Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MWENYEEZI MUNGU NI MLINZI

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MWENYEEZI MUNGU NI MLINZI

* Inaposemwa kwamba Mwenyeezi Mungu ni Walii (Mlinzi) ina maana gani?.

* Hivi kweli Ulinzi wa Mwenyeezi Mungu kwa watu wote ni sawa?.

* Hivi kweli kuna uwiano baina ya ulinzi wa Mwenyeezi Mungu na ulinzi wa shetani?.

Uwalii (Ulinzi) wa Mwenyeezi Mungu.

Hapana shaka mwanaadamu anapata saada ya dunia na Akhera pale tu atakapoukubali uwalii na ulinzi wa Mwenyeezi Mungu,  Kwa sababu Mwenyeezi Mungu ni Mwenye nguvu na rehema katika matatizo yoye yanayomfika mwanaadamu, na Yeye ndiye Mwenye kumuongoza na kumsaidia mwanaadamu pindi anapokutwa na matatizo au mitihani yake Allah (s.w). kama inavyosema Qur-ani tukufu:-

وَجَاهِدُوا فِى اللهِ حَقَّ جِهَادِهِ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِى الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ مِّلَّةَ اَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمينَ مِن قَبْلُ وَفِى هَذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيداً عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاء عَلـٰي النَّاسِ فَاَقِيمُوا الصَّلاَةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللهِ هُوَ مَوْلاَكُمْ فَنِعْمَ الْمَوْلَي وَنِعْمَ النَّصِيرُ[1]

Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini.Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu,na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi bora kabisa,na Msaidizi bora kabisa.

Kwa hiyo mtu yoyote yule aliyejiharamishia ulinzi wa Mwenyeezi Mungu, kwa hakika atakuwa hana muongozi au msimamiaji na atakuwa katika matatizo katika dunia, na siku ya Kiama hatapata chochote isipokuwa adhabu kali ya Mwenyeezi Mungu, na hayo ndiyo makadirio yake aliyojikadiria. Kama inavyosema Qur-ani:-

وَلاُضِلَّنَّهُمْ وَلاُمَنِّيَنَّهُمْ وَلآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الاَنْعَامِ وَلآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللهِ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيّاً مِّن دُونِ اللهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَاناً مُّبِيناً[2]

Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.

*Yanatajwa baadhi ya mambo atakayowapotezea, kuwatumainisha kuwa:-

a) Mwenyeezi Mungu Ghafur Rahim.

b) Ukifanya kitu fulani au ukisoma dua fulani utafutiwa dhambi zako zote, isisalie hata moja, hata haki za watu zote zitaruka pia.

c) Mtume hataridhia kumuona hata mtu mmoja katika umma wake yuko motoni.

d) Maadamu mtu ni Mwislamu basi hatagusa Moto wa jahannamu. Na huambia Manasara kuwa maadamu mtu Mnasara basi hatagusa Moto.

Na huwaendea Mayahudi akawaambia vivi hivi. Na Mabaniani, Maparisi, Mabuda na wengineo wenye dini fulani au madhehebu mbali mbali akawadanganya kuwa maadamu wao wanafuata njia ya madhehebu fulani, au dini fulani basi pepo inawangoja tu bila ya msuko suko wowote.

Na haya na kama hayo, ndiyo aliyoyavunja Mwenyeezi Mungu katika Aya ya 123 ya Suratun Nisaa na mahala pengine.

لَّيْسَ بِاَمَانِيِّكُمْ وَلا اَمَانِيِّ اَهْلِ الْكِتَابِ مَن يَعْمَلْ سُوءاً يُجْزَ بِهِ وَلاَ يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللهِ وَلِيّاً وَلاَ نَصِيراً[3]

Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu.

*Wanakatazwa hapa watu kujidanganya roho zao, wakajinasibishia kupata wasiyostahiki ila kwa matamanio tu ya nafsi zao.

“wakaona vinaelea vimeundwa” sio vimepatikana kwa matamanio. Kama anavyosema Allah (s.w).

وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتَ مِن ذَكَرٍ اَوْ اُنثَي وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَاُوْلَـئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلاَ يُظْلَمُونَ نَقِيراً

وَمَنْ اَحْسَنُ دِيناً مِّمَّنْ اَسْلَمَ وَجْهَهُ لله وَهُوَ مُحْسِنٌ واتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفاً وَاتَّخَذَ اللّهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلاً[4]

Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.

Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.

Thamani ya pepo ukiitaka          Dhiki moyo wako kutozunguka.

Thubutisha taa yake Rabbuka     Mola akujazi majaza mema.

Jannatu Naimu fil jinani           jina na Insi waitamani

Jumla ya watu hawaioni           ila kwa ambao watenda mema.

Sharia husema: aso thawabu   shida na mashaka yatamsibu Shufaa ya Tumwal mahbubu    huwa mbali naye   na kumwegema.

Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu ni mmoja, na hakuna anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Yeye Allah (s.w).

Kwa hiyo kwa wale wanaodai kuwa kuna waungu wengine, basi wafahamu kuwa waungu hao hawana milki wala ufalme, na hawajui manufaa au madhara yao. Kama vile anavyosema Allah (s.w).

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ قُلِ اللّهُ قُلْ اَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ اَوْلِيَاء لاَ يَمْلِكُونَ لِاَنفُسِهِمْ نَفْعاً وَلاَ ضَرّاً قُلْ هَلْ يَسْتَوِى الاَعْمَي وَالْبَصِيرُ اَمْ هَلْ تَسْتَوِى الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ اَمْ جَعَلُواْ لِلّهِ شُرَكَاء خَلَقُواْ كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ قُلِ اللّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ[5]

Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu.

Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!.

Na panapotokea hatari hakuna mtu yoyote mwenye uwezo au nguvu ya kuizuilia adhabu hiyo. Na Qur-ani inaashiria uhakika huo kwa kusema:-

لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ اَمْرِ اللهِ إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّي يُغَيِّرُواْ مَا بِاَنْفُسِهِمْ وَإِذَا اَرَادَ اللّهُ بِقَوْمٍ سُوءاً فَلاَ مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَالٍ[6]

Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake.

* Ukiona watu wanaharibikiwa sana na mambo yao, basi ni kwa kuwa wao wenyewe wamebadilisha ule uliokuwa mwendo wao ukawapa hayo waliyokuwa nayo.

 Na lililo zaidi katika hayo ni akhlaqi (mwendo , tabia na sifa zao njema).

Katika somo hili tutafafanua maana ya neno - wilayat – (Walii). Na faida zinazopatikana pindi tutakapokubali uwalii wa Mwenyeezi Mungu.

Mwenyeezi Mungu ni walii kwa waja wake katika njia mbili zifuatazo:-

1) Mwenyeezi Mungu ni walii kijumla jamala kwa waja wake wote.

2)Mwenyeezi Mungu ni Walii kwa waja wake makhsusi na maalumu.

[1] Suratul-hajj Aya ya 78

[2] Surat Nisaa Aya ya 119

[3] Suratun Nisaa Aya ya 123

[4] Suratun Nisaa Aya ya 124-125

[5] Surat Ar-raad Aya ya 16

[6] Surat Ar-raad aya ya 11

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini