Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 1

0 Voti 00.0 / 5

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 1

AYA YA UDHU NI AYA MUHKAMAH

Waislamu wameafikiana kwa mujibu wa na Kitabu kitukufu kuwa Swala haiwi sahihi isipokuwa kwa tohara, nayo ni: Wudhu, Josho, na Tayammum, na Allah (s.w.t.) amebainisha siri ya taklifu ni kwakuipata tohara kabla ya Swala kwa kauli yake:

(Mwenyezi Mungu hataki kuwafanyiyeni ugumu, lakini anataka kuwatoharisheni).
Udhu katika sheria ya kiislamu umepata umuhimu mkubwa kama ambavyo Qur’an na Sunna vimetamka. Amesema Mtume (s.a.w.w.): (Hapana Swala ila kwa tohara), na katika maneno yake mengine: (Wudhu ni sehemu ya imani) (Al’wasaailu, Juz.1, mlango wa kwanza miongoni mwa milango ya Wudhu).

Ikiwa hii ndio nafasi ya Wudhu basi ni wajibu kwa Muislamu kuzitambua sehemu zake, na sharti zake, na vitanguzi vyake na vibatilisho vyake. Vitabu vya Fiq’h vimebainisha umuhimu huu. Ambalo twalitilia mkazo hapa ni kubainisha lile ambalo neno la wanavyuoni limehitilafiana kwalo. Naikusudia hukumu ya miguu upande wa kuosha au kupaka, hivi basi twasema:

Mungu Mtukufu amesema ndani ya Kitabu chake kitukufu akibainisha wajibu wa wudhu na jinsi yake kwa kauli yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ مِنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ حَرَجٍ وَلَٰكِنْ يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ {6}

“Enyi! ambao mmeamini mnapokusudia kusali osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye viwiko, na pakeni sehemu za vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu mbili, na endapo mkiwa na janaba jitoharisheni na muwapo wagonjwa au safarini au yeyote kati yenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake na hamkupata maji, hivyo fanyeni Tayamamu kwa mchanga safi. Pakeni sehemu za nyuso zenu na mikono yenu kwa huo (mchanga). Mungu hataki kukutieni shida, lakini tu yuataka kukutoharisheni na kukutimizieni neema yake kwenu ili mpate kushukuru. (Al-Maidah; 5: 6).

Aya hii ni mojawapo ya Aya za hukumu ambazo humo huchukuliwa hukumu za kisharia kiutekeleza inayorejea kwenye kunadhimu matendo ya wanaopasa kutenda katika ambayo yanaambatana na shughuli za maisha yao ya kidini na ya kidunia.

Na kipande hiki cha Aya kina ufafanuzi ulio wazi, na dalili iliyo safi, kwa kuwa anayeambiwa hapa ni umma wa waumini ambao wapenda kutekeleza kama ilivyo mwenendo wake wa kimatendo kulingana nazo (Aya). Kwa ajili hiyo zinatofautiana na Aya zinazoambatana na tawhid ya kina na maarifa ya kiakili, ambayo hufungiwa humo maoni ya wanafikra waliobobea, khususan katika ambayo yanaambatana na masuala ya chanzo na ufufuo.

Na mtu endapo atazizingatia Aya hizi na zilizo mfano wake, miongoni mwa Aya ambazo zinachukuwa dhamana ya kubainisha wadhifa wa muislamu, mfano wa kutekeleza Swala katika nyakati tano, atakuta maelezo yake ni thabiti, ubainifu wake uko safi, dalili yake ni ya wazi inayowasemesha waumini wote ili kuwachorea majukumu yao wakusudiapo kusali.

Na kauli ya tamko - kama ulivyokwishajua - kuwa yabidi liwe mbali na utata na ugumu, mbali na kutanguliza (neno au kuchelewesha, mbali na kukadiria jumla moja au neno, ili madhumuni yake wayaelewe Waislamu wote hali wakiwa wanatofautiana viwango vyao bila tofauti kati ya mjuzi wa kanuni za Lugha ya kiarabu na asiye mjuzi.

Hivyo basi mwenye kujaribu kuitafsiri Aya hii kwa utaratibu usiokuwa huu atakuwa ameghafilika mahali pa Aya na nafasi yake, kama ambavyo mwenye kujaribu kuitafsiri kupitia mwanga wa fatwa za kifiq’hi za maimamu wa fiq’hi atakuwa ameingia mlango usio wake.

Ruhul’amiinu Jibril aliiteremsha Aya hii kwenye moyo wa Bwana wa mitume, naye aliwasomea Waislamu na waliufahamu wajibu wao kuielekea Aya kwa uwazi kabisa, bila ya kutaradadi, bila ya kuingiwa na hali isiyoeleweka wala ugumu katika hiyo Aya. Isipokuwa utata ulijipenyeza kwenye Aya zama za mgongano wa rai na kujitokeza kwa ijtihadi (nyingi).
Hivyo mwenye kuisoma Aya hii iliyobarikiwa kwa mazingatio atasema moyoni mwake na ulimini mwake: Sub’haanaka maneno yako yana balagha ilioje na ubainifu wako una fasaha ilioje, umeweka wazi faradhi na kuubainisha jukumu la yale yaliyo wajibu kwa Muislamu kuyatenda kabla ya Swala, uliposema: (Yaa ayyuha lladhiyna Aamanuu idhaa qumtum ila swalaati). Kisha ukasema ukibainisha jinsi ya wadhifa ulivyo, kuwa ni mambo mawili:

( fagh’siluu wujuhakum wa aydiyakum ilal’marafiqi)
(wa msahu biruusikum wa arjulakum ilal’ka’abayni)

Umetakasika haukubakisha maelezo ya jumla jumla ndani ya maneno yako, wala utata katika kubainisha kwako, kwa hiyo umeufunga mlango wa tofauti na umeziba mlango wa kutojali kwa kufafanua faradhi na kuibainisha.

Umetakasika Ewe Allah ikiwa Kitabu chako kitukufu ndio msimamizi wa vitabu vya mbinguni kama ulivyosema:

وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ {48}

Na tumekuteremisha Kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Kitabu na kuyalinda.(Al-Maidah:48).

Hivyo basi Kitabu hiki ni msimamizi - kwa ithibati na yakini - wa riwaya zilizokuja katika athari kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) nazo ziko kati ya zinazoamrisha kuosha miguu na zinazoamrisha kuipaka.

Tufanye nini sasa na hizi riwaya zilizokuja katika athari zinazopingana zilizoelezwa kutoka kwa ambaye la yantwiqu ila anil’wahyi, hatamki ila kutokana na wah’yi wala hajipingi binafsi katika usemi wake? umetakasika hatuna upenyo isipokuwa kuyachukua yaliyonadiwa na Kitabu chako kitukufu na Qur’an Yako yenye enzi, na kwa hakika umebainisha katika jumla mbili zinazoweka wazi ukweli wa wajibu kuwa yafanyika kwa (viungo) viwili vya kuosha (Fagh’siluu wujuhakum wa aydiyakum ilal’marafiqi). (na osheni nyuso zenu na dhiraa zenu mpaka kwenye viwikozviwili). Kama unavyofanyika kwa (viungo) viwili vya kupaka:

وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ {6}

Na pakeni sehemu za vichwa vyenu na miguu yenu mpaka kwenye nguyu (kiungo cha mguu na kanyagio) mbili. (Al-Maidah: 5: 6)

أَفَغَيْرَ اللَّهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنْزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ {114}

“Je nimtake hakimu ambaye sio Mungu hali yeye ndiye ambaye amekuteremshieni kitabu - kifafanuzi.” (Al’An’aam:114)

Umetakasika Mola wangu hujabakisha fumbo katika maneno yako wala utata katika kubainisha kwako, kwa hiyo umeufunga mlango wa mfarakano, na kuufunga mlango wa ujahili kwa kuuweka wajibu wazi na kuubainisha.

Umetakasika ewe Mola wangu, ikiwa Kitabu Chako kitukufu ndio kinachosimamia vitabu vya mbinguni kama ulivyosema:

وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ {48}

“Na tumekuteremshia kitabu kwa ukweli chenye kusadikisha yaliyokuwa kabla yake katika kitabu, na mchunga wa hivyo vitabu.” (Al-Maidah; 5: 48)

Kwa hiyo ( hiki kitabu) ni mchunga – kwa (dalili) ya mkato na yakini - wa yaliyopatikana kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) nayo yapo kati ya yaamrishayo kuosha miguu na yaamrishayo kuipaka.

Sasa tutafanyaje na hizi habari zinazopingana zilizoelezwa kutoka kwa asiyetamka isipokuwa ni wahyi na wala hajitangui mwenyewe maneno yake?

Umetakasika hatuna kimbilio ila kuchukua ambalo Kitabu Chako kitukufu kimelinadi na kimebainisha katika jumla mbili zinazoweka wazi ukweli wa wajibu, kuwa unatimia kwa sehemu mbili za kuosha

(fagh’siluu wujuhakum, wa aydiyakum ilal’marafiqi)

Kama unavyotimia kwa sehemu mbili za kupaka:

(famsahu biru’usikum wa arjulakum ilal’ka’abayni)

أَفَغَيْرَ اللَّهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنْزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ {6}

(afaghayra’llahi abtaghi hakaman wahuwa lladhiy anzala ilaykumul’kitaba mufaswalan) (Al’an am: 6)
MWANZO WA TOFAUTI

Waislamu walikuwa wanaafikiana katika suala la Wudhu kabla ya enzi ya Khalifa wa tatu, wakati huo hapakuwa na tofauti yoyote iliyojitokeza kuhusu kupaka miguu miwili au kuiosha; bali tofauti ilianza wakati wa enzi ya khalifa wa tatu, kama inavyoonyesha katika riwaya nyingi za ubainifu zilizoelezwa na Seyydna Uthman. Na Muslim ametaja kundi miongoni mwazo ndani ya Sahihi yake.

1. Muslim ameitoa (kuieleza) kutoka kwa Humran, huria wa Uthmani amesema: “Nilimletea Uthman bin Affani maji, alitawadha, hati maye akasema:

“Kwa kweli watu wanaongea kuhusu Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) Hadith sijui ni zipi hizo? Tambua! Kwa hakika mimi nimemuona Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) akitawadha mfano wa wudhu wangu huu; kisha akasema: Mwenye kutawadha kama hivi, atasamehewa dhambi zake zilizotangulia, na itakuwa Swala yake na kwenda kwake msikitini ni naafilah - Sunna.”1

2. Ametoa Muslim kwa Abiy Anasi kuwa Uthman alitawadha kwa mgao na akasema: “Je nisiwaonyesheni wudhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.).” Hatimaye alitawadha mara tatu tatu. Na Bw. Qutaybah amezidisha katika riwaya yake. Amesema Sufyani: Abu Nadhri amesema kutoka kwa Abiy Anasi amesema: Akiwa na watu miongoni mwa swahaba wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.).2

Na kuna Riwaya nyingine za kubainisha kwa ulimi wa Uthmani. Muslim hakuzieleza, lakini zimetajwa na wengine, zote zinaonyesha kujitokeza kwa tofauti kuhusu jinsi ya wudhu wa Mtume, kwamba kulikuwa katika zama zake (Othman), ama kuhusu nini sababu ya tofauti, ubainifu wake unakujia..

ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO..

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini