Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MAMZAZI YA IMAMU MAHDY (A.J) 2

1 Voti 04.0 / 5

Kuzaliwà kwa IMAMU MÀHDI a.s 15 SHAABANI 255 HIJIRIA. - 2.

Mwenyezi Mungu Amesema katika Qur'an: "Wao (maadui) Wanapenda kuzima Nuru yake (Mwenyezi Mungu ) kwa vinywa vyao lakini Mwenyezi Mungu atakamilisha Nuru yake ijapokuwa wasioamini watachukia.9:32 Qur'an.

Maadui wa Mwenyezi Mungu hawakuacha jambo lolote katika jitihada zao za kumuumbua Mtukufu Mtume s.a.w.w na Ahlubayt wake a.s.  Wamewaua kwa kuwachinja au kuwapa sumu dhuria wa Mtume s.a.w.w moja baada ya moja, lakini "NURU" imeendelea kuangaza na itaangaza hadi siku ya Kiyama.

Khalifa (Mfalme) Mu'utamid aliyekuwa katika Makhalifa wa Bani Abbas alimweka kizuizini Imamu wa kumi na moja, Imamu Hassan Askàriy a.s, miaka mingi gerezani. Alikuwa ana habari kamili juu ya hadithi ya Mtume Muhammad s.a.w.w kwamba Imamu Hassan Askàriy atapata mwana ambaye ni Imamu wa kumi na mbili Imamu MÀHDI a.s na huyo ataanzisha na kustawisha utawala wa dhuria wa Mtume s.a.w.w Ulimwenguni na kuangamiza maadui wa Ahlubayt wa Mtume s.a.w.w. Kwa hiyo, alimweka Imamu Hassan Askàriy a.s gerezani kwa muda mrefu sana ili kuzuia biashara ya Mtume s.a.w.w.

Firaun alidai kwamba yeye ni Mungu. Wanajimi (watabiri) walimshauri kwamba kutokana na kizazi cha Bani Israel atazaliwa mtoto atayeangamiza ufalme wake, kumuua yeye (Firaun) , wafuasi na Maswahaba zake . Kwa hiyo Firaun akiweka ulinzi mkali juu ya wanawake wa Bani Israel: Kila mtoto wa kiume akizaliwa akiuliwa ili kuzuia kuzaliwà kwa Nabii Musa a.s. Hata hivyo, alivyotaka Mwenyezi Mungu ikawa. Nabii Musa alizaliwa katika nyumba hiyo hiyo ya Firaun. Licha ya kuzaliwà tu hata kulelewa nyumbani mwa Firaun. Kama vile alivyo Firaun, Mu'utamid alitaka Imamu MÀHDI a.s asizaliwe. Lakini hakuna mtu anayeweza kufaulu kuzuia amri ya Mwenyezi Mungu.

Katika kipindi Imamu Hassan Askàriy a.s alipokuwà kizuizini kulitokea ukame mkali sana Samarra. Kwa muda mrefu hapakunyesha mvua hata tone moja. Waislamu waliswali swala maalum ya kuomba mvua inyeshe lakini hawakufanikiwa. Wakati Waislamu wote walipokusanyika nje ya jiji la Samarra, padri mmoja wa Kikristo akanyanyua mikono yake kuomba Mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika na mvua ikanyesha kidogo. Kuona hivyo Waislamu wote walibabaika . Wakaanza kupatwa na wasiwasi kwamba labda Ukristo ni dini ya kweli. Khalifa Mu'utamid papo hapo akaitisha baraza lake na kuchukua ushauri wa wanavyuo, mawaziri na maofisa wake. Wote walipigwa butwaa. Mmoja wa washauri Wake akatoa wazo kwamba yuko mwokozi moja tu ambaye anaweza kuwaokoa, naye ni Imamu Hassan Askàriy a.s ambaye alifungwa gerezani. Khalifa Mu'utamid alikuwa na hakika (yakini) juu ya elimu, ukweli na Uimam wa Imamu Hassan Askàriy a.s na haki yake ya utawala (Ukhalifa). Akamwita Imamu Hassan Askàriy a.s katika baraza lake la kifalme.

 

Imamu Hassan Askàriy a.s alipofika, Khalifa Mu'utamid akasimama kwa taadhima, akamkaribisha, na akamkalisha karibu na kiti cha kifalme na kumweleza mambo yote. Imamu Hassan a.s akasema "Usiwe na wasiwasi. Hilo si jambo kubwa. Waamrishe Waislamu wote wakusanyike nje ya jiji kesho ili waswali na kuomba mvua inyeshe. Na wakati huo huo mwamrishe huyo Padri wa Kikristo afike". Kesho yake Waislamu wote pamoja na Yule Mkiristo walikusanyika huko. Imamu Hassan Askàriy a.s akamwambia huyo padri aombe Mungu na papo hapo mawingu yakakusanyika. Imamu Hassan Askàriy a.s akamuomba Khalifa Mu'utamid kumtuma mtu akalete kile kitu padri huyo alichoficha katikati ya vidole vyake. Khalifa Mu'utamid aliamrisha afisa wake akamnyang'anye kitu hicho, akamnyang'anya mfupa uliofichwa katikati ya vidole vya padri, na akamkabidhi Imamu Hassan Askàriy a.s. Imamu Hassan Askàriy a.s akaufunika huo mfupa kwa kitambaa na kukiweka hicho kitambaa mfukoni mwake. Papo hapo mawingu yaliyokusanyika yakatawanyika. Hapo Imamu Hassan Askàriy a.s akamwambia huyo padri amwombe Mungu ili inyeshe mvua. Padri huyo alijitahidi sana kumwomba Mungu lakini hakufanikiwa.

Hapo Imamu Hassan Askàriy a.s akamjulisha Khalifa Mu'utamid kwamba ule mfupa ulikuwa wa Nabii mmojawapo na wakati wowote unapowekwa chini ya mbingu basi mawingu hukusanyika. Imamu Hassan Askàriy a.s akiwaongoza Waislamu katika swala akanyanyua mikono yake mitakatifu. Papo hapo mawingu yakakusanyika pande zote. Imamu Hassan Askàriy a.s akawaamuru watu waende makwao na baadaye mvua kubwa ikanyesha. Imamu Hassan Askàriy a.s na Khalifa Mu'utamid walirudi kitaluni na hilo lilikuwa jambo pekee likizungumzwa na kila mtu.

Khalifa Mu'utamid alifurahi mno kwa sababu Uislamu umenusurika. Khalifa Mu'utamid na watu wote waliamini manufaa ya swala, ukweli na utawala wa Imamu Hassan Askàriy a.s. Baada ya muda Imamu Hassan Askàriy a.s akaondoka . Khalifa Mu'utamid alipomuuliza alikokuwa anaelekea Imamu Hassan Askàriy a.s akamjibu kuwa alikuwa anarudi kifungoni alimowekwa na Khalifa Mu'utamid. Kusikia hayo, Khalifa Mu'utamid aliona haya sana na akasema, "Eh mjukuu wa Mtume, tafadhali rudi nyumbani kwako".

Hapo Imamu Hassan Askàriy a.s alirudi nyumbani kwake. Katika muda huo Narjiskhatun (mama yake Imamu wa kumi na mbili) akawa mjamzito. Swalawaat!!!

Mwenyezi Mungu hukamilisha Nuru yake ijapokuwa Makafiri wanachukia 61:8. Qur'an

Fuatana nami sehemu ya kumi na tisa historia ya Imamu MÀHDI a.s

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini