Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

Makala

MAKALA MBALIMBALI
LENGO LA SHARAFU DIIN

LENGO LA SHARAFU DIIN

LENGO LA SHARAFU DIIN Umoja wa Umma wa Kiislamu, lengo kuu la uandishi wa Sharafu Deen. Hata kama, kama walivyokuwa wanazuoni wengine muhimu katika historia ya Kiislamu, Sayyid Sharafu Deen alipambana na ukoloni, lakini alikuwa akiamini kwamba changamoto na matatizo muhimu zaidi ya Ulimwengu wa Kiislamu, ni ya ndani na wala hayatokani na madui wa nje, na wakati huohuo kusisitiza kwamba utatuzi wa matatizo hayo unahitajia mbinu za kielimu na kimantiki. Kwa kawaida fikra, umashuhuri, kiwango cha elimu, ubunifu na kina cha fikra cha kila mwandishi hujulikana kupitia maandishi yake. Ni maandishi hayo ndiyo huwafanya wasomaji kutambua elimu kubwa na maarifa aliyonayo msomi fulani katika uwanja unaomuhusu wa kielimu na hivyo kumpa majina na lakabu kama vile 'ensaiklopidia', 'allama' au majina mengine yanayoonyesha mtu aliye na kipaji kikubwa cha elimu. Amma, kuna waandishi wachache mno ambao katika vitabu vyao hujishughulisha na masuala maalumu na kuchukua misimamo mahususi kuhusiana na utatuzi wa matatizo yanayoikabili jamii. Ni wazi kuwa waaandishi kama hao wana thamani na umuhimu mkubwa zaidi katika jamii kwa sababu huongoza na kuielekeza katika upande maalumu, ikiwa inafuatilia maalengo maalumu pia. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, waandishi kama hao huyachukulia maisha humu duniani kuwa na malengo maalumu. Huyatazama maisha ya kijamii ya Waislamu pia katika mtazamo huohuo. Suala hilo bila shaka hufungamana na jambo linalochukuliwa na waandishi hao kuwa muhimu na nyeti katika zama zao na kwamba jamii inahitajia swali, jibu na utatuzi wake wa haraka. Huenda likawa ni jambo la busara kuwaita waandishi kama hao kuwa ni wasomi warekebishaji wa jamii. Marekebisho bila shaka hufanyika katika masuala ya kijamii au mara nyingine ya kisiasa, ambayo huishughulisha jamii kifikra. Ni kutokana na hali kama hiyo ndipo wasomi kama hao wa Kiislamu huamua huchukua misimamo na kufuata njia maalumu katika kuwaongoza wafuasi wao kwenye njia nyoofu.

Midahalo
NJIA YA UZIMANI

NJIA YA UZIMANI

NJIA YA UZIMANI Njia ya uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache. UKWELI ni kwamba, Wakristo wana shahada (ubatizo) ambao hauhusiki na Nabii yeyote wa Mwenyezi Mungu. Sasa itakuwaje? Haya ni mambo ambayo Yesu aliyaona katika Roho kwamba watu watadanganywa kwa nguvu za shetani wamuitikadi kinyume na jinsi yeye mwenyewe alivyofundisha, hata akasema asiyeshika maneno yake atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba juu ya mchanga. Kujenga nyumba juu ya mchanga hata kama utaipamba namna gani na kuigharamia namna gani lakini ulilofanya ni sifuri (ziro). Mfano huu katika dini ni kushindwa kuelewa ile amri kuu (upweke wa Mungu) na kuwatambua Manabii wake wote kama alivyowaleta kwa haki ili wafundishe tumjue. Lile alilolilaani Yesu ndilo Wakristo wamelishika na lile alilolitukuza ndilo Wakristo wamelitupa. Hii inatokana na utabiri uliotoka mbali, kwani hata Nabii Isaya aliona katika Roho jinsi hali itakavyokuwa kuhusu chuo cha Qur'an kwani anasema: "... Vipofu wataona katika upofu na wenye akili, akili zao zitafichwa..." (Isaya 29:18) Qur'an imeletwa ili kuondoa giza. Basi wasiotaka kuelewa walete mfano wake kama wataweza (Qur'an 17:88). Na kama kweli ingelikuwa Qur'an ni mashairi aliyoyatunga Muhammad (s.a.w.) nadhani hicho kitabu kingesambaratikia mbali hata kizazi hicho kisijue jina la kitabu hicho isipokuwa labda katika historia tu.

Misingi mikuu ya Dini
UKHALIFA

UKHALIFA

UKHALIFA JAWABU KWA SHEIKH MAZRUI Baada ya kifo cha mtume Suala la Ukhalifa ni suala nyeti sana, sina budi kabla ya kumjibu Bwana Juma Mazrui niwaletee habari muhimu zilizotokea kabla ya tukio la Ukkhalifa na kama zilivyoelezwa na Hadithi sahihi na masimlizi ya Historia katika Vitabu tunavyovitegemea: Sina budi kumshukuru Bwana Juma Mazrui kwa jitihada zake za kutaka kuwaelewesha watu kuwa Seyyidna Ali hakuwa Khalifawa Kwanza wa Waisilamu, pia nawaomba wasomaji pia wawe na subira katika kusikiliza Upande wa pili wa maoni ya Waisilamu Huru usiotaka kushutumu yo yote kati ya Shia na Sunni juu ya suala hili. Kwanza kabisa, Mtume Muhammad alikufa mwaka 632 AD, alikufa kutokana na ahadi yake kufika na baada ya kupewa sumu kule Khaybar baada ya kuiteka ngome ya wayahudi wa Khaybar. Mtume Muhammad (s) baada ya ushindi wake dhidi ya Mayahudi wa Khaybar alikubaliana nao na kuwapa sharti ya kulipa jizya, walilipa nusu ya mazao wanayovuna hapo Khaybar kwa Dola ya Kiislamu ya Madina. Baada ya kufa kwa Mtume Muhammad (s) mayahudi waliobakia Khaybar waliondolewa na kufukuzwa kutoka madina na Khalifa wa pili Omar Bin al-Khattab.

MAKALA MBALIMBALI
SEREKALI YA MTUME (S.AW.W)

SEREKALI YA MTUME (S.AW.W)

SEREKALI YA MTUME (S.AW.W) Ushahidi na nyaraka za historia za kabla ya kudhihiri Uislamu zinaonyesha kuwa hakukuwepo utawala na serikali katika ardhi ya Hijaz na kwamba maisha ya Waarabu wa jangwani hayakutawaliwa na mfumo makhsusi wa kisiasa. (1) Ni baada ya kudhihiri dini ya Uislamu huko Makka na kuhamia Mtume Muhammad katika mji wa Madina ndipo mtukufu huyo alipoanzisha serikali kuu na kubadili mfumo wa kikabila uliokuwa ukitawala kwa kuasisi mfumo mpya wa kisiasa na kijamii. Mbali na kutoa mafunzo na malezi kwa jamii ya watu wa Hijaz, Mtume Muhammad (saw) pia aliongoza yeye binafsi jamii changa ya Kiislamu na kushika hatamu za mfumo wa kijamii wa Waislamu katika nyanja mbalimbali za sheria, utamaduni, siasa, masuala ya kijeshi na kiuchumi.(2) Suala hilo linaonekana wazi zaidi katika mtazamo wa aya za Qur'ani na ushahidi wa kihistoria kiasi kwamba hata wataalamu wa masuala ya Mashariki (orientalist) wasiokuwa Waislamu wamelifafanua kwa uwazi zaidi. Msomi wa Kitaliano Fel Lino anasema: Mtume Muhammad (saw) aliasisi dini na dola kwa pamoja na masuala yote hayo mawili yalipanuka na kukuwa sambamba katika kipindi cha uhai wake. (3) Dr. Strotmann anaamini kwamba: Uislamu ni tukio la kidini na kisiasa, kwani muasisi wake mbali na kuwa Mtume alishika hatamu za serikali na alikuwa na utaalamu kamili wa kuongoza serikali". (4) Hata hivyo katika karne za hivi karibuni baadhi ya waandishi (5) wametilia shaka uhakika kwamba serikali ya Mtume Muhammad (saw) ilikuwa serikali yenye uhusiano na wahyi na mafundisho ya Mwenyezi Mungu kutokana na kuathirika kwao na mafundisho ya fikra za kisekulari yanayotilia mkazo kutenganishwa dini na siasa. Waandishi hao wanasisitiza kuwa suala la serikali na uongozi ni suala la kibinadamu lizilokuwa na uhusiano wowote wa dini. Wanadai kuwa Nabii Muhammad (saw) hakuwa kiongozi wa kisiasa wala hakuamrishwa na Mwenyezi Mungu kuunda serikali na kuongoza masuala ya jamii. Kwa msingi huo, kama mtukufu huyo aliunda serikali na kuongoza masuala ya jamii alifanya hivyo kutokana na haja ya jamii hiyo na si wajibu wa kidini kutoka kwa Mwenyezi Mungu!

Elimu ya fiq-hi
IBADA YA HIJA

IBADA YA HIJA

IBADA YA HIJA Hija ni ibada kubwa inayokusanya ibada kadhaa. Umuhimu wa ibada ya hija umo katika ahadi iliyowekwa baina ya mja na Mola wake Muumba. Imepokelewa katika hadithi zinazotaja utukufu wa ibada ya hija kwamba "Mtu anayefariki dunia hutamani kwamba laiti angetoa dunia na yaliyomo kwa ajili ya kufanya hija walau mara moja katika maisha yake. Imam Ja'far Sadiq (as) ambaye ni miongoni mwa Watu wa Nyumba tukufu ya Mtume wetu Muhammad (saw) amesema: "Watu wanaofanya hija au umra ni wageni wa Mwenyezi Mungu. Kama watakuwa na haja basi atawakidhia, na kama watamuomba, atajibu maombi yao, na iwapo watanyamaza kimya na wasimuombe chochote, basi Yeye Mwenyezi Mungu atawapa bila ya wao kumuomba." Hija ni ibada inayokusanya mambo mengi yanayomkurubisha mja kwa Mola wake Karima. Ni shule ya kutoa malezi na maarifa kwa waja kwa msingi wa tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Safari hiyo ya hija huanza kwa kuwekwa nia safi na ikhlasi na kukamilika kwa ibada na amali makhsusi. Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu huanza ibada hiyo kwa kufanya ihram katika maeneo maalumu yanayojulikana kwa jina la Miqaat na hapo huvaa vazi la ihram.

Imam Baaqir (a.s)
MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S)

MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S)

MAISHA YA IMAMU BAAQIR (A.S) Tarehe saba mwezi wa Dhihijja inasadifiana na siku ya kukumbuka siku aliyoaga dunia mmoja wa wajukuu watoharifu wa Mtume Muhammad (saw). Tonakupeni mkono wa pole enyi wapenzi Waislamu kwa mnasaba huu mchungu na tunakukaribisheni kusikilza machache kuhusu maisha ya mtukufu huyo. Siku ambayo habari za kuaga dunia Imam Muhammad Baqir (as) zilienea katika mji mtakatiu wa Madina, mji huo ulighubikwa na huzuni kubwa ya wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). Hii ni kwa sababu hawakuwa wakiuona tena uso wenye nuru wa mjukuu huyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wala kusikia sauti yake changamfu na yenye kutuliza nyoyo katika Msikiti wa Mtume (saw). Hali hiyo ya huzuni iliwaathiri zaidi wafuasi wa karibu wa Imam Baqir na hasa Jabir bin Yazid Ju'fi. Siku na wakati ulikuwa ukimpitia kwa tabu kubwa Jabir. Alikuwa na kumbukumbu nzuri na ya kuvutia kutoka kwa Imam Baqir (as). Alipomwona Imam kwa mara ya kwanza, alikuwa kwenye Msikiti wa Mtume (saw) ambapo alikuwa amezungukwa na watu walioonekana kuwa na hamu kubwa na kusikiliza kwa makini maneno ya hekima aliyokuwa akiyasema. Imam alikuwa akizungumzia utafutaji elimu na umuhimu wake. Alipomkaribia, alimsikia Imam akisema: "Tafuteni elimu, kwa sababu utafutaji elimu ni jambo zuri. Elumu ni mwongozi wako kwenye giza, msaidizi wako katika mazingira magumu na rafiki mwema wa mwanadamu."

MAKALA MBALIMBALI
KUKOMBOLEWA QUDS

KUKOMBOLEWA QUDS

KUKOMBOLEWA QUDS Abdallah Fahd, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kuwait amesisitiza kwamba kukombolewa kwa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya utawala ghasibu wa Israel kunahitajia muamko, azma na irada thabiti ya Waislamu wote duniani. Akizungumza katika kikao cha kimataifa cha "Quds katika Dhamiri ya Waarabu" kinachofanyika mjini Kuwait na ambacho kimefunguliwa na Nasir Muhammad Ahmad Swabah, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Fahd amesema kuwa nchi za Kiislamu zinapasa kuwa na mikakati madhubuti na ya pamoja kwa ajili ya kuikomboa Quds kutoka mikononi mwa walowezi wa Kizayuni. Amesema kuwa jambo hilo litathibiti tu iwapo nchi za Kiislamu zitaamua kushirikiana na kuwa na umoja pamoja na urafiki miongoni mwao. Amesema nchi za Kiislamu na Kiarabu zina majukumu mazito kuhusiana na suala la Palestina. Amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba utawala ghasibu wa Israel umewafukuza mamilioni ya Wapalestina kutoka kwenye ardhi zao za jadi na kuwafanya waishi kama wakimbizi katika ardhi zao wenyewe na kwingineko huku ukiharibu kabisa sura ya mji wa Quds Tukufu ambao zamani ulikuwa nembo ya umoja na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti.

MAKALA MBALIMBALI
VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA

VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA

VIZUIZI NA CHANGAMOTO ZA UMOJA Umoja wa umma wa Kiislamu ni lengo muhimu na aali ambalo wanafikra na maulamaa wa Kiislamu wamekuwa wakifanya jitihada kubwa tangu zama za awali za Uilslamu kwa ajili ya kufikia lengo hilo. Hivi sasa tumo katika Wiki ya Umoja kati ya Waislamu ambayo ilitangazwa na hayati Imam Khomeini kutokana na hitilafu za mapokezi kuhusu siku aliyozaliwa Mtume Muhammad (saw). Wiki hiyo inaanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal. Makala hii inazungumzia Umoja wa Umma wa Kiislamu, Vizuizi na Changamoto. Umoja wa umma wa Kiislamu ni lengo muhimu na aali ambalo wanafikra na maulamaa wa Kiislamu wamekuwa wakifanya jitihada kubwa tangu zama za awali za Uilslamu kwa ajili ya kufikia lengo hilo. Hadi sasa kumetolewa fikra nyingi na kuitishwa vikao na mikutano chungu nzima kujadili kadhia ya udharura wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya Waislamu wote. Udharura wa umoja na mshikamano wa Kiislamu umesisitizwa mno katika maandiko ya kidini na dalili za kimantiki na kiakili. Hata hivyo inasikitisha kwamba Waislamu wanapokaribia kuungana na kuimarisha umoja na mshikamano wao hujitokeza vizuizi chungu nzima ambavyo kunahitajika juhudi kubwa, tadbiri na mwamko wa Waislamu ili kuweza kuviondoa na kukabiliana navyo. Baadhi ya vizuizi na vikwazo vya umoja wa Waislamu vinatokana na hitilafu za ndani ya umma wa Kiislamu japokuwa hapana shaka kwamba wakoloni na madola ya kibeberu daima yamekuwa yakifanya njama za kuzusha hitilafu na mifarakano katika umma wa Kiislamu.

MAKALA MBALIMBALI
UMOJA WA WAISLAMU

UMOJA WA WAISLAMU

UMOJA WA WAISLAMU Ayatullah Ali Taskhiri, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Fars amebainisha malengo na shughuli za taasisi hiyo katika kukabiliana na vitendo vya uchochezi na mgawanyiko dhidi ya Waislamu. Amesema Taasisi ya Kukurubisha pamoja Mahdhebu ya Kiislamu imekuwa na nafasi muhimu katika kunyanyua uelewa wa Waislamu na kwamba ili kufikia lengo hilo taasisi hiyo imetuma jumbe mbalimbali katika vikao vya kimataifa na pia katika nchi tofauti kwa madhumuni ya kuondoa sutafahumu na shubha za kidini. Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukurubisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema, kuongezeka kwa uelewa katika ulimwengu wa Kiislamu kumekuwa na nafasi muhimu katika kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu na kwamba hilo ni moja ya malengo muhimu ya taasisi hiyo. Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amesema kuwa juhudi kubwa zimefanywa na zingali zinafanywa na mabeberu wa dunia kwa lengo la kuharibia jina la Uislamu na Ushia na hasa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Wanavyuoni wa Kiislamu
SHEIKH SHALTUT

SHEIKH SHALTUT

SHEIKH SHALTUT Sheikh Shaltut: "Madhehebu ya J'afariya maarufu kwa jina la madhehebu ya Shia Ithnaashariya, ni madhehebu ambayo kisheria inajuzu kufuatwa kama zilivyo madhehebu za Kisuni. Kwa msingi huo, ni vyema kwa Waislamu kuelewa ukweli huo na kujiepusha na taasubi (chuki za kimadhehebu) zisizofaa dhidi ya madhehebu makhsusi; kwani dini ya Mwenyezi Mungu na sheria yake haifuati madhehebu wala haiwezi kuhodhiwa na madhehebu makhsusi. Watu wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu wanafanya ijtihadi na kazi yao hiyo itatakabaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu." Sheikh Mahmoud Shaltut alizaliwa tarehe 5 Shawwal mwaka 1310 (Aprili 23, 1893) katika kijiji cha Minyat Bani Mansur katika mkoa wa Buhayrah nchini Misri katika familia ya wanazuoni. Baba yake Sheikh Muhammad alimpa jina la Mahmoud na akafanya jitihada kubwa za kumlea na kumuelemisha mwanae.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini