Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

FADHILA ZA MTUME (S.A.W.W) KATIKA QUR_ANI

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

2. HUKUMU NA FADHILA ZA QUR_ANI, NI ALAMA BORA INAYOONESHA UBORA WAKE (S.A.W.W).

Vitabu vyote vya Mwenyeezi Mungu alivyoviteremsha kwa Mitume yake ni vyenye nuru na vinavyowaongoza watu katika njia ya uongofu,kama tunavyosoma katika kitabu cha Injili:-

وَقَفَّيْنَا عَلـٰي آثَارِهِم بِعَيسَي ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَآتَيْنَاهُ الإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ[1]

Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu.

*Hapa inatajwa Injili – kitabu alichpteremshiwa Nabii Issa juu ya kuambiwa afuate na Taurati pia, hii Injili ilikuwa na mawaidha zaidi kuliko hukumu, na Taurati ina hukumu nyingi zaidi kuliko mawaidha, ilivyokuwa mwishowe Mayahudi wameharibika sana ndiyo hiyo Injili ikajazwa mawaidha hivyo ili zilainike kidogo nyoyo za Mayahudi lakini wapi.

Na huyu Nabii Issa alipelekwa kwa Mayahudi vile vile kama Nabii Mussa, si kwa Wazungu ila wengi kabisa walikataa kumfuata, akafuatwa na Wazungu kwa kulinganiwa na hao Mayahudi waliomfuata. Hawa Wazungu wamefuata nyuma, baada ya kuondoka ulimwenguni Nabii Issa kwani dini ya Mwenyeezi Mungu haina wenyewe makhsusi.

Kwa hiyo vitabu vyote vya Mwenyeezi Mungu vinatuonesha nuru na uongofu lakini kitabu cha qur-ani ndani yake kimekusanya hukumu zote zilizomo ndani ya vitabu hivyo, yaani kitabu cha Qur-ani ni kiongozi wa vitabu vyote hivyo vya Mwenyeezi Mungu, kama inavyosema Qur-ani:-

وَاَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِناً عَلَيْهِ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ اَهْوَاءهُمْ عَمَّا جَاءكَ مِنَ الْحَقِّ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجاً وَلَوْ شَاء اللّهُ لَجَعَلَكُمْ اُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِى مَا آتَاكُم فَاسْتَبِقُوا الخَيْرَاتِ إِلَي الله مَرْجِعُكُمْ جَمِيعاً فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ[2]

Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.

*Mitme wote wamekuja na hukumu moja katika Itikadi ya Mungu, Mitume, Malaika, Kiama, Tabia njema na kama haya.

Lakini katika mambo ya baadhi ya Hukumu wakikhitilafiana kidogo katika Sharia zao kwa mujibu wa nyakati zao hizo ambao ukikhitilafiana sana umbali wa nyakati wa baadhi ya Mitume na Mitume wengine, na mambo lazima yakhitalifu, na kila anayoyafanya Mwenyeezi Mungu,anayafanya kwa hikima.

Tukitupilia macho zama zilizopita, na tukizingatia Qur-ani kwa makini tunaweza kufahamu na kubagua yale yaliyo sahihi na yaliyoharifiwa,mbali na hayo ndani ya Qur-ani kumeelezewa hukumu za Mwenyeezi Mungu kwa ukamilifu na uwazi kabisa. Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَمَا كَانَ هَـذَا الْقُرْآنُ اَن يُفْتَرَي مِن دُونِ اللهِ وَلَـكِن تَصْدِيقَ الَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لاَ رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ[3]

Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote.

*Wanaonyesha ukweli wa Qur-ani. Haipingani na ya kweli yaliyomo katika vitabu vya Mitume wote wa haki waliotangulia Natija tunayoipata kutokana na maelezo hayo ni kuwa fadhila na ubora wa elimu ya Qur-ani kulinganisha na vitabu vyengine inaonesha ukamilifu na ubora wa elimu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kulinganisha na Mitume iliyopita.

 

[1] Surat Almaidah Aya ya 46

[2] Surat Al-Maidah Aya ya 8

[3] Surat Yunus Aya ya 37

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini