Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

ADABU ZA MAISHA YA NDOA

0 Voti 00.0 / 5

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

ADABU ZA MAISHA YA NDOA
Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema katika Surat Ruum aya ya 21:
ومن آياته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها وجعل بينكم مودة ورحمة إن في ذلك لآيات لقوم يتفكرون
"Na katika ishara Zake (za Kuonyesha ihsan juu yenu) ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofikiri." (al-Ruum: 21)

Katika aya hii kuna ishara katika misingi inayosimamisha maisha mazima ya mke na mume ambayo itapelekea katika furaha. Furaha ambayo itakuwa na misingi madhubuti ya mapenzi na huruma, mawaddatan warahmah. Ni juu ya wanandoa wawili kuujenga vizuri uhusiano wao hadi ufikie katika sifa hii ya mapenzi (mawadda) wanapokuwa ni vijana, na kuhurumiana (rahma) wanapokuwa ni watu wazima.

Na katika jumla za adabu ya maisha ya ndoa ni:
1. Tabia Njema
- حسن الخلق
Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
وعاشروهن بالمعروف
" … na kaeni nao kwa wema…" (an-Nisai: 19) katika aya nyingine ya sura hiyo hiyo Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaendelea kututanabaisha
وأخذن منكم ميثاقا غليظا
"…Nao wanawake wamepokea kwenu ahadi thabiti (kuwa mtakaa nao kwa uzuri)." (an-Nisai: 21) Mtume wetu Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) akielezea fadhila za tabia njema anasema:
أكمل المؤمنين إيمانا أحسنهم خلقا, وخياركم خياركم لنسائهم خلقا
"Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia." (Abu Daud na Tirmidhi)

Na Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema tena:
خيركم خيركم لأهله , وأنا خيركم لأهلي
"Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani (ahli)." (Ibn Majah na Darimy)

Na Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
إنّ المرأة خلقت من ضلع وإنّ أعوج شيئ في الضّلع أعلاه , فإن ذهبت تقيمه كسرته , وإن تركته لم يزل أعوج , فاستوصوا بالنساء
Mwanamke Ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni (kuwafanyia wema) wake zenu." (Al-Bukhaariy na Muslim)

Si hayo tu aliyohimiza Mtume wetu Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu wanawake. Bali kwa umuhimu na unyeti wa suala hili tunaona kuwa katika usia wake wa mwisho anatuuusia:
الله الله في النساء فإنّهن عوان في أيديكم , أخذتموهنّ بأمانة الله , واستحللتم فروجهنّ بكلمة الله
"Allah, Allah, kwa wanawake, hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) (Iijaab na Qubuul)." (Muslim, Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad)

Na katika jumla ya tabia nzuri katika maisha ya ndoa ni kuacha kumfanyia mke maudhi ya aina yoyote ile. Vile vile kumfanyia na kumtendea mazuri, na kucheza nae na kuongea nae kwa upole. Hali kadhalika kujali zaidi uadilifu katika mambo yake na kufuata siasa za kati kwa kati katika muamala wako nae na haswa katika yale yenye maslahi kwake na yale yenye kuhifadhi akhlaq zake kulingana na haja, sehemu au tukio.Nyumbani " Zawadi Kwa Wanandoa " ADABU ZA MAISHA YA NDOA
- آداب الحياة الزّوجية
2. Kuishi nae kwa Wema hata Ikiwa Unamchukia
- المعاشرة بالمعروف حتّى في حال الكراهية
Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema:
وعاشروهن بالمعروف فإن كرهتموهن فعسى أن تكرهوا شيئا ويجعل الله فيه خيرا كثيرا
" …na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu Ametia kheri nyingi kwake." (an-Nisai:19)

Katika hilo Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
لا يفرك مؤمن مؤمنة إن كره منها خلقا رضي منها آخر
"Habughudhiki muumini mwanamme kwa tabia ya mke wake akichukizwa na moja ( ya tabia) atapenda nyingine." (Muslim na Ahmad)

Hata hivyo hakuna binaadamu aliyekamilika, anayeweza kusifika kwa ukamilifu wa tabia zote za kuigwa, na vile vile hakuna maisha yenye furaha yaliyokamilika. Hivyo basi ni lazima yawepo mapungufu na matatizo, ambayo yanahitajia suluhisho litakalofikiwa kwa ushirikiano wa pande zote mbili (mume na mke) ili kutatua na kuyashinda. Katika kuamiliana na matatizo yanayojitokeza kunahitaji subira, uvumilivu na utulivu ili maisha yaweze kuendelea na mambo kuweza kurejea kama yalivyokuwa kabla.

Na katika matengamano ya maisha haya ya ndoa ni kuishi na mke kwa wema hata katika hali ya kuwa hata kama unamchukia. Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) anatufundisha:

أن تطعمها إذا طعمت , وتكسوها إذا اكتسيت , ولا تضرب الوجه ولا تقبّح , ولا تهجر إلاّ في البيت
"Kumlisha unapokula, na kumvisha unapovaa, wala usimpige usoni na kumharibu na usimtusi (kwa matendo yake na maneno yake) wala usimhame kwenda nyumba nyingine (umhame kitanda tu)." (Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad)

Na ni juu ya mwanamme yeyote kumtizama na kumuangalia mwanamke kulingana na kauli yake Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) :
ارفق بالقوارير
"Wafanyieni wema vyombo vyenu (qawariira)." (Al-Bukhaariy) Na usia huu unaohusu wema unakusudia upole na mazungumzo mazuri na kuvumilia maudhi. Hali kadhalika kumfanyia uadilifu katika hali zote.
MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini