Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SABABU 7 ZA KUSOMA QURANI

0 Voti 00.0 / 5

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

SABABU 7 ZA KUSOMA QURANI

(1) BAYANA Jee Utathubutu Kuikanusha vipi ?, Quran inatueleza wazi kuwa Binaadamu hatoweza kuandika kitabu kama hiki hata wakijikusanya pamoja na Kila kitu walichonacho ama rasilimali yoyote ile wanayoweza kuipata.

(2) HAKIPINGIKI Ni Maandishi pekee Matakatifu ambayo yapo kwa muda mrefu na yatabaki kama yalivyoteremshwa. Ndani yake humo hakitaongezwa wala kupunguzwa chochote.

(3) HAKIPITWI Qurani ni ufunuo wa mwisho kutoka kwa ALLAH kwa wanadamu wote, Mungu alimpa ufunuo wa Tawrat Mussa, Akampa Daud Zabur, Injil akapewa Isa na Muhammad akapewa Quran.Rehma na Amani za Allah ziwe juu yao wote. Hakuna kitabu chengine kitakacholetwa kutoka kwa Allah kuondoa ufunuo huu wa Mwisho.

(4) HAKIPINGIKI Qurani imesimama madhubuti kwenye majaribio na utafiti mwingi. Na hakuna aliekuja na sababu madhubuti za kuipinga ukweli uliomo ndani yake. Qurani inazungumzia mambo yaliopita na kinaonekana kinaeleza ukweli. Kimeeleza kuhusu Manabii waliotangulia na kimeonekana ukweli wake na kinachambua na kueleza mambo ya kuustajibisha ambayo yalikuwa hayajulikani na watu katika wakati huo. Na bado mambo ya uchunguzi na utafiti wa Sayansi umegundua na kuthibitisha ya kwamba Quran ishaeleza mambo hayo zamani kabisa. Kila kitabu huwa kinahitaji mapitio kuhakikisha kinakwenda na mahitaji ya wakati uliopo. Qurani ni kitabu pekee ambacho hakihitaji kupitiwa ili kukidhi mahitaji ya wakati ulipo, Qurani ipo imara na ipo kwa Wakati. (up to date).

(5) RAMANI YA MAISHA Qurani ni kitabu pekee bora ambacho kitakuonyesha jinsi gani ya kupanga maisha yako. Hakuna kitabu chengine ambacho kimepanga mpangilio bora wa maisha yako kama Qurani. Mpangilio ambao unajumuisha kila kitu ambacho mwanadamu anahitaji katika maisha yake. Qurani pia hukuonyesha jinsi ya kuweza kufanikiwa kupata maisha yako ya Akhera yenye furaha ya Milele.

(6)ZAWADI YA MUONGOZO KUTOKA KWA MOLA Mungu bado hajakuacha pekee yako, umeumbwa kwa sababu kisha amekuambia kwanini amekuumba, na nini anataka kuona kutoka kwako, na zawadi gani amekutayarishia juu yako. Kama vile Mwanadamu akiunda mashine huwa anaitolea kitabu cha malelezo ya jinsi ya kuitumia mashine ile, na ukienda kinyume na maelezo yake basi mashine itaharibika. Jee vipi sasa kuhusu wewe ? Jee si yapo maelezo kwa yule aliekuumba ?. Qurani ni mafanikio yako na ukiiacha utaharibika,Qurani inakujengea Imani kwa Mungu,Inakufanya moyo wako uwe umekinai,na inakusafisha moyo kwa kila matanio machafu pia inakuhakikishia usalama wa maisha yako.

(7) NI CALLING CARD YAKO Binadamu viumbe wenye Mashirikiano. Binadamu anapenda mawasiliano yenye kuleta maarifa kwenye Maisha yake. Qurani inamfahamisha jinsi gani ya kuweza kuwasiliana na mambo yote anayoyahitaji. Qurani Itamfahamisha Mungu ni Nani, na Akimuhitaji atampata vipi, na vipi ataweza kumsifu na kumtaja kwa wingi, na kwa majina gani atumie katika kuwasiliana nae. Jee sababu hizi Saba Hazikutoshi wewe kusoma Quran ?.
MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini