Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

BAADHI YA TABIA NJEMA ZA MTUME S.A.W.W

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

BAADHI YA TABIA ZAKE NABII MUHAMMAD (S.A.W.W)

Miongoni mwa tabia njema nyengine za Mtume (s.a.w.w) ni kuwa Yeye alikuwa ni mwenye upendo na huruma, na alifanya jitihada zake zote katika kuwaongoza watu katika njia njema yenye saada, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ اَن تَبْتَغِيَ نَفَقاً فِى الاَرْضِ اَوْ سُلَّماً فِى السَّمَاء فَتَاْتِيَهُم بِآيَةٍ وَلَوْ شَاء اللّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلـٰي الْهُدَي فَلاَ تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ[1]

Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua.

* Nabii Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na hamu kubwa kabisa ya kutaka watu wote wasilimu upesi upesi. Wapewe hiyo miujiza wanayoitaka wishe udhia. Lakini Mwenyeezi Mungu alikuwa hapendi Uislamu huo, akipenda wasilimu baada ya kufahamu vyema hayo wanayoambiwa. Siyo wanasilimu kwa nguvu za miujiza, kama alivyobainisha haya katika aya ya 51 ya Suratul-Ankabuut.

اَوَلَمْ يَكْفِهِمْ اَنَّا اَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَي عَلَيْهِمْ إِنَّ فِى ذٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَي لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ[2]

Je! Kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanacho somewa? Hakika katika hayo zipo rehema na mawaidha kwa watu wanao amini.

* Kuonyesha kuwa hakuna muujiza mkubwa na shahada kamili ya ukweli wa Uislamu kuliko hii Qur-ani isiyoweza kugunduliwa na kosa wala kutiwa kombo kwa lolote. Hayo yalikuwa ni maelezo kwa ufupi kuhusiana na Aya hiyo tukiendelea na mada yetu, hapana shaka kuwa:-

Fadhila na ubora alionao Mtume (s.a.w.w) umemsababishia Yeye kupewa utukufu huo, wa kuwa Yeye ni mwisho wa Mitume yote na ni rehema

kwa viumbe wote ulimwenguni, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَمَا اَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ[3]

Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.

* Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kila mmoja alipelekwa kwa kabila yake na taifa lake tu. mtume Muhammad(s.a.w.w) peke yake ndiye aliyepewa utukufu wa kupelekwa kwa watu wote.

Na kwa upande mwengine Mwenyeezi Mungu, Malaika na Waumini siku zote wanamtukuza kumsalia na kumtukuza Mtume (s.a.w.w). na siku zote Mtume(s.a.w.w) ananufaika na rehema zake Allah (s.w). kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

إِنَّ اللهَ وَمَلاَئِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلـٰي النَّبِيِّ يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيماً[4]

Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini!

Msalieni na mumsalimu kwa salamu.

a) Allahumma Salli Alaa Muhammadin wa Alaa Ali Muhammad, kama Sallayta Alaa Ibrahima wa Alaa Ali Ibrahim. Wabarik Alaa Muhammadin wa Alaa Ali Muhammad, kamaa Barakta Alaa Ibrahima wa Alaa ali Ibrahim. Wasallim alaa Muhammadin wa Alaa Ali Muhammad, kama Sallamta Alaa Ibrahima wa Alaa Ali Ibrahim Fil Alamin. Innaka Hamydun Majiyd. Au

b) Assalatu Wassaalaamu Alan Nabiyyi Warahmatullahi Wabarakaatuhu. Au

c) Allahuma salli Wassallim Wabaarik Alaa ali Muhammadin wa Alaa ali Muhammad, Adada Khalqiqa, Waridhaa Nafsika, wazinata arshika,wamidada Kalimaatik.

 Maelezo kwa ufupi ya somo lililopita.

* Kutokana na kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yeye ndiye aliyekuja na dini kamili ya Mwenyeezi Mungu, basi ni lazima awe M-bora kulinganisha na Mitume yote iliyokuja kabla yake.

* Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye Muislamu wa mwanzo aliyetukuka Kidaraja na kiimani.

*Ubora wa Kitabu cha qur-ani, kulinganisha na vitabu vyengine, - Taurati, Injili, Na Zaburi – ni moja kati ya sifa zinazothibitisha ubora wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

* Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye Mtume aliyefikia cheo cha juu kabisa na kilicho tukufu cha kuwa Yeye yuko karibu zaidi na Allah (s.w).

* Mtume Muhammad (s.a.w.w) anasifika kwa kuwa Yeye alikuwa na ikhlaqi na tabia njema.

Masuali.

1. Kwa kuzingatia na kutumia qur-ani Kariym, vipi tunaweza kuthibitisha kuwa baadhi ya Mitume ni bora kuliko Mitume wengine?.

2. Kwa kuzingatia nadharia ya qur-ani kariym, (Muslim) ni mtu wa aina gani? Au ni mtu gani huitwa Muslim?

3. Vipi tunaweza kuthibitisha na kutoa dalili ya kuwa kitabu cha Qur-ani ni bora kulinganisha na vitabu vyengine, na vipi tunaweza kuthibitisha kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni m-bora wa Mitume yote?.

4. Kwa nini Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni Mtume wa mwisho, na ni dalili inayoonesha ubora wa Mtume huyo?.

5. Elezea kwa ufupi kuhusiana na cheo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa Yeye yuko karibu zaidi na Mola wake.

6. Unaelewa nini kuhusu ikhlaqi, tabia na mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)?.

 

[1] Surat Al-An-aam Aya ya 35

[2] Suratun Ankabuut Aya ya 51

[3] Surat Al-Anbiyaa Aya ya 107

[4] Surat Al-Ahzaab Aya ya 56

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini