MAKHALIFA KUMI NA MBILI KATIKA VITABU VYA PANDE MBILI
HADITHI YA MAKHALIFA KUMI NA MBILI, NI MAARUFU INAKUBALIWA NA WANAZUONI WA AHLISUNA NA SHI'AH IPO KATIKA VITABU VYA AHLISUNA NA SHI'AH KWA MATAMKO ZAIDI YA MATATU NA YOTE YANA MAANA MOJA.
BAADHI YA WANAZUONI WA AHLISUNA WA KISASA AMBAO HAWAJISHUGHULISHI NA KUFANYA UTAFITI WANADHANI HADITHI HII IPO KWA SHI'AH TU. NA WANABWETEKA NA KUNG'ANG'ANA NA HADITHI YA KHULAFAU RASHIDUNA WANNE, AMBAYO HAIPO HATA KWENYE VITABU VYA AHLISUNA
Kuna hadithi inasema: Katika ummah wangu kutakuwa na Maamiri kumi na mbili.
Kuna kauli nyingine inasema: Kuna Makhalifa waongofu kumi na mbili.
Kuna kauli nyingine inasema: Kutakuwa na Maimamu kumi na mbili.
Kuna kauli nyingine inasema: kutakuwa na watawala kumi na mbili.
Kwa hiyo, Mtukufu Mtume saww anaposema: Makhalifa kumi na mbili wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho ni Imamu Muhammad Bin Hassani Al Mahdy as.
Mtukufu Mtume saww akisema: Kutakuwa na Maamiri kumi na mbili, wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho wa Muhammad bin Hassani Al Mahdy as.
Akisema: Maimamu watakatifu baada yangu ni kumi na mbili, wa kwanza wao ni Ally Bin Abi Twalib as na wa mwisho wao ni Muhammad Bin Hassani Al Mahdy as
في الدين الإسلامي، جاء عن نبي الإسلام محمد أن أمر الإسلام سيظل قائماً وعزيزًا حتى يمضي 12 خليفة كلهم من قريش. وورد هذا الحديث في مصادر المسلمين سنة وشيعة بصيغ مختلفة.
Katika Dini ya Uislamu imekuja hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume saww anasema kuwa: Hakika jambo la Uislamu litaendelea kuwa imara na Tukufu mpaka watakapoisha Makhalifa waongofu kumi na mbili wote ni Maquraishi.
Hadithi imepokewa kutoka vyanzo vya Wanazuoni wa Kiislamu wote Ahlisuna na Shi'ah kwa matamko tofauti tofauti.
في كتب أهل السنة والجماعة روي عن جابر بن سمرة في صحيح البخاري:
Katika vitabu vya Wanazuoni wakubwa maarufu waliotangulia wa Ahlisuna Wal jamaa wamepokea hadithi kutoka kwa Jabir bin Samrah iliyo katika Sahihi Bukhari:
حديث الاثني عشر خليفة سمعت النبي ﷺ يقول يكون اثنا عشر أميرا فقال كلمة لم أسمعها فقال أبي إنه قال كلهم من قريش[1]، حديث صحيح حديث الاثني عشر خليفة
Kuna hadithi ya Makhalifa kumi na mbili, Jabir bin Samrah anasema: nilimsikia Nabii saww akisema: (katika ummah wangu) Kutakuwa na Maamiri kumi na mbili, kisha akasema maneno ambayo sikuyasikia baba yangu akaniambia (haya maneno ambayo hukuyasikia mimi nimeyasikia) amesema wote ni Maquraishi.
Hadithi ya Makhalifa kumi mbili hii kwa tamko la Maamiri kumi na mbili ni hadithi Sahihi.
روي عن جابر بن سمرة في صحيح مسلم:
Riwaya kutoka kwa Jabir bin Samrah iliyo katika Sahihi Muslim.
حديث الاثني عشر خليفة دخلت مع أبي على النبي ﷺ فسمعته يقول إن هذا الأمر لا ينقضي حتى يمضي فيهم اثنا عشر خليفة قال ثم تكلم بكلام خفي علي، قال: فقلت لأبي ما قال: قال كلهم من قريش[2]، حديث صحيح حديث الاثني عشر خليفة
Hadithi ya Makhalifa kumi na mbili, Jabir bin Samrah anasema: Niliingia mimi na baba yangu nyumbani kwa Mtukufu Mtume saww nikamsikia Nabii saww akisema: Hakika jambo hili la (Uislamu) halitoisha hadi wapite (watawale) kwa Waislamu Makhalifa kumi na mbili, kisha akatamka maneno mimi sikuyasikia, Jabir bin Samrah anasema: nikamuuliza baba (eti) amesema Je hapo mwisho, baba akasema: Mtume saww amesema: (Hao kumi na mbili) wote ni Maquraishi.
Hadithi hii kwa tamko la Makhalifa kumi na mbili katika Sahihi Muslim ni Sahihi.
روي عن حسن بن موسى في مسند الإمام أحمد:
Kuna riwaya kutoka kwa Hassani Bin Musa ndani ya kitabu Musnad Ahmad bin Hanbal:
حديث الاثني عشر خليفة قال حدثنا حماد بن زيد عن المجالد عن الشعبي عن مسروق قال قال كنا جلوسا عند عبد الله بن مسعود وهو يقرئنا القرآن فقال له رجل يا أبا عبد الرحمن هل سألتم رسول الله كم تملك هذه الأمة من خليفة فقال عبد الله بن مسعود ما سألني عنها أحد منذ قدمت العراق قبلك ثم قال نعم ولقد سألنا رسول الله فقال اثنا عشر كعدة نقباء بني إسرائيل.[3]، حديث مرفوع حديث الاثني عشر خليفة.
Hadithi hii ya Makhalifa kumi na mbili, Hassani Bin Musa anasema: Ametuhadithia Hamadi Bin Zaidi kutoka kwa Mujaalid kutoka kwa Sha'abiy, kutoka kwa Masruuq anasema: Tulikuwa tumekaa mbele ya Ibn Mas'ud akitusomea Qur-ani Tukufu, Mtu mmoja akasema: Ewe Aba Abdir Rahman ! Je mliwahi kumuuliza Mtukufu Mtume saww, kuwa ni Makhalifa wangapi watakaoutawala ummah huu?
Abdallah Bin Mas'ud Akasema: Swali hili tangu nije hapa Iraq hajaniuliza Mtu yeyote kabla yako, kisha akasema: ndiyo kwa hakika tulimuuliza Mtume saww akatuambia kuwa wakuwepo Makhalifa kumi na mbili kama Koo za Bani Israel.
Hadithi hii iliyo katika Musnad Ahmad bin Hanbal ya Makhalifa kumi na mbili ni Marfu'u.
ذكر كذلك الحديث بعدة ألفاظ مختلفة
Vilevile hadithi hii kaitaja kwa matamko tofauti tofauti.
وفي لفظ آخر: «(لا يزال هذا الدين قائما حتى يكون عليكم اثنا عشر خليفة كلهم تجتمع عليه الأمة)»، بزيادة لفظ (كلهم تجتمع عليه الأمة).[4]
Kuna tamko jingine linasema: Dini hii ya Uislamu haiachi kuwa ni yenye kudumu mpaka kuwe juu yenu na Makhalifa kumi na mbili, wote ummah utajikusanya kwao. (Kwenye tamko hili ameongeza tamko jingine la kusema wote watakusanyika kwao).
وفي لفظ آخر لمسلم : «(لَا يَزَالُ الْإِسْلَامُ عَزِيزًا إِلَى اثْنَيْ عَشَرَ خَلِيفَةً)».[4]
Na katika tamko jingine lililo ndani ya Sahihi Muslim, Mtukufu Mtume saww alisema: Uislamu hauachi kuwa ni wenye Utukufu hadi kuwe na Makhalifa kumi na mbili.
وفي لفظ آخر لمسلم: «(لَا يَزَالُ هَذَا الدِّينُ عَزِيزًا مَنِيعًا إِلَى اثْنَيْ عَشَرَ خليفه
Tamko jingine lililo ndani ya Sahihi Muslim, Mtukufu Mtume saww alisema: Dini hii haiachi kuwa ni dini Tukufu na yenye kuvutia hadi kuwe na Makhalifa kumi na mbili.
وفي لفظ البخاري فجاء فيه : «(يَكُونُ اثْنَا عَشَرَ أَمِيرًا - فَقَالَ كَلِمَةً لَمْ أَسْمَعْهَا فَقَالَ أَبِى إِنَّهُ قَالَ - كُلُّهُمْ مِنْ قُرَيْشٍ)».
Tamko jingine lililo ndani ya Sahihi Bukhari, Mtukufu Mtume saww alisema: Kutakuwa na Maamiri kumi na mbili, akasema neno ambalo sikulisikia baba yangu akaniambia hilo neno ambalo hujalisikia ni kuwa Mtume saww amesema: wote ni Maquraishi.
في كتب الشيعة:
Sasa tuangalie ndani ya vitabu vya Wanazuoni wakubwa maarufu waliotangulia wa Shi'ah.
لا يزال أمر أمتي ظاهرا حتى يمضي اثنا عشر خليفة، كلهم من قريش [5]
Kuna hadithi Mtukufu Mtume saww alisema: Jambo hili la ummah wangu (Uislamu) halitaacha kudhihiri (na kuenea) mpaka wapite (watawale) Makhalifa kumi na mbili wote ni Maquraishi.
عن جابر بن سمرة قال «أتيت النبي صلى الله عليه وآله فسمعته يقول: إن هذا الامر لن ينقضي حتى يملك اثنا عشر خليفة كلهم، فقال كلمة خفية لم أفهمها فقلت لأبي: ما قال؟ فقال: قال عليه السلام: كلهم من قريش»[6]
Kutoka kwa Jabir bin Samrah anasema: Nilienda kwa Mtukufu Mtume saww nikamsikia akisema: Hakika jambo hili la (Uislamu) halitoisha hadi watawale Makhalifa kumi na mbili wote, kisha akasema: kasema neno ambalo lilikuwa kwa sauti ya chini sikulifahamu, nikamuuliza baba eti amesema Je? Baba akasema: Mtume saww amesema wote ni Maquraishi.
حدثنا أحمد بن الحسن القطان قال: حدثنا عبد الرحمن بن أبي حاتم قال: حدثنا العلاء بن سالم، قال: حدثنا يزيد بن هارون، قال: أخبرنا شريك، عن سماك، وعبد الله بن عمير، وحصين بن عبد الرحمن قالوا: سمعنا جابر بن سمرة يقول «دخلت على رسول الله صلى الله عليه وآله مع أبي فقال: لا تزال هذه الأمة صالحا أمرها ظاهرة على عدوها حتى يمضي اثنا عشر ملكا - أو قال: اثنا عشر خليفة - ثم قال: كلمة خفيت علي فسألت أبي فقال: قال: كلهم من قريش»[7]
Kutoka kwa Samaak na Abdallah Bin Umayr na Huswein Bin Abdur Rahman wanasema: Tulimsikia Jabir bin Samrah akisema: Niliingia mimi na baba yangu nyumbani kwa Mtukufu Mtume saww, Mtukufu Mtume saww akasema: hauachi kuwa ummah huu ni wenye kuswafika jambo lake likidhihiri kwa adui wake mpaka wapite (watawale) Makhalifa kumi na mbili au kauli nyingine inasema: kuwe na wafalme kumi na mbili. Kisha akatamka maneno kwa sauti ya chini sikuyafahamu, nikamuuliza baba eti amesema Je? Baba akasema Mtume saww alisema wote ni Maquraishi.
Tafsiri ya Wanazuoni wa Ahlisuna na Shi'ah hazijapishana wote wanakubaliana.
Fuatana nami katika ufafanuzi wa hadithi ya Makhalifa kumi na mbili tutataja majina yao kwa hadithi Sahihi kutoka vitabu vya Wanazuoni wakubwa maarufu waliotangulia wa Ahlisuna na Shi'ah