Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.6

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.6

* Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?.

katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaendelea na mada yetu ile ile inayohusiana na malengo ya Mitume.

4. KUPIGANIA HAKI ZA WATU DHAIFU NA KUPIGANA NA MADHALIMU

Watu dhaifu ni wale watu ambao kutokana na hukuma za madhalimu, hawawezi kupigania haki zao, na wameharamika katika kuhifadhi tamaduni zao, na kwa sababu hizo basi hawapati kuamua mambo yao, vile ambavyo inawapasa kuayaamua, watu hao ndani ya Qur-ani wamesifiwa hivi :-

إِلاَّ الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ لاَ يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلاَ يَهْتَدُونَ سَبِيلاً[1]

Isipo kuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama.

Na kwa upande mwengine madhalimu ni wale watu ambao, kutokana na nguvu walizonazzo katika serikali au jamii, wao hujiona bora kuliko wengine, na natija ya hayo huwadhalilisha watu dhaifu na kuwaweka chini ya miguu yao, na kuwatendea kila wanayoyataka, kama anavyosema Allah (s.w) kumwambia Firauna:-

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلاَ فِى الاَرْضِ وَجَعَلَ اَهْلَهَا شِيَعاً يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ اَبْنَاءهُمْ وَيَسْتَحْيِى نِسَاءهُمْ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ[2]

Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.

Kwa hiyo kupigania haki za watu madhaifu na kuwaokoa na hukuma za kidhalimu, ni miongoni mwa sehemu ya ujumbe wa Mitume katika kuwalingania wanaadamu. Kama anavyosema Mtume Muhammad (s.a.w.w), ya kwamba nimewaokoa watu na utumwa, na ndani ya Qur-ani tunasoma:-

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الاُمِّيَّ الَّذِى يَجِدُونَهُ مَكْتُوباً عِندَهُمْ فِى التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ يَاْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَآئِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالاَغْلاَلَ الَّتِى كَانَتْ عَلَيْهِمْ فَالَّذِينَ آمَنُواْ بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُواْ النُّورَ الَّذِيَ اُنزِلَ مَعَهُ اُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ[3]

Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa Mitume walitilia umuhimu katika kutimiza wajibu wao, na kuufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu. Na walifanya jitihada zao zote kuwalingania watu katika njia ya Mwenyeezi Mungu. Kama tunavyosoma ndani ya qur-ani:-

وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِى سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ اَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً[4]

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.

Na hii ni ahadi ya Mwenyeezi Mungu kwamba atawasaidia madhaifu waliodhulumiwa na madhalimu, na atawapa madhaifu serekali na hukuma. Kama anavyosema:-

وَنُرِيدُ اَن نَّمُنَّ عَلـٰي الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِى الاَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ اَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ[5]

Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.

[1] Suratun Nisaa Aya ya 98

[2] Surat Qasas Aya ya 4

[3] Surat Al-Aaraf Aya ya 157

[4] Suratun Nisaa Aya ya 75

[5] suratQasas Aya ya 5

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini