Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO NO.2

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIFA WANAZOTAKIWA MAKHALIFA KUWA NAZO No2

3. kufikiri na kutafakari katika kuiongoza jamii.

katika maelezo yaliyopita tulielezea sifa ya pili wanayotakiwa Mitume kuwa nayo, nayo ni uadilifu, tukiendelea na mada yetu katika kipengele hiki tutaelezea sifa ya tatu, nayo ni kutafakari katika kuiongoza jamii, miongoni mwa nyadhifa anazotakiwa kiongozi wa jamii ya Kiislamu, au  hata isiyo ya kiislamu kuwa nazo ni kuwa yeye anatakiwa azingatie maslahi na manufaa ya watu wa jamii hiyo anayoiongoza, na yeye ndiye anayeweza kutoa amri ya kuwa watu wapigane vita, au wakubali suluhu,na katika hatua ya mwanzo, yeye ndiye mwenye hiyari na anayeweza kuitumia mali ya Baytul mali kutokana na maslahi ya jamii, basi wadhifa huo mkubwa ni lazima apewe mtu anayestahiki kuwa khalifa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kama anavyosema Imamu Ali (a.s):-

ایها الناس ان أحق الناس بهذ الامر أقواهم علیه[1]

Enyi watu; mtu M-bora miongoni mwenu anayestahiki kupewa ukhalifa ni yule ambaye anaweza - kuiongoza jamii katika maadili ya kiislamu- .

Na ni jambo lililowazi kabisa kuwa baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Imamu Ali (a.s) ndiye aliyekuwa M-bora wao, - na elimu ya historia inathibitisha hayo - . kama tunavyosoma katika kitabu chake cha nahjulbalagha :-

و انه لیعلم أن محلی منها محلی القطب من الرحی[2]

Imamu Ali (a.s) anasema Yeye na ukhalifa ni vitu viwili visivyotengana, ni sawa na sehemu ya kinu na mchi wake.

- ni sawa na  position of pestle in the mill - .hii inaonyesha umuhimu wa nasabu yake Imamu Ali katika ukhalifa.

*(Kwa hiyo Imamu Ali (a.s) alikuwa anaelewa kuwa cheo cha ukhalifa kwake Yeye ni jambo la lazima katika jamii ile ya kiislamu).

4. Mwanasiasa bora, ni yule awezae kutambua hila za maadui wake.

Viongozi wa Kiislamu ni lazima wawe wajuzi katika kufahamu hila za maadui zao. kiasi ya kwamba waweze kupambanua baina hila zao na ukweli wao, kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia wafuasi wao kujua mbinu na hila za maadui wao. kama anavyoeleza Allah (s.w) kuhusiana  na ushindi  watakaoshinda Waislamu katika vita, au maadui kushindwa.

Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema :-

وَإِذَا جَاءهُمْ اَمْرٌ مِّنَ الاَمْنِ اَوِ الْخَوْفِ اَذَاعُواْ بِهِ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَي الرَّسُولِ وَإِلَي اُوْلِى الاَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلاَ فَضْلُ اللهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لاَتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلاَّ قَلِيلاً[3]

Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.

* Wanakatazwa hapa watu kutangaza mambo yaliyohusu siasa ya dola. Wasiyaseme ila yale yaliyosemwa na hao wakubwa, kwani wao ndio wanaojua yepi yanafaa na yepi hayafai kusemwa.

baada ya  Mtume Muhammad (s.a.w.w) kufariki, Imamu Ali (as) ndiye aliyekuwa  mjuzi zaidi kuliko wengine ambaye alizielewa mbinu za maadui wa Kiislamu nje na ndani ya nchi.

kimya cha Ali (amani iwe juu yake) cha muda wa miaka 25 baada ya mtume (amani iwe juu yake), ukiongezea na ile miaka 5 ambayo aliitumia  akiwa ni kama khalifa, ni vitu viwili vilivyo weza kuzuia utokeaji wa machafuko.

Imamu Ali (a.s) anasema:-

فأما الناکثون فقد قاتلت * وأما القاسطون فقد جاهدت * وأما المارقة فقد دوخت"[4]“

Katika vita vya jamal nilipigana nao wale waliopinga ujumbe wa Mwenyeezi Mungu, na nilipigana  jihadi katika vita safayn kwa wale waliopigania haki, na katika vita vya Nahriwan nikawachanganya wale walioritadi dini - wale waliotoka nje ya  dini - .

[1] Nahjulbalagha, خ 173, Nahjulbalagha, Feydh, خ 172

[2] Nahjulbalagha خ 3

[3] Surat Nisaa Aya ya 83

[4] Nahjulbalagha, sabhy. خ. 192. Nahjulbalagha Feydhخ.  234

 

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini