Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UISLAMU KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

0 Voti 00.0 / 5

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.

UISLAMU KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

Sarojini Naidu
(1879-1949) Mwanamke huyu ni Mwandishi, Mshairi, ambaye pia alikuwa ni mmoja mwa viongozi mashuhuri India kabla ya uhuru. Rais wa chama cha Indian National Congress na ni Gavana wa kwanza mwanamke baada ya India kupata uhuru. Amesema: " "Uadilifu ni moja kati ya maadili mazuri zaidi ya Uislamu, kwa kuwa nisomapo Qur'an nakuta kwamba misingi hii maisha, si nadharia tu bali ni maadili hasa ya kivitendo katika maisha ya kila siku yanayofaa kwa ulimwengu mzima."

" "Ilikuwa ni dini ya kwanza iliyohubiri na kutekeleza kwa vitendo demokrasia, kwani kunapoadhiniwa na waaabuduo wanapokusanyika, ndipo demokrasia ya kiislamu inapodhihirika mara tano kwa siku, pale mfalme na mkulima wanapoinama bega kwa bega na kusema: "Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mkuu." Nimekuwa nikiathiriwa mara kwa mara na umoja huu wa kiislamu usiogawanyika unaomfanya mtu moja kwa moja kumpenda mwingine na kumfanya kuwa nduguye."
[Hotuba iitwayo "The Ideals of Islam;" Tazama: Speeches and Writings Of Sarojini Naidu, Madras, 1918, Uk. 167-9]

Arnold J. Toynbee
(1889-1975) Mwanahistoria Mwingereza, Mhadiri katika Chuo kikuu cha Oxford. " "Kutokuwa na ubaguzi kati ya Waislamu ni moja kati ya mafanikio ya kipekee kabisa ya Uislamu, na kwa jinsi ulimwengu wa sasa ulivyo, kuna haja kubwa sana ya kuenezwa maadili haya ya Kiislamu."
[Civilization On Trial, New York, 1948, Uk. 205]

William Montgomery Watt
(1909- ) Profesa (Emeritus) wa lugha ya Kiarabu na taaluma ya dini ya Kiislamu katika Chuo kikuu cha Edinburgh. " "Mimi si Muislamu kama ijulikanavyo hasa, japokuwa nataraji kuwa ni "Muislamu" yule "anayemnyenyekea Mwenyezi Mungu," lakini naamini kwamba kilichomo ndani ya Qur'an na maelezo mengine ya mtazamo Kiislamu ni hazina kubwa ya ukweli wa dini ya Mwenyezi Mungu ambayo mimi na watu wengine wa Kimagharibi tuna mengi ya kujifunza kutoka kwayo, na kwa hakika Uislamu ndio mshindani mkubwa katika kuleta msingi mkuu wa dini moja ya wakati ujao."
[Islam And Christianity Today, London, 1983, Uk. ix.]

"Ambao husikiliza kauli (nyingi zinazosemwa), wakazifuata zile zilizo njema. Hao ndio aliowaongoza Mwenyezi Mungu, na hao ndio wenye akili." (Qur'an 39:18)
Wasemavyo wasio Waislamu juu ya…
Uislamu
DINI INAYOKUA KWA HARAKA ZAIDI ULIMWENGUNI
Huuni mkusanyiko wa nukuu fupifupi kutoka kwa watu mbalimbali mashuhuri wasiokuwa Waislamu, wakiwamo wasomi, waandishi, wanafalsafa, washairi, wanasiasa na wanaharakati wa Kimashariki na wa Kimagharibi. Tujuavyo ni kwamba hakuna hata mmoja mwao aliyewahi kuwa Mwislamu. Hivyo basi, maneno haya yanaonyesha maoni yao binafsi juu ya mitazamo mbalimbali wa dini ya Kiislamu.

Bertrand Russell
(1872-1970) Huyu ni Mwanafalsafa wa Kiingereza, Mwanahisabati, na mshindi wa tuzo la umalenga la Nobel, ambaye msisitizo wake katika utafiti wa kimantiki uliathiri sana mwelekeo wa falsafa ya karne ya ishirini. Amesema: " "Matumizi yetu ya neno 'the Dark Ages' (zama za giza) tunapotaja kipindi cha kuanzia mwaka 699 mpaka 1,000, yanaonyesha kuwa tunazingatia Ulaya ya Magharibi…Kutoka India hadi Uhispania, maendeleo makubwa ya Kiislamu yalinawiri. Kile kilichopotelea kwa Ukristo wakati huo hakikupotelea kwenye maendeleo ya ustaarabu, bali ni kinyume chake…Kwetu sisi yaonekana kuwa ustaarabu wa Ulaya ya Magharibi ndio ustaarabu, lakini haya ni maoni finyu."
[History of Western Philosophy, London, 1948, Uk. 419]

Hamilton Alexander Roskeen Gibb
(1895-1971) Huyu ni mtaalamu bora wa mambo ya Mashariki wa wakati wake. Asema: " "Lakini Uislamu ungali na huduma ya kutoa kwa wanaadamu. U karibu zaidi na Mashariki halisi kuliko Ulaya ilivyo, na una maadili ya maelewano na ushirikiano wa tabaka mbalimbali. Hakuna jamii nyingine yoyote yenye kumbukumbu ya mafanikio ya kuweza kuwaunganisha matabaka ya makabila mbalimbali ya wanaadamu katika usawa wa hadhi, nafasi na juhudi kama Uislamu… Uislamu bado una nguvu ya kuzipatanisha tabaka ambazo haiwezekani kuzipatanisha. Iwapo upinzani ulioko wa jamii kubwa za Kimashariki na Kimagharibi yapasa ufanywe kuwa ushirikiano, basi upatanishi wa Uislamu ndio ufaao kabisa. Mikononi mwake mna uamuzi wa tatizo linaloikabili Ulaya juu ya uhusiano wao na Mashariki."
[Whither Islam, London, 1932, Uk. 379.]

" "Kwamba mageuzi yake (Muhammad) yaliyooongeza ubora wa hali ya wanawake kwa ujumla, yanakubalika ulimwengu mzima." [Mohammedanism, London, 1953, Uk. 33]

James A. Michener
(1907-1997) Huyu ni Mwandishi mahiri Mmarekani; aliyepokea tuzo la heshima ya honorary doctorate, kutoka kwenye Vyuo vikuu 30 katika nyanja tano za kielimu, pia alipata nishani ya Rais ya uhuru, ambayo ni tuzo kubwa zaidi kwa raia wa Marekani. Amesema:
" "Katika historia, hakuna dini iliyoenea kwa kasi sana kama ya Uislamu . . . Wamagharibi waliamini kwamba kuenea huku kulisababishwa na upanga. Lakini hakuna msomi yeyote wa kisasa anayekubali nadharia hii, na Qur'an iko wazi juu ya suala la kuunga mkono uhuru wa dhamira ya kukubali ukweli na uongo." [Islam - The Misunderstood Religion, Readers' Digest (Toleo la Amerika) Mei 1955]

Edward Gibbon
(1737-1794) Mwanahistoria mkuu wa Kiingereza wa wakati wake. Amesema: " "'Naamini Mungu mmoja na Mohammed ni Mjumbe wa Mungu' kutamka hivi ni jambo la kila siku katika Uislamu. Dhahania ya kiakili ya Mungu katu haijavunjiwa heshima na vimungu-sanamu vyovyote vinavyoonekana; heshima ya Mtume katu haijavunja heshima ya sifa nzuri za mwanaadamu, na miongozo yake imehifadhi ridhaa ya wafuasi wake ndani ya mipaka ya mantiki na dini."
[History Of The Saracen Empire, London, 1870, Uk. 54.] " "(Uislamu) ni msafi zaidi kuliko mfumo wa ki-Zorosta. Ni wenye kupenda mambo ya wasitani kushinda sheria za Musa, dini ya Mohammed yaonekana kidogo yakubaliana na hoja kuliko imani za kishirikina ambazo, katika karne ya saba, ziliudhalilisha usahali wa Injili."
[The History of the Decline and Fall of the Roman Empire, Juz. 5. Uk. 487]

Jared Diamond
Profesa wa Saikloogia katika UCLA School of Medicine; aliyepokea zawadi ya Pulitzer for General Non-Fiction mnamo mwaka 1998. amesema:
" "Enzi za kati (1100-1500) Uislamu ulikuwa umepiga hatua kubwa katika teknolojia, na maendeleo. Ulifikia kiwango cha juu sana cha elimu kuliko Ulaya ya wakati huo; ulikuza tirathi za Kigiriki za zamani za kimaendeleo kiasi kwamba vitabu vingi vya zamani vinavyojulikana kwetu hivi leo tumevijua kupitia kwa nakala za Kiarabu. Uislamu umeunda Vinu vya upepo (Windmills), Trigonometria (Hesabu ya uhusiano kati ya pembe na pande zake tatu), Tanga la pembe tatu (Lateen sails), pia ulileta maendeleo makubwa katika ufuaji wa vyuma, uhandisi wa Kemikali na kimitambo na njia za umwagiliaji maji. Katika enzi ya kati, Teknolojia ilikuwa ikimiminika kutoka kwa Uislamu kwenda Ulaya, na si Ulaya kwenda kwa Uislamu, ila tu baada ya miaka ya 1500 ndipo mwelekeo huo wa mmiminiko ulianza kugeuka na kuwa kinyume."
[Guns, Germs, and Steel - The Fates of Human Societies, 1997, Uk. 253]

Annie Besant
(1847-1933) Rais wa The Indian National Congress in 1917. Amesema: " "Daima nadhani kuwa mwanamke, katika Uislamu, ana uhuru zaidi kuliko katika Ukristo. Mwanamke analindwa zaidi na Uislamu kuliko imani nyingione inayohubiri ndoa ya mke mmoja. Katika Qur'an sharia imuhusuyo mwanamke ina uadilifu na sahali zaidi. Ni katika kipindi cha miaka ishirini tu iliyopita Ukristo wa Uingereza ulipotambua haki ya mwanamke ya kumiliki mali, ambapo Uislamu uliruhusu haki hiyo kutoka wakati wote." [The Life and Teachings of Muhammad, Madras, 1932, Uk. 25, 26]

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini