Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

WAFUASI WA KWELI WA MITUME NO.2

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WAFUASI WAKWELI WA MITUME NO.2

* Ni alama gani zinazoonesha ukweli wa wafuasi wa Mitume?.

* Kuna athari gani katika kuwakubali na kuwafuata Mitume?.

Kwa hakika kuwatii Mitume ni kumtii Mwenyeezi Mungu.

1. SIFA ZA WATIIFU.

1-1. Kuwasadiki Mitume yote.

Alama Inayoonesha ukweli na uaminifu wa wafuasi wa Mitume ni kwamba, watu hao wana imani na Mitume yote ya Mwenyeezi Mungu. kama tunavyosoma katika Qur-ani:-

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا اُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ اَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَاَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ[1]

Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake.

Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.

Kwa hakika kumkadhibisha Mtume mmoja ni kuwakadhibisha Mitume yote, kwa sababu Mitume yote ni ya Mwenyeezi Mungu na imekuja kutokana na amri yake Yeye Allah (s.w), imekuja kuwalingania watu katika njia ya Mwenyeeiz Mungu na kuwataka kuwa na imani ya siku ya Kiama. Mitume, wao wenyewe mbali ya kuwahakikishia watu kuwa wao wametumwa na Mwenyeezi Mungu, vile vile waliwabashiria watu kuwa watakuja Mitume wengine baada ya wao, kama tunavyosoma kuhusiana na Nabii Issa (a.s):-

وَإِذْ قَالَ عِيسَي ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِى إِسْرَائِيلَ إِنِّى رَسُولُ اللهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّراً بِرَسُولٍ يَاْتِى مِن بَعْدِى اسْمُهُ اَحْمَدُ فَلَمَّا جَاءهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ[2]

Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!.

1-2. Kuwa na mapenzi na wale wanaowapenda Mitume, na kuwa na bughudhi na wale maadui wa Mitume.

Wafuasi wa kweli wa Mwenyeezi Mungu huwa na mwenendo mzuri na kujenga mapenzi kwa wale wanaowapenda Mitume, na Mwenyeezi Mungu huwapa nguvu ili kukabiliana na maadui au wale wanaowakhalifu Mitume. Kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ اَشِدَّاء عَلـٰي الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعاً سُجَّداً يَبْتَغُونَ فَضْلاً مِّنَ اللهِ وَرِضْوَاناً سِيمَاهُمْ فِى وُجُوهِهِم مِّنْ اَثَرِ السُّجُودِ ذٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِى التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِى الإِنجِيلِ كَزَرْعٍ اَخْرَجَ شَطْاَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَي عَلـٰي سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَاَجْراً عَظِيماً[3]

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.

*Hapa wanatajwa Waislamu wazuri na namna walivyosifiwa katika Taurati na namna walivyosifiwa katika injili, basi natuwe hivi, ili tuwe Waislamu wa kweli, natupate maghufira na huo ujira mwema.

Muhajiri na Maansari ni mfano bora unaoonyesha wafuasi wa kweli wa Mitume, kwani wao walikabiliana na maadui wa Mitume, na wakajenga umoja na mapenzi baina yao wenyewe – yaani wafuasi waaminifu wa Mitume – Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِى سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ اُولَـئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ[4]

Na walio amini wakahama (kuja Madina) na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, (Nao ni Muhajiri) na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, (dini ya Mwenyeezi Mungu na Mtume wake). (Nao ni Ansaari), hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.

 

[1] Suratul-Baqarah Aya ya 285

[2] Surat Saff Aya ya 6

[3] Surat Al-Fat-h Aya ya 29

[4] Surat Al-Anfaal Aya ya 74

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini