Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

HISTORIYA YA IMAMU HUSSEIN (A.S) 1

0 Voti 00.0 / 5

IMAMU HUSSEIN A.S

Sehemu ya kwanza

Jina: Hussein a.s

Jina la heshima: Sayyidush shuhada.

Jina la Utoto (kunia): Aba Abdillah.

Jina la baba yake: Haidar Ally a.s

Jina la mama yake: Bi Fatimah Zahara a.s

Tarehe ya kuzaliwa: Tarehe 3 tatu Shaban mwaka wa nne 4 hijiria.

Mji alip[1]ozaliwa: Mji Mtukufu Madina Munawarah.

Muda aliotumika katika uimamu: Miaka kumi na moja 11.

Tarehe ya kuuawa shahidi: Siku ya kumi 10 Ashura Muharram mwaka 61 sitini na moja hijiria.

Aliyemuua: Yazeed bin Muawiyyah (l.a) mjukuu wa mla maini (l.a)

Mji alioifia na kuzikwa :. Mji Mtukufu Karbala Iraq

Umri wake: Hamsini na saba 57

Imamu Hussein (a.s) Alizaliwa tarehe tatu 3 Shaban mwaka wa nne 4 hijiria katika mji wa Madina. Yeye ni mtoto wa pili wa Imamu Aliy (a.s) na Fatimah Zahara (a.s) Baada ya habari ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) kufika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alifurahi sana na akasema aletewe mtoto huyo.

Asmaa ambaye alikuwa ni msaidizi wa kazi wa nyumba ya Ally na bi Fatumah (a.s) alimchukua mtoto mchanga katika kitambaa cheupe na kumpeleka kwa Nabii saww. Mtume saww alimchukua mtoto huyo na akambusu. Alimudhinia katika sikio lake la kulia na kukimu sala katika sikio la kushoto. Muda huo huo Malaika wakateremka na kumwambia Mtume (s.a.w.w): Ewe Mtume! Mwenyezi Mungu amekutumia salamu kwamba mtoto huyo umwite Hussein".

Imamu Aliy Zainul Abidina (a.s) anasema: Alipozaliwa Hussein a.s Mwenyezi Mungu alimkabidhi Jibrilu a.s wahyi kwamba :. Muhammad amepata mtoto teremka kwake kumpa pongezi, mwambie hakika Ally kwako wewe ana nafasi ya Haruna kwa Musa, hivyo mpe jina la mtoto wa Haruna.

Jibrilu (a.s) Akampa pongezi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kisha akasema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakuamuru kwamba umpe jina la mtoto wa Haruna. Mtukufu Mtume saww akamuuliza ni lipi jina la mtoto wa Haruna? Akasema Jibrilu (a.s): Shubairi, Mtukufu Mtume saww akasema: Lugha yangu ni kiarabu. Jibrilu (a.s) akasema: Mwite Hussein ".

ITHBATI JUU YA UIMAMU WA HUSSENI A.S

Kutoka kwa Fatimah Zahara (a.s) amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu saww aliingia kwangu nilipojifungua mtoto wangu Hussein (a.s) nikamkabidhi akiwa ndani ya kitambaa cha njano, ndipo akakitupa na kuchukua kitambaa cheupe na kumfunga nacho, kisha akasema :. Mchukue ewe Fatimah hakika yeye ni Imamu, mtoto wa Imamu baba wa Maimamu tisa, watatoka katika mgongo wake Maimamu (Makhalifa) wema na wa tisa wao ndio Mwakilishi (al Qaim) wao.[2]

Kutoka kwa Imamu Hassan a.s amesema: Hakika Hussein a.s ni Imamu (Khalifa) baada yangu baada ya kutoweka nafsi yangu, na roho yangu kutengana na mwili wangu. Na mbele ya Mwenyezi Mungu ana mirathi kutoka kwa Mtukufu Mtume saww ndani ya kitabu, Mwenyezi Mungu ameiongeza kwenye mirathi ya baba yake na mama yake. Mwenyezi Mungu alijua kwamba nyinyi ndio chaguo bora katika viumbe wake hivyo akamteua Muhammad kutoka kwenu, (awe Nabii), na Muhammad akamchagua Ally (kuwa wasii wake), naye Ally akanichagua mimi kwa ajili ya Uimamu (Ukhalifa), nami nimemchagua Hussein a.s (kuwa Khalifa baada yangu).[3]

Tarehe tatu Shaban, Amezaliwa Hussein, Nikijana wa peponi, Yeye na kakaye pia.

Yeye watatu Imamu, Kuiongoza Qaumu, Nikijana Mkarim, Shahidi alijifia.

Mtoto wa Haydari, Mwana Bint Rasuli, Alikuwa Jemedari, Dini Kuipigania.

Mtukufu Mtume saww alikuwa akimchezesha Imamu Hussein a.s kwa kumweka miguuni kwake na kumkumbatia kifuani mwake. Wakati mwingine alikuwa akimbusu na kusema :. Mimi ninatokana na Hussein na Hussein anatokana na mimi ".

Mtukufu Mtume saww amesema :. Ama Hussein a.s hakika yeye anatokana na mimi, na yeye ni mwanangu na mtoto wangu na mbora kushinda viumbe wote baada ya kaka yake.

Na yeye ni Imamu (Khalifa) wa waislamu, kiongozi wa waumini, Khalifa wa Mola mlezi wa viumbe wote, na msaada wa watakao msaada, kimbilio la wale watakao hifadhi na Hoja(dalili) ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake wote.

Na yeye ni chifu wa vijana wa watu peponi na mlango wa uokovu wa Ummah, amri yake ni amri yangu na kumtii Hussein ni kunitii Mimi, atakayemfuata huyo (Hussein a.s) ni katika Wafuasi (Shi'ah) wangu na atakayemuasi huyo si katika Wafuasi wangu ".[4]

Kutoka kwa A'azib anasema :. Nilimuona Mtume saww akiwa amembeba Hussein a.s na huku akisema :. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nampenda Hussein a.s nawe mpende.[5]

Mtukufu Mtume saww alikuwa amembeba Hussein bin Ally a.s juu ya shingo yake, ndipo mtu mmoja akasema :. Ni kipando kizuri kilioje ulichopanda ewe mtoto! "Mtume saww akasema :." Naye ni mpandaji mzuri alioje!.[6]

Ya'la al Amiriy amesema :. Nilitoka na Mtukufu Mtume saww kwenda kwenye chakula ambacho alialikwa, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaelekea watu akiwa mbele yao huku Hussein a.s akiwa na watoto wakicheza. Mtume wa Mwenyezi Mungu saww akataka kumchukua lakini mtoto (Hussein) akaanza kukimbia huku na kule, Mtukufu Mtume saww akamchekesha mpaka akamchukua. Akaweka mkono wake mmoja nyuma ya shingo yake na mwingine chini ya kudevu chake, na akaweka mdomo wake juu ya mdomo wa Hussain huku akimbusu, kisha akasema :. Hussein a.s anatokana na mimi na mimi natokana na Hussein a.s, Mwenyezi Mungu humpenda ampendaye Hussein, na Hussein ni Mjukuu chaguo la kwanza katika wajukuu wengine.[7]

Fuatana nami sehemu ya pili historia ya Maasum Hussein a.s

 


[1]. Ilalus Sharaiu, Jz 5 UK 137.

[2]. Kifayatul Athari UK 194.

[3].  Al Kafiy Jz 1 UK 301 hadithi 2.

[4]. Al A'amal cha Saduq UK 101.

[5]. Biharul anuwari Jz 43 UK 264 hadithi 16.

[6]. Sunanut Tirmidhiy Jz 5 UK 661 hadithi 3784.

[7]. Al Mustadrakul Sahihayn Jz 3 UK 177.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini