Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UHAKIKI WA DINI NO.5

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UHAKIKI WA DINI NO.5

UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI.

Katika makala iliyopita, tulielezea umuhimu wa uhakiki wa dini kupitia msingi wa Ijtihadi, katika makala hiyo tulielezea misingi mitatu inayoweza kumuongoza mwanaadamu katika uhakiki wake wa dini, katika makala hii tutaendelea kuelezea misingi mengine ya uhakiki wa dini.

9. Kutambua falsafa ya dini, ikiwa kama ni moja ya misingi ya dini kunaleta athari nyingi nzuri katika taaluma za dini, na dalili bora inayothibitisha kutokuwepo sawa wanaadamu duniani na Akhera ni kutokana na daraja ya elimu waliyonayo, kama anavyosema Allah (s.w):-

[1]"اَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاء اللَّيْلِ سَاجِداً وَقَائِماً يَحْذَرُ الآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِين لاَ يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ اُوْلُوا الاَلْبَابِ"

 Je, afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama na kuogopa Akhera na kutarajia rehema ya Mola wake (ni sawa na asiyefanya hayo)? Sema: “Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.

Taaluma ya dini ndio inayomfanya mwanaadamu awe mtiifu katika maisha yake ya duniani na kumfanyia wepesi baada ya kufa,

" معرفة العلم دين يدان به به يكتسب الانسان الطاعة في حياته و جميل الآحدوثة بعد وفاته  "

Kupitia elimu na maarifa ya dini mwanaadamu anakuwa na dini, na kupitia elimu hiyo mwanaadamu anakuwa mtiifu katika maisha yake, na matokeo mema ni baada ya kufariki kwake.

Na katika hadithi nyengine anasema: Maulamaa wa dini ndio warithi wa Mitume (a.s)

   " العلماء ورثة الأنبیاء  "

Yaani: Maulamaa ndio warithi wa Mitume.

 Basi ni lazima kuitambua falsafa ya dini ili tunufaike na athari nyingi zisizo mpaka ambazo hupatikana kutokana na taaluma za dini.

Hiyo ilikuwa ni misingi ya uhakiki wa dini, tunategemea tutakuwa tumenufaika na maelezo hayo.

[1] Surat Azzumar Aya ya 9.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini