati alipokuja mtu mwenye shida kwenye mlango wa nyumba yako na kuomba nguo. Kukawa hamna nguo ndani ya nyumba yako hivyo ukavua shati lako na ukampatia yeye, na ndipo ikashuka Aya hii:

"Wala usiufanye mkono wako uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue kabisa, usije ukakaa hali ya kulaumiwa na kufilisika ukajuta. 17:29

ولا تجعل يدك مغلولة إلى عنقك ولا تبسطها كل البسط فتقعد ملوما مخسورا.

Mtukufu Mtume saww akiwa amezidiwa na mshangao kwa upendo na uaminifu wa binti yake Fatimah Zahraa as, yalimdondoka machozi kutoka machoni mwake, na kama ishara ya upendo, yeye alimkumbatia Bibi Fatimah Zahraa as kifuani mwake saww.[2]

Fuatana nami Sehemu ya kumi na saba historia ya Ma'asumah Fatimah Zahraa as

 

[1]. Rejea: Sar Guzashthaaye Hadharat Ally as wa Fatimah as UK 30.

[2]. Rejea: Sar Guzashthaaye Hadharat Ally wa Fatimah Zahraa as, UK 31.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini