Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W) 2

0 Voti 00.0 / 5

MAISHA YA BIBI FATIMA BAADA YA MTUME (S.A.W.W)  KUFARIKI

Sehemu ya Pili

NDANI YA NYUMBA YA FATIMA.

Katika nyumba ya Fatima yaliongelewa matukio ya vita vya mtume (S.A.W.W)kama vile Khandaq,Khaibar,n.k,na vilevile yaliongelewa matukio ya ushindi wa imamu Ally(A.S)katika vita hivyo na vinginevuo,kama ambavyo ziliongelewa katika nyumba hiyo habari za Jibraailul amiin(A.S).

Basi amani ya mwenyezimungu iwe juu ya nyumba ya Fatima.

UGONGAJI MLANGO WA FATUMA

Imenukuliwa kutoka kwa Ummu aiman ya kuwa amesema:

Fatima (A.S) alikuja nyumbani kwa mtume (S.A.W.W)na kugonga mlango,

Mtime (S.A.W.W)akamwambia Ummu Aiman ugongaji huu wa mlango ni wa Fatima.ummu Aiman akamwambia mtume (S.A.W.W)kwa mshangao ni hisia gani na uaminifu gani ulio nao hata unapo gongwa mlango unamfahamu mgongaji?.Mtume (S.A.W.W)akasema na kumjibu kwa mshangao ni maisha gani ya kupendeza aliyonayo Fatima (A.S)hata anapo gonga malngo hujulikana kuwa yeye ni Fatima(A.S).Kutokana na riwaya hii tuna kuta kwamba ugongaji wake wa mlango ulikuwa ni wa aina ya pekee, na vilele mtume (S.A.W.W)aliweza kumfahamu Fatima kupitia njia mbali mbali.

FATIMA NI MKUBWA KIMA ANAWIA

Maisha ya mtume na roho ya mtume vina nafasi kubwa kwa Fatima,kama vile ambavyo mtume hakuwahi kuabudia masanam,kwa dalili hii kutokana na utukufu wa mtume Fatima anakuwa mfano wa baba yake kima anawia,pamoja na kwamba kuna tofauti ya kima anawia kati ya Fatima na baba yake.Na kama ilivyo pokelewa katika hadithi.

((kumuudhi Fatma ni sawa na kumuudhi Mwenyezi Mungu na kumridhisha Fatima ni sawa na kuridhisha Mwenyezi Mungu)).

Mwili wake na moyo wake umebobea katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu,kwa mfanio huu MwenyeziMungu alitaka watu wajue nafasi ya Fatima (A.S)ambae ni mja mtii

fu. Na ndio maana Mwenyezi mungu akamfanya kuwa alama ya ghadhabu zake na radhi zake.

Vile vile imenukuliwa riwaya kutoka kwa mtume (S.A.W.W)ya kuwa amesma:

((Mwenye kumghadhibisha Fatima amemghadhibisha Mwenyezimungu na

Mwenye kumridhisha Fatima amemridhisha Mwenyezimungu)).

Kwa hivyo basi kila ambae ameridhiwa na Fatima Mwenyezi Mungu nae amemridhia na kila ambae Fatima amemghadhabikia Mwenyezi Mungu amemghadhabikia.

Kuna riwaya nyingi ambazo Mtume ame elezea ndani yake ubora,fadhila ,na cheo na ukubwa wa kima anawia wa Fatima (A.S).

Kwa ufupi hii ni historia fupi ya maisha ya na uhai wa Fatima (A.S).

TAWASSUL YA HADHRAT ADAM KWA FATIMA.

Imenukuliwa kutoka kwa ibnu Abbas ya kuwa amenukuu kutoka kwa Mtume (S.A.W.W)kuhusiana na neno ambalo alilipokea Adam kutoka kwa mola wake na kwa neno hilo akatubia kwa Mwenyezi Mungu.Ibnu Abbas akamuuliza Mtume , ((Ni neno gani hilo?))Mtume akajibu: Neno hilo ni kwa haki ya Mohammad,Ally,Fatima,Hassan na Hussen,na akatubia kupitia neno hilona toba yake kukubaliwa.

Fuatana nami katika makala ijayo kuhusu Maisha ya Mtukufu Huyu Baada ya Mtume (s.a.w.w) .

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini