Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 2

0 Voti 00.0 / 5

MUHAMMAD MTUME WA ALLAH 2

KUZALIWA MPAKA KUANZA KWA WAHYI

MUENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA

KUHAMA KWENDA MAKKAH
Katika takriban mwaka wa kumi wa Utume wake, wakati Mtume alipoondoka kwenye “bonde la Shi’ab Abu Talib”, ami yake, Abu Talib, ambaye pia alikuwa ndiye mlinzi wake pekee, alifariki dunia, kama alivyofariki pia mke wake mpendwa Khadijah. Kuanzia hapo ikawa hakuna tena ulinzi wa maisha yake wala mahali pa kukimbilia.
Hatimaye wale waabudu masanamu wa Makkah walibuni mpango wa siri wa kumuua Mtume. Wakati wa usiku wao waliizunguka nyumba yake kwa nia ya kuivamia nyumba yake mwishoni mwa usiku na kumkata kata vipande vipande wakati akiwa kitandani. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjulisha kuhusu mpango huo na kamuamuru kuondoka na kwenda Madina, wakati huo ikiitwa Yathrib. Mtume alimwambia ‘Ali alale kitandani mwake ili kwamba maadui wasigundue kutokuwepo kwake; bila kusita ‘Ali alikubali kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya Mtume na akalala katika kitanda cha Mtume. Kisha Mtume akaondoka hapo nyumbani chini ya ulinzi Mtukufu wa kimbinguni, akiwapita maadui zake katikati yao, na akichukua hifadhi ndani ya pango karibu na Makkah. Baada ya siku tatu, maadui zake, baada ya kutafuta kila mahali, walikata tama ya kumkamata yeye na wakarudi Makkah. Mtume naye akaondoka kuelekea Yathrib.
KUANZISHA JAMII YA KIISLAMU
Watu wa Yathrib, ambao uongozi wao walikuwa tayari wamekwisha ukubali ujumbe wake Mtukufu Mtume na kula kiapo cha utii kwake, walimkaribisha kwa ukarimu kabisa na wakayaweka maisha na mali zao chini ya mamlaka yake. Huko Yathrib, kwa mara ya kwanza, Mtume aliunda Jumuiya ndogo ya Kiislam na akawekeana saini mikataba na makabila ya Kiyahudi, ndani na kandoni mwa mji huo, vile vile na yale makabila ya kiarabu yenye nguvu katika eneo hilo. Alijiandaa kuyafanya kazi ya kuutangaza ujumbe wa Uislam na Madina ikawa maarufu kama “Madinatu ‘r-Rasul” (Mji wa Mtume). Baadae kabisa ulikuja kujulikana kama “Madina”.
Uislam ulianza kukua na kupanuka kuanzia siku hadi siku. Wale Waislamu, ambao huko Makkah walikuwa wamenasa kwenye nyavu za uonevu na dhulma za Makuraishi, pole pole waliyaacha majumba na mali zao na wakahama kwenda Madina, wakimzunguka Mtume kama wadudu nondo waliozunguka mshumaa. Kundi hilo lilijulikana kama “wahamiaji” (Muhajiriin) kwa namna ile ambayo wale waliomsaidia Mtume huko Yathrib walivyojipatia jina la “Wasaidizi” (Ansar).
Mtume aliinda jamii hiyo katika misingi ya haki na usawa miongoni mwa waumini. Undugu – sio tu kwa maneno bali pia kwa vitendo – ulianzishwa miongoni mwa Muhajir na Ansar. Mfumo mwake ili kwamba maadui wasigundue kutokuwepo kwake; bila kusita ‘Ali alikubali kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya Mtume na akalala katika kitanda cha Mtume. Kisha Mtume akaondoka hapo nyumbani chini ya ulinzi Mtukufu wa kimbinguni, akiwapita maadui zake katikati yao, na akichukua hifadhi ndani ya pango karibu na Makkah. Baada ya siku tatu, maadui zake, baada ya kutafuta kila mahali, walikata tama ya kumkamata yeye na wakarudi Makkah. Mtume naye akaondoka kuelekea Yathrib.
MAPAMBANO KATIKA MEDANI ZA VITA
Uislam ulikuwa unaendelea haraka sana lakini wakati huo huo wale waabudu masanamu wa Makkah, na vile vile makabila ya Kiyahudi ya Uarabuni, yalikuwa hayazuiliki katika kuwabughudhi kwao Waislamu. Kwa msaada wa wanafiki wa Madina, ambao walikuwa miongoni mwa jamii ya Waislam, walisababisha mabalaa mapya kwa ajili ya Waislam kila uchao hadi mwishowe jambo hilo likaongezea kwenye vita.
Vita vingi vilitokea kati ya Waislam, washirikina wa Kiarabu na Wayahudi. Waislam waliibuka washindi katika mengi ya mapambano hayo. Katika mapigano yote makubwa kama vile vita vya Badr, Uhud, Khandaq, Khaybar, Hunayn na kadhalika, Mtume alikuwepo mwenyewe katika uwanja wa mapambano. Vile vile katika vita vyote vikubwa na vidogo vingi, ushindi ulipatikana zaidi kwa kupitia juhudi za Ali bin Abi Talib. Alikuwa ndiye mtu pekee ambaye kamwe hakugeuka kwenye vita vyovyote kati ya hivi. Katika vita vyote vilivyotokea katika miaka kumi yote baada ya kuhama kutoka Makkah kwenda Madina, chini ya Waislamu miambili, na makafiri chini ya elfu moja waliuawa.
VITA VYA BADR
Watu wa Makkah waliendeleza majaribio yao ya kuuvunja Uislamu. Waliendelea kuwabughudhi Waislam waliokuwa wamebakia hapo Makkah na pia walikamata mali na vitu vyao. Abu Jahl, kiongozi wa watu wa Makkah, alituma hata barua kwa Mtume akimtishia na shambulio kutoka kwa watu wa Makkah. Ilikuwa ni katika kujibu uchochezi huu ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Mtume ruhusa ya kuwapiga makafiri wa Makkah. Yeye alisema:
“Imeruhusiwa kupigana kwa wale wanaopigwa kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia. Ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki………” (22:)
Katika mwaka wa pili wa (Hijiria), Mtume akiwa na takriban Waislamu 300 wasioandaliwa vizuri, walikabiliana na jeshi lililoandaliwa vema kutoka Makkah lenye takriban wapiganaji1,000. Ingawa walizidiwa kwa idadi, Waislam waliweza kuwashinda makafiri katika pambano la kwanza la silaha dhidi ya maadui.
VITA VYA UHUD
Ili kulipiza kisasi cha kushindwa kwao huko Badr, watu wa Makkah waliandaa kikosi kingine cha jeshi katika mwaka wa tatu wa hijiria na wakatoka kuelekea Madina. Baada ya kuvifikia vilima vya Uhud, maili nne nje ya madina, Mtume alichukua nafasi yake chini ya mlima. Jeshi likajipanga katika mifumo ya mapigano. Watupa mishale 50 waliwekwa chini ya kamandi ya Abdullah bin Jubair kwenye kijinjia katikati ya vilima hivyo ili kuwalinda Waislamu na mashambulizi yoyote kutoka upande wa nyuma. Walikuwa na maagizo makali ya kutokuondoka kwenye sehemu zao, kwa matokeo yoyote ya vita yatakayokuwa.
Waislamu mwanzoni waliwashinda watu wa Makkah. Maadui hao, baada ya kushindwa na kupata hasara kubwa, walirudi nyuma kwa mparaganyiko na Waislam wakaanza kukusanya ngawira.
Wakidhania kwamba mapigano yamekwisha; wengi wa wale watupa mishale 50 wanaochunga vile vilima waliondoka kwenye sehemu zao kinyume na amri ya kiongozi wao. Khalid bin Walid, kamanda mmoja wa kikosi cha farasi cha jeshi la Makkah aliikamata fursa hii na akakiongoza kikosi chake kupitia kwenye kinjia hicho cha mlimani na baada ya kuwauwa wale watupa mishale wachache waliokuwa wamebakia, alianzisha shambulizi kali juu ya Waislam kutoka upande ule wa nyuma.
Kwa sababu ya kuasi na kutotii amri kwa kikundi kidogo, ule ushindi wa Waislamu ukachukuliwa kutoka mikononi mwao Waislam. Wengi wao wakakimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano. Wachache tu, hususan Ali, walisimama imara na kupigana mpaka mwisho. Hatimae Waislamu wakakimbilia kwenye usalama wa vilele vya mlima wa Uhud. Miongoni mwa wale Waislam 70 ambao walikufa katika shambulizi hili la majibu la watu wa Makkah alikuwa ni Hamza bin Abdul Muttalib, yule ami yake jasiri Mtume. Yeye kwa hakika alikuwa ni simba wa Mungu (Assadullah).
VITA VYA KHANDAQ (AHZAB)
Katika mwaka wa tano hijiria, kabila moja la kiyahudi liliunda ushirikiano na watu wa Makkah; na kwa pamoja wakaandaa jeshi la takriban wapiganaji 10,000. Vita hivi vinajulikana kama vita vya Ahzab (ushirikiano) na vile vile Khandaq (Mtaro, handaki) kwa sababu Waislamu walichimba mitaro kuzunguka kambi yao ili kumzuia adui kuingia mjini.
Yale majeshi ya muungano ya wasiokuwa Waislamu yaliizingira Madina kwa mwezi mmoja. Isipokuwa kwa wapiganaji mashuhuri wachache tu, walikuwa hawana uwezo wa kuvuka ule mtaro. Majeshi hayo ya muungano mwishowe yalirudi nyuma baada ya Ali, katika pambano la mtu mmoja mmoja, alipomuua yule jasiri kabisa wa hao wapiganaji wao.

ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini