Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SIFA TUKUFU ZA MITUME NO.4

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIFA TUKUFU ZA MITUME (A.S) NO 4.

USHAHIDI WA MITUME KWA UMATI WAO

Katika makala iliyopita tulielezea kuhusu sifa tukufu za Mitume (s.a), na tukaelezea miongoni mwa sifa hizo kuwa ni elimu, Maasumu na kuweza kuleta miujiza. katika makala hii tutaendelea na mada hiyo kwa kuelezea kuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu inashuhudia amali na matendo ya umma zao. Mitume inashuhudia amali na matendo ya umati wao.

Miongoni mwa sifa nyengine za Mitume, sifa ambazo zitadhihirika siku ya Kiama, ni kwamba kila Mtume ataona amali za umma wake, na siku ya Kiama atatoa shahada ya amali zao. Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِى كُلِّ اُمَّةٍ شَهِيداً عَلَيْهِم مِّنْ اَنفُسِهِمْ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيداً عَلـٰي هَـؤُلاء وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَاناً لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَي لِلْمُسْلِمِينَ[1]

Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Kwa hiyo ni lazima tufahamu kuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu inashuhudia kila tunalolitenda katika dunia hii, na siku ya Kiama watatoa shahada kwa yale waliyoyaona, na Mwenyeezi Mungu anasisitiza kwa kumwambia Mtume wake Muhammad (s.a.w.w):-

يَا اَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا اَرْسَلْنَاكَ شَاهِداً وَمُبَشِّراً وَنَذِيراً. وَدَاعِياً إِلَي اللهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجاً مُّنِيراً[2]

Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji,Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru.

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala zilizopita.

* Mitume ni lazima wawe na elimu ya kutosha ili kufikisha ujumbe wa Mola wao, na Mwenyeezi Mungu huwapa Mitume yake kila elimu ambayo wanahitajia katika kufikisha ujumbe huo.

* Elimu ya Mitume kwa sababu inatoka kwa Mwenyeezi Mungu basi huitwa Elimu laduniy.

* Ismat au Maasumu yaani ni kujiepusha na kila madhambi, au kumuasi Mwenyeezi Mungu, na hii ni miongoni mwa sifa za Mitume ambazo ni lazima kila Mtume kuwa nayo.

*Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni lazima waje na miujiza katika kuthibitisha madai yao .

* Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni yenye kushuhudia amali za umma wao, na siku ya Kiama watatoa shahada ya kuthibitisha kuona kwa amali za uma wao.

Masuala

1. Mitume ya Mwenyeezi Mungu ili kufikisha ujumbe wa Mola wao wanahitajia kuwa na elimu gani?

2. Mitume ya Mwenyeezi Mungu vipi wamepata elimu hiyo?.

3. Neno Maasumu lina maana gani?.

4. Hivi ni kweli wale ambao wasiokuwa Mitume wanaweza kupata sifa hii tukufu ya kuwa ni maasumu?.

5. Kwa nini Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni lazima ije na miujiza?.

6.Kwa kutumia aya za Qur-ani thibitisha vipi Mitume inashuhudia na kuona amali za umma wao.

7. Neno muujiza lina maana gani?.

[1] Surat Nahli aya ya 89

[2] Surat Al-Ahzaab Aya ya 45-46

 

MWISHO
 
 

 

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini