HISTORIYA YA IMAMU HUSSEIN (A.S) 10
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- Hassani Buss
- Chanzo:
- mailto:buHassani Busssihassan@gmail.com
IMAMU HUSSEIN (A.S)
SEHEMU YA KUMI
JIHADI YA IMAMU HUSSEIN BIN ALIY (A.S) 7.
SAFARI YA IMAMU HUSSEIN (A.S)
Ilipomfikia habari ya kuwa yazeed l.a amemtuma amru bin saad bin al aasi katika kikosi cha askari na amemuamuru kwenda kuhiji, na amempa uongozi wa hijja na kumuusia kumuuwa hussein (a.s) popote atakapomkuta, hussein (a.s) aliamua kutoka makkah kabla ya kumaliza hijja na akatosheka na umra, kwa kuchukia usije ukavunjwa utukufu wa nyumba ya mwenyezi mungu kwa ajili yake. Na kabla ya kutoka alisimama akahutubia kwa kusema:
"nashukuru mwenyezi mungu, anayoyataka mwenyezi mungu huwa na hakuna nguvu isipokuwa kutoka kwa mwenyezi mungu, na rehema za mwenyezi mungu zimuendee mtume wake. Mnyororo wa mauti uko juu ya kizazi cha adam kama mkufu katika shingo ya msichana, na hakuna kilichonipendezesha kwa waliotangulia kama shauku ya ayubu kwa yusufu.
na nimepewa hiyari ya mauti nitakayokutana nayo kana kwamba mishipa yangu inakatwa na wanyama wa jangwani baina ya nawawis na karbala, basi kwangu watajaza matumbo yao, meno yenye makali na panga zenye njaa, hakuna kuepuka siku iliyoandikwa, ridhaa ya mwenyezi mungu ni ridhaa yetu ahlul bayt,.
Tunasubiri kwa balaa yake na atatulipa malipo ya wenye kusubiri, haitajitenga kutoka kwa mtukufu mtume wa mwenyezi mungu nyama yake bali itakusanywa kwake katika makazi ya qudus, kwayo yataburudika macho yake, na kwayo itatekelezwa ahadi yake. Ee ambaye amejitolea damu yake kwetu, aliye tayari nafsi yake kukutana na mwenyezi mungu, basi aondoke pamoja na mimi nitaondoka asubuhi inshaallah.
Na kutoka kwake makkah ilikuwa ni baada ya siku nane dhulhija akiwa pamoja na ahlul bayt wake, waliokuwa watumwa wake, wafuasi (shi'ah) wake na miongoni mwa watu wa hijazi, basra, na kufah, ambao walijiunga naye wakati wa kukaa kwake makkah, na alimpa kila mmoja dinar kumi na ngamia anayebeba mizigo yake.
Muhammad bin hanafiyyah alimwendea usiku ambao asubuhi yake hussein (a.s) alielekea iraq na kumwambia :. Umeshajua hiyana ya watu wa kufah kwa baba yako na kaka yako, na mimi naogopa hali yako itakuwa ni hali ya waliotangulia, kaa hapa hakika wewe ni mtukufu mno katika haramu na ni mwenye kuihifadhi zaidi.
Hussein (a.s) akasema :. Naogopa yazeed bin muawiyyah l.a asije kuniuwa katika haramu na hatimaye nikawa mtu ambaye utukufu wa nyumba hii umevunjwa kwa ajili yake.
Ibn al hanafiyyah akamwamuru aende yemen au baadhi ya sehemu za bara, hussein (a.s) akamuahidi kuitafakari rai hii, na katika mapambazuko ya usiku huo hussein (a.s) aliondoka, ibn al hanafiyyah alimwendea na akashika hatamu ya ngamia wake akiwa ameshampanda, akasema : je hukuniahidi kutafakari yale niliyokuomba?
Imamu hussein (a.s) akasema :. Kweli lakini baada ya kukuacha alinijia mtume wa mwenyezi mungu na akasema :. Ewe hussein! Toka, hakika mwenyezi mungu ametaka kukuona ukiwa umeuliwa. ""
Muhammad bin hanafiyyah akasema :. Innaa lillaahi wainnaa ilayhi raajiuna. "na kwa kuwa muhammad hakua anajua sababu ya hussein (a.s) kubeba watoto katika hali hii! Hivyo hussein (a.s) alimwambia mwenyezi mungu mtukufu ametaka kuwaona wakiwa mateka.
Abdillahi bin ja'far at tayari akamwandikia barua ikiwa pamoja na watoto wake auni na muhammad. Ama baad :. Hakika mimi nakuombea kwa mwenyezi mungu usiondoke utakaposoma barua yangu hii, kwani mimi nakuogopea kwa upande huu isije ikawa ni mauti yako na kutekwa kwa familia yako ikiwa utauliwa.
Kisha abdillahi akachukua barua kutoka kwa gavana wa yazeed wa makkah amru bin saidi bin yahya bin said bin al'aasi, ikiwa imetoa hifadhi kwa hussein (a.s) na akajitahidi kubadilisha uamuzi alioutaka hussein (a.s), lakini abu abdillahi hakukubali na akamjulisha kwamba alimuona mtume wa mwenyezi mungu (s.a.w.w) katika usingizi na alimwamuru jambo ambalo hakuna budi ya kulitekeza, ndipo abdillahi akamuuliza juu ya ndoto yake, akasema :. Sikumweleza mtu wala sitaeleza mpaka nikutane na mola wangu mtukufu.
Abdullah bin abbas akamwambia :. Ewe mtoto wa ami! Hakika mimi najipa subira lakini inanishinda, kwani naogopea katika upande huu kuangamia na kutekwa, hakika watu wa iraq ni watu wa usaliti, basi usiwakaribie, ishi katika mji huu hakika wewe ni bwana wa watu wa hijazi, na watu wa iraq ingawa wanakutaka kama walivyodai basi wamkamate gavana wao na adui yao kisha waendelee, na kama utakataa isipokuwa kutoka basi nenda yemen kwani huko kuna ngome na watu, nayo ni ardhi pana na ndefu, na baba yako ana wafuasi (shi'ah) huko, na wewe utajitenga na watu, utawaandikia watu, utatuma wajumbe wako, hakika mimi nataraji wakati huo watakujia ambao wanakutakia maisha. "
Hussein (a.s) akasema :. Ewe ibn ammi, wallahi hakika mimi najua kwamba wewe ni mtoa nasaha mwenye kupenda, lakini nimeshaazimia kutoka. Ibn abbas akasema :. Kama utaenda usiende na wake zako na watoto wako, hakika mimi naogopa utauliwa na hali wao wanakuangalia. Hussein (a.s) akasema :. Wallahi hawataniacha mpaka watoe hii nyama katika mwili wangu na wakifanya hivyo mwenyezi mungu atawatawalisha atakayewadhalilisha mpaka wawe dhalili kuliko pamba anayoitumia mwanamke (wakati wa hedhi).
Na abu hurrah al asadiy akamwambia :. Hakika bani umayyah wamechukua mali yangu nikasubiri, wakakashifu utu wangu nikasubiri na wakataka damu yangu nikakimbia.
Hakubaki yeyote pamoja na hussein (a.s) makkah isipokuwa alihuzunika kwa kwenda kwake, na walipozidisha maneno kwake alikariri beti za mashairi ya ndugu wa ausi alipoyasoma pale alipoonywa na mtoto wa ammi yake kutopigana jihadi pamoja na mtukufu mtume wa mwenyezi mungu (s.a.w.w):
nitakwenda mauti siyo aibu kwa kijana, anaponuia haki na akapigana jihadi hali ni muisilam.
Na akashirikiana na wanaume wema kwa nafsi yake, akaaga kwa kuuliwa na akawakhalifu waovu.
Kisha akasoma "na jambo la mwenyezi mungu ni hukumu iliyopangwa. 33:37
وكان أمر الله مفعولا.
Wakaondoka.
Fuatana nami sehemu ya kumi na moja historia ya maasum hussein (a.s)