Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UHUSIANO THABITI WA DUNIANI NA AKHERA

0 Voti 00.0 / 5

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UHUSIANO THABITI WA DUNIANI NA AKHERA.

* Kuna uhusiano gani baina ya ulimwengu wa dunia na ulimwengu wa Kiama?.

*Kuna uhusiano gani baina ya matendo na amali anazozifanya mwanaadamu duniani na malipo atayolipwa siku ya Kiama?

2. Uhusiano thabiti wa mwanaadamu Duniani na Akhera.

Kuna uhusiano madhubuti wa maisha ya duniani na Akhera, na kuna tofauti baina ya kustahamili mashaka ya duniani na kustahamili adhabu za Akhera. Kwa hakika mtu ambaye atamsahau Mola wake ijapokuwa atakuwa katika hali ya juu na nzuri ya maisha, lakini akawa anataka awe na mali zaidi na zaidi, na akawa na hofu ya kupoteza mali yake, kwa hakika mtu huyo hatakuwa na utulivu katika maisha yake. Na kwa sababu mtu huyo amejitia punguani na kusahau Aya za Mola wake, basi atakuwa ni kipofu batini mwake ijapokuwa ni mwenye kuona dhahirini mwake, na siku ya Kiama - ambayo ni siku ya kudhihirika yale yaliyo batini katika nafsi zetu-  atafufuliwa mtu huyo hali akiwa ni kipofu. Na katika hali hiyo basi atazidi kughumiwa, na hofu yake itazidi mara nyingi zaidi, Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَمَنْ اَعْرَضَ عَن ذِكْرِى فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ اَعْمَي[1]

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.

Kwa kila mtu atakayepotoka na kufumba macho ili asione au asikubali haki na uhakika wa mambo, basi siku ya Kiama atafufuliwa mtu huyo hali akiwa ni kipofu,kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani Takatifu:-

وَمَن كَانَ فِى هَـذِهِ اَعْمَي فَهُوَ فِى الآخِرَةِ اَعْمَي وَاَضَلُّ سَبِيلاً[2]

Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi Njia.

3. Uhusiano wa adhabu katika dunia na Akhera.

Ni kipindi kirefu sasa elimu ya Historia inathibitisha kuwa Mwenyeezi Mungu atawaadhibu kwa adhabu kali wale madhalimu waliojiona bora waliokuwa na kibri,na wakadai kuwa wao ni Mungu, basi Mwenyeezi Mungu amewaahidi watu hao adhabu kali duniani na Akhera. Kama anavyosema Allah (s.w) kumwambia Firauna:-

فَاَخَذَهُ اللهُ نَكَالَ الآخِرَةِ وَالاُولَي[3]

Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.

Na vile vile kwa wale ambao wamekabiliana na kuyapinga mafunzo ya Mitume kwa ulajuji na wakawakadhibisha Mitume hao, basi Mwenyeezi Mungu atawaadhibu na kuwadhalilisha kwa kuwaletea balaa katika maisha yao, na siku ya Kiama amewaandalia adhabu kali iumizayo, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

فَاَذَاقَهُمُ اللهُ الْخِزْيَ فِى الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَعَذَابُ الآخِرَةِ اَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ[4]

Basi Mwenyeezi Mungu akawaonjesha hizaya (fedheha) katika maisha ya dunia, na adahabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laity wangelijua!.

 

[1] Surat Taha, Aya ya 124.

[2] Surat bani Israiyl Aya ya 72.

[3] Suratu- Annaziaati aya ya 25.

[4] Surat Az-Zumar Aya ya 26.

 

MWISHO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini