Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UIMAMU KWA MTIZAMO WA KISUNNI NA KISHIA

0 Voti 00.0 / 5


UIMAMU KWA MTIZAMO WA KISUNNI NA KISHIA  

Suala la mwanzo lililoleta utata ndani ya jamii changa ya kiislamu baada ya kuondoka Mtume (s.aw.w), ni suala la ukhalifa, kundi fulani ambalo lilitegemea rai za baadhi ya masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), lilimkubali Abuu Bakar, na kundi jengine liliitakidi kua nafasi hii ni ya Ali (a.s) kwa chaguo la Mtume (s.a.w.w), na baada ya

UIMAMU
Suala la mwanzo lililoleta utata ndani ya jamii changa ya kiislamu baada ya kuondoka Mtume (s.aw.w), ni suala la ukhalifa, kundi fulani ambalo lilitegemea rai za baadhi ya masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w), lilimkubali Abuu Bakar, na kundi jengine liliitakidi kua nafasi hii ni ya Ali (a.s) kwa chaguo la Mtume (s.a.w.w), na baada ya kupita zama fulani, kundi la kwanza likajulikana kwa jina la (Sunni), na kundi la pili likajulikana kwa jina la (Shia).
Kitu muhimu cha kukiashiria hapa, ni kua malumbano na tofauti baina ya Shia na Sunni, si katika suala la kua ni nani atakaeshika nafasi ya Mtume (s.a.w.w) baada ya kufa kwake, bali tofauti za makundi haya mawilili zipo katika kulifasiri neno (imamu), pamoja na nafasi ya neno hili, hapo ndipo kila moja kati ya makundi haya mawili linapotafautiana na jenziwe.
Neno uimamu katika lugha lina maana ya kuto kutanguliwa (yaani kuwepo mbele kuliko wote waliobakia), na Imamu ni yule mtu mwenye kuliongoza kundi fulani katika njia na misingi maalum, na neno hili katika dini ya kiislamu, limefasiriwa katika maana tofauti.Kwa mtizamo wa madhehebi ya Kisunni, uimamu ni cheo cha kidunia na wala si cheo maalum cha Mwenye enzi Mungu ambacho humpa mja wake anayestahiki, na kwa kutokana na kwamba kila jamii inahitajia kua na kiongozi, basi jamii ya kiislamu vile vile baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) inatakiwa kujichagulia kiongozi atakayeyasimamia mambo yao, na kwa kutokana na kua hakujawekwa njia maalum ndani ya uislamu katika kumchagua kiongozi, basi kunaweza kukatumika njia tofauti katika suala hili, kama vile kuzisikiliza rai za walio wengi, au kuwasikiliza wakubwa wanasemaje, au kufuata wasia wa makhalifa waliopita, au hata kupitisha mapinduzi kama itawezekana.

Ama Mashia kwa kutokana na kuwa wao wanaona kua uimamu ni kuendelea kwa kazi ya Mtume na ni nguzo ya Mwenye enzi Mungu katika jamii, na ni chanzo cha kufikishia neema za Mwenye enzi Mungu kwa viumbe vyake, kwa msingi huu basi wao wanaamini kua Imamu huainishwa na Mwenye enzi Mungu tu kwa kupitia mtume wake, na imani hii imetokana na fikra za kishia katika kulifahamu neno imamu pamoja na uzito wake, na neno imamu katika Ushia halikueleweka kama vile lilivyoeleweka katika Usunni, bali limeeleweka katika maana pana zaidi, kwani Imamu katika Ushia ni msimamizi wa Waislamu katika mambo yote yale, ya kidini na kidunia.

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini