KIFO CHA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W)
- Imesambazwa tarehe
-
- Mwandishi:
- Hassani Buss
- Chanzo:
- mailto:buHassani Busssihassan@gmail.com
MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (SAWW), AFARIKI DUNIA.
28/swafar 11 Hijria 08/06/632 AD
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehem.
Shukran zote zinamustahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye katujaalia kuwa katika ummah wa Muhammad saww Sayyid (Bwana) wa Manabii.
Na aliye tujaalia kushikamana na utawala wa Sayyid (Bwana) wa mawasii Ally bin Abi Twalib as
Na ubora wa rehema na amani zimshukie Muhammad saww na kizazi chake kitukufu ambacho kimelindwa (kisifanye) uchafu (makosa) na kutoharishwa moja kwa moja.
Na rehema na amani ziwashukie Shi'ah (wafuasi) wao ambao wamesifiwa ndani ya Quran tukufu yenye hekima.
Mwenyezi Mungu anasema :. Wape habari njema waja ambao wanasikiliza (wanasoma) maneno na kufuata mazuri yake nao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza na wao hasa ndio wenye akili. 39 :18 Qur-an
Mtukufu Mtume Muhammad saww alifariki akiwa kifuani mwa Ally bin Abi Twalib as ndani ya Chumba cha Fatima as.
Imamu Aliy as anasema kuwa :. "Niliitwa na Mtume nikakaa naye karibu, nikampakata, akawa akininong'oneza kwa muda mrefu, mpaka mate ya Mtume yakanitiririkia!! Mtume Muhammad saww akakata roho akiwa kifuani kwangu!!!
إنا لله وإنا إليه راجعون
Hakika sisi ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea!!![1]
Mtukufu Mtume Muhammad saww amefariki tarehe 28 safar mwaka kumi na moja hijiria Sawa na tarehe 08 June 632 AD.
Mtukufu Mtume Muhammad saww Alizaliwa siku ya Jumatatu, amepewa utume siku ya Jumatatu, ameihama Makka siku ya Jumatatu, amefika Madina siku ya Jumatatu, na amefariki siku ya Jumatatu. Akiwa na umri wa miaka sitini na tatu 63 hadi leo umri wa Mtukufu Mtume Saww ni miaka 1493.
Familia ya Mtume ikakusanyika hapo tayari kwa mipango ya maziko.
Mwili wa Mtume Muhammad saww ulioshwa siku ya Jumanne. Ni watu sita, waliokuwapo kwenye huduma hii ya mazishi ni
(1) Ally bin Abi Twalib as
(2) Abbas Ibn Abdul Mutwalib
(3) Fadhil Ibn Abbas
(4) Qutham Ibn Abbasi
(5) Osama bin Zaidi bin Harithi
(6) Aus bin Khuli Ansari.[2]
Osama, mkuu wa jeshi la kwenda Roma (utawala wa warumi ulikuwa Siria kipindi hicho) alikuwa yuko Jurf, akiwa bado anawangojea maswahaba. Baadhi yao walimpelekea habari kwamba Mtume Muhammad saww alikuwa amefariki, na kwamba angepaswa arudi Madina. Alirudi , na Muda kidogo baadaye, Bwana wake akafariki.
Ally aliuosha mwili wa Mtume Muhammad saww wakati Osama akiwa anammwagia maji. Wakati mwili ulipo kwisha kuoshwa, Ally aliufunika na Sanda, na akauswalia. Kisha yeye akatoka nje, na akawaambia waislamu waliokuwa msikitini waende chumbani na kuswali swala ya maiti. Banu Hashim walikuwa wa kwanza kumswalia, na kisha Muhajirina na Ansari wakatekeleza wajibu huu.
Hapo Madina, palikuwa na wachimba kaburi wawili. Walikuwa ni Abu Ubayda bin al Jarrah na Abu Twalha Zayd bin Sahl. Waliitwa wote lakini Abu Twalha Zayd bin Sahl tu ndiye aliyepatikana. Alikuja akalichimba kaburi. Ally aliingia mle kaburini ili kulisawazisha vizuri. Kisha akanyanyua mwili wa Mtume kutoka pale chini, na akauteremsha taratibu ndani ya kaburi, akisaidiwa na ami yake Abbas na binamu zake. Kaburi kisha likafunikwa kwa udongo, na Ally akanyunyizia maji juu yake.
Abu Bakr bin Abi Quhafa na Umar bin khatabi na Abu Ubayda bin Jarrah na Wengineo hawakuhudhuria mazishi ya Mtume mkwe kipenzi Chao kitukufu Muhammad saww walikuwa kwenye ukumbi wa Bani Saaidah Saqifah wakicheza bahati nasibu ya madai ya Ukhalifa[3].
Mara tu baada ya Imamu Ally bin Abi Twalib as kutangaza kuwa Mtume Muhammad saww amefariki! Umar bin khatabi alikwepo karibu na maeneo hayo, lakini akagundua timu ya wanamapinduzi haijakamilika alichokifanya alichukua upanga akawa anazunguka huku na kule katika eneo la msikitini na nyumba ya Mtume. Anazuia watu wasiingie kuuaga na kushuhudia mwili wa Mtume wao baada ya Kufariki.
Umar Khattab kwa sauti yake ya juu akawa aonya : "Wanafiki" wanasema Mtume Muhammad saww amekufuru, na hakika Mtume hakufa, atakaye sema Mtume amekufa nitakata shingo yake. Mpaka (timu ya mapinduzi ilipo kamilika) Abu Bakr bin Abi Quhafa alipofika akitokea kijijini kwake Sunhi kwa mkewe, akaingia ndani alikolazwa Mtume Muhammad saww. Alipotoka akasoma aya ;. "Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa Visigino vyenu? Na atakaye rudi nyuma kwa Visigino vyake hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru. 3:144 Qur-an.
Umar Khattab akasema: "Wallahi, kana kwamba watu hawajui kuwa Aya hii ilishuka kwa Mtume."
Walipo tazamana timu ya mapinduzi imekamilika Abu Bakr bin Abi Quhafa Umar bin khatabi na Abu Ubayda bin al Jarrah wakaondoka kwenda kwenye ukumbi wa Bani Saaidah Saqifah kwa ajili ya uchaguzi[4].
Umar kamtukana Ally bin Abi Twalib as na Bani Hashim kwa ujumla kuwa ni wanafiki!! Dakika chache baada ya Mtume kufariki. Je Omari ni nani? Kwa mujibu wa wale wasemao kuwa kutukana maswahaba ni ukafiri?..........
Aisha mke wa Mtume baada ya kufanikiwa kumuuwa mme wake naye kakimbia hakuhudhuria mazishi ya Mtume mme wake hata kuombeleza na kuhuzunika hakushiriki.
Na hakuwepo nyumbani kwa Mtume siku mbili, mwenyewe mwana Aisha anasimulia hapa : "Wallahi hatukuelewa maziko ya Mtume mpaka tulipo sikia kelele za majembe usiku wa Jumanne wakati wakichimba kaburi[5].
إنا لله وإنا إليه راجعون
Msiba juu ya msiba Mtume hakuzikwa kitaifa, alizikwa kifamilia.
Walikuwepo wale waislamu, wengi wao wakitokana na watu wa kawaida, ambao walimpa Muhammad saww upendo wao na hakuna ambaye angeweza kukataa kwamba upendo wao ulikuwa ni halisi. Wakati Mtume alipofariki, walipatwa na majonzi ; walivunjika mioyo, na kwao wao ule Msikiti, mji na dunia yote ilionekana iliyotelekezwa.
Lakini hisia za masahaba wakubwa wa Muhammad saww kwenye kifo chake, zilikuwa tofauti. Wakati Muhammad saww alipofariki, masahaba wake wakuu hawakushtushwa na kifo chake. Kama kifo chake kiliwahuzunisha, wao hawakuonyesha kuhuzunika kokote. Kitu kimoja ambacho hawakukifanya, kilikuwa ni kutokutoa rambirambi zao kwa ile familia iliyoondokewa. Hakuna hata mmoja miongoni mwao aliye kuja na kuwaambia: "Enyi watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume Muhammad saww, tunachangia pamoja nanyi huzuni yenu
Kwa kifo chake. Kifo chake ni pengo sio kwenu tu bali kwetu sisi sote."
Katika wakati ambapo huruma inatarajiwa hata kutoka kwa wageni, kwa kweli, hata kwa maadui, haisadikiki lakini ni kweli kwamba maswahaba wa Muhammad saww, Mtume wa Mwenyezi Mungu waliinyima familia yake mwenyewe. Waliiacha familia yake kuombeleza kifo cha Mtukufu Mtume Muhammad saww yenyewe.
kinyume chake walienda na mapanga na vijinga vya moto na kuvamia familia ya Mtume saww bila ya huruma wala aibu na kuwaumiza wengine na wengine wakafungwa na kuburutwa hadi msikitini.
MWISHO wa historia ya Mtukufu Mtume Muhammad saww ni mwanzo wa kujua historia ya Fatimah bint Muhammad.
[1]. Rejea: At Tabaqatul kubra Jz 2 UK 263. Assiratun Nabawiyyah, ya Najahu Attai Jz 2 UK 316.
[2]. Rejea Tarekhul Tabariy Jz 3 UK 80. Almuntadham Jz 2 UK 477.
[3]. Rejea: Almuswannaf ya Ibn Abi Shaybat, babu Maghaz khilafatu Abi Bakr. Kanzul Ummal, kitabu khilafa maal imara khilafatu Abi Bakr.
[4]. Rejea :Nurul Absaar UK 57-59. Tarekhul Tabariy Jz 3 UK UK 67-69. Tarekhul Ibn Athir Jz 2 UK 219.
[5]. Rejea Tarekhul Tabariy Jz 3 UK 81. Assunanul kubra Jz 3 UK 574.Assiratun Nabawiyyah, ya Najahu Attai Jz 2 UK 314. Almuntadham Jz 2 UK 482.