Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 2

0 Voti 00.0 / 5

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 2

MWENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA
QUR’AN TUKUFU NDIO MSIMAMIZI NA REJEA PEKEE, PINDI ATHARI ZIKITOFAUTIANA.
Qur’an tukufu ni msimamizi wa vitabu vya mbinguni. Nayo ni mizani ya (kuutambua ) ukweli na batili. Hivyo basi habari zitakazokuja humo (kati- ka vitabu vya mbinguni) huchukuliwa endapo hazitokhalifu Kitabu kituku- fu, vinginevyo zitapigwa ukutani.
Ikiwa huu ndio msimamo wa Qur’an Tukufu kuvihusu vitabu vya mbin- guni, ni bora zaidi iwe hivyo kuzihusu Sunna zilizotokana na Mtume (s.a.w.w.). Qur’an ni msimamizi wake, kwa hiyo Sunna hufanyiwa kazi - endapo sanadi itakuwa sahihi - ilimradi tu haipingani na Kitabu - Qur’an.
Wala hilo halimaanishi kutosheka na Qur’an na kuifutilia mbali Sunna kwa kuiweka kando na sharia, hiyo ni itikadi ya wazandiki. Sunna ni hoja ya Waislamu, ya pili-baada ya Kitabu kitukufu - kwa sharti Sunna ielezayo isipingane na sanadi ya uhakika kwa Waislamu.
Ikiwa Qur’an Tukufu imesema chochote kuhusu kupaka au kuosha, Sunna au habari inayoamrisha kinyume chake ina thamani gani! Na’am; Endapo yawezekana (Aljam’u) kuziowanisha kati ya Qur’an Tukufu na zile habari kwa kuichukua ya pili kuwa ilikuwa kwa muda tu wa wakati, kisha Qur’an ilifutilia mbali hivyo itakuwa ndivyo, kama sivyo naipigwe ukutani.
Bw. Ar-Raziy amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema:
Endapo mmeelezwa Hadith basi ipimeni na Kitabu cha Mungu, ikiafikiana nacho ikubalini, ama si hivyo ikataeni.3
AL-MAIDAH NI SURA ILIYOSHUKA MWISHO
Kwa hakika Sura ya Al-Maidah ni Sura iliyoshuka mwisho kwa Mtume (s.a.w.w.), ndani yake hakuna Aya ambayo (imeondolewa hukumu yake). Ametoa (habari) Ahmadi, na Abu Ubaydi ndani ya kitabu chake:
Al-fad- hwailu na an-Nuhasu na ndani ya kitabu chake: An-Naasikhu, na an-Nasaaiy na Ibnul’Mundhir, na Al-Haakimu na Ibnu Mardawayhi, na al’Bayhaqiy ndani ya SunNanu yake kutoka kwa Jubayru ibni Nafiiru. Amesema: “Nilihiji nikaingia kwa (mama) Aisha akaniambia: Ewe Jubayru wasoma (sura ya) Al-Maaidah, nikasema: Naam, Akasema: Kwa hakika hiyo ni Sura iliyo shuka mwisho, hivyo basi mukutacho humo miongoni mwa halali kihesabuni kuwa ni halali, na mukikutacho humo miongoni mwa haramu basi kihesabuni kuwa ni haramu.”
Na ametoa (habari) Abu Ubaydi, kutoka kwa Dhwamra bin Habiibu, na Aatiyatu bin Qaysi, wawili hao wamesema: “Amesema Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) kuwa: “Al-Maaidah ni ya mwisho kuteremka katika Qur’an, hivyo basi halal- isheni halali yake na haramisheni haramu yake.”
Na ametoa (habari) Al-Fariabiy na Abu Ubaydi, na Abdu bin Hamiidi, na Ibin Al Mundhiri, na Abu Sheikh kutoka kwa Abu Maysarah, Amesema:
(fil maidati thamaniy ashrata fariidhwata laysa fii Suratin minal’Qur’an ghairaha walaysa fiiha mansukhu, wa adda minha (wa idha qum tum ilaswalati fagh’siluu)
“Ndani ya Suratul-Maaidatu kuna faradhi kumi na nane hazipo katika Sura nyingine yeyote katika Sura za Qur’an isio hii, wala katika hizo hakuna mansukhu (iliyoondolewa) na alizihesabu miongoni mwazo,
(wa idha qumtum ila swalati fagh’siluu).
Na Abu Daudi na An-Nuhaasi wametoa (habari) hao wote wawili katika An-Nasikhu kutoka kwa Abiy Mysarah Amru bin Sharhiil alisema: “Ndani ya Surati Al-Maidah hapajanasikhiwa (kuondolewa) kitu.”
Na ametoa (habari) Abdu bin Hamidu alisema: “Nilimuuliza Hasan, Je katika Sura ya Al-Maaidah kuna kilichofutwa? Akasema: La, hapana.”4
Hayo yote yanajulisha kuwa Surati Al-Maidah ni Sura iliyoteremka kwa Mtume mwisho, hivyo basi hakuna upenyo wa kuacha kutenda kwa mujibu wake wala haina naskhi – kilichoondolewa.
Riwaya kutoka kwa maimamu wa Ahlul-Bayt zimesaidiana (kuthibitisha) kuwa Sura ya Al-Maidah ni Sura iliyoteremka mwisho wala ndani yake hakuna Aya mansukhah - iliyoondolewa hukumu yake.
Muhammad bin Mas’udi Al’Ayaashiy As-Samarqandiy ametoa (habari kutoka kwa Ali (a.s.):
“Qur’an ilikuwa baadhi yake inafuta baadhi nyingine. Huchukuliwa kutoka amri za Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) ile ya mwisho wake tu. Na ya mwisho iliyoteremka kwake ni Suratu Al-Maidah ilifuta zilizoshuka kabla yake wala yenyewe haikutenguliwa na kitu.”5
Ametoa Shaikh Tusiy sanadi yake kwa Aswadiqu na Al-Baaqiru (a.s.), kutoka kwa Amirul-Muuminin Ali (a.s.) aliposema katika hadith ndefu:
Kwa mwanga huo lau kitabu kingejulisha chochote kuhusu kupaka na kuosha, fathari zinazotofautiana nacho, aidha zingefanyiwa ta’awili kuwa zimefutwa na Qur’an au hutupiliwa mbali.
CHIMBUKO LA TOFAUTI
Ikiwa mwanzo wa tofauti ni wakati wa enzi ya khalifa wa tatu, kuna swali lajitokeza lenyewe: Nini sababu ya tofauti katika suala la Wudhu, baada ya kupita taqriban miaka 20 toka kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.). Hivyo basi twasema: Kuna sababu na uwezekano kadhaa:
1. TOFAUTI ZA QIRA’AH
Huenda ikafanywa taswira kuwa chimbuko la tofauti katika zama zile ni tofauti ya usomaji kwa kuwa wasomaji wametofautiana katika irabu ya katika kauli yake (s.w.t.): Kuna ambao wameisoma kwa jarri wakiizingatia kuwa ni “Miguu imeunganishwa na kichwa katika hukumu ya kupaka kwa mujibu wa kiunganishi.”
Na miongoni mwao kuna ambao wameisoma kwa fat’ha wakiizingatia katika kauli yake (s.w.t.) ambayo yalazimu ioshwe.
Kwa kweli mtizamo huu ni batili kabisa, kwa kuwa Mwarabu halisi aisomapo Aya akiwa mbali na rai nyingine yeyote hatoridhika (aisome Aya) bila ya kuiunganisha miguu na kichwa, sawa aisome kwa nasbi yaani fat’ha au jarri yaani kisra. Ama kuiunga na neno: wujuuhakum hilo halimjii mawazoni mwake hata iwe ndio chimbuko la tofauti.
Kwa hiyo mwenye kuitaka tafsiri ya Aya na kufahamu yajulishwayo na Aya hii ajifanye yeye mwenyewe kana kwamba yu katika zama zile za kushuka Aya na yuasikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu kutoka kinywa cha Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) au swahaba wake, kwa vile atakalolifa- hamu hapo ni hoja kati yake na Mola wake, hapo hatokuwa na haja ya kutegemea yawezekana hivi au vile! Na mitazamo tofauti ambayo haikuwa wakati ule na ilijitokeza baada ya wakati ule.
Lau tuilete Aya mbele ya Mwarabu aliye mbali na mazingira ya kifiq’hi na tofauti za Waislamu katika jinsi ya kuchukua wudhu, na tumuombe abain- ishe alilofahamu, angesema kwa wazi kabisa: Kwa kweli wudhu ni sehemu mbili za kuosha na mbili za kupaka bila ya kufikiria kuwa je miguu inaungwa na hukumu ya kichwa au inaungwa na hukumu ya nyuso?
Kwani yeye anadiriki kuwa hii (jumla) ndani yake mna jumla mbili zilizoeleza wazi hukumu mbili:
Kuanza na jumla ya kwanza:
(Osheni nyuso zenu na mikono yenu pamoja na maraafiqi (viwiko) ( mir- faq ni: kiwiko cha mkono, wingi wake ni maraafiq) kwa kuosha nyuso kisha imeunganishwa mikono hukumu moja na nyuso, hivyo, mikono ikawajibika kuwa na hukumu ile ya nyuso kwa sababu ya at’fu (kiungo) cha herufi wau ? .
Hatimaye ilianza jumla ya pili:
(Na pakeni baadhi ya vichwa vyenu na baadhi ya miguu yenu mpaka kwenye ka’ab mbili) kwa amri ya kupaka vichwa kisha akaiunga pamoja miguu (kwa amri hiyo hiyo hivyo basi ikawajibika kuwa na hukumu ile ya vichwa, kwa sababu ya at’fu yaani kiungo wau?, na wau yajulisha ushirikiano wa kile kinachokuja baada yake na kile cha kabla yake katika hukumu. Na kufarikisha kati ya hukumu ya vichwa na hukumu ya miguu hakutumainii Mwarabu halisi bali yuaona ni kinyume na dhahiri ya Aya.
2. KUSHIKILIA RIWAYA YA KUOSHA ILIYONASIKHIWA
Yaonyesha kutokana na si moja miongoni mwa riwaya kuwa kuosha miguu miwili ilikuwa ni sunna, Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha muda fulani katika umri wake, na ilipoteremka Suratul’Maaidah ndanimwe mukiwa na Aya ya wudhu na amri ya kuipaka miguu miwili mahali pa kuiosha, kwa muda fulani - asiyejuwa naasikhu na mansuukhu aliichukuwa Sunna iliyonasikhiwa na kutimua (vumbi la) mfarakano akiwa ameghafilika kuwa wajibu wake ni kuifuata Qur’an iliyonasikhi Sunna. Ndani ya hiyo (Qur’an) kuna Suratul’Maaidah ambayo ni Sura ya mwisho iliyoteremka kwa Mtume (s.a.w.w.).
Ibn Jariri ametoa kutoka kwa Anasi amesema: “Qur’an ilishuka na mas’hu (kupaka), na Sunna ilileta ghuslu (kuosha).”6
Kwa Sunna, anakusudia tendo la Nabii (s.a.w.w.) kabla ya kushuka Qur’an. Na yajulikana kuwa Qur’an ni hakiimu na nasikhu. Na Ibin Abbas amesema: “Watu hawataki ila kuosha, na wala sikuti ndani ya Kitabu cha Mungu ila kupaka.”7
Kwa mujibu huu yawezekana kuoanisha kati ya yaliyosemwa kutokana na tendo la Nabii (s.a.w.w.) la kuosha na kudhihiri kwa Aya katika kupaka, na kuwa kuosha kulikuwa kabla ya kuteremka kwa Aya.
Na twaona mfano wa hilo katika kupaka juu ya khofu mbili. Ameeleza Haatim bin Ismail, kutoka kwa Ja’far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ali kuwa yeye alisema: (Kitabu kimezitangulia khofu mbili).
Ikrima alieleza kutoka kwa Ibin Abbas alisema: (Kitabu kimezitangulia khofu mbili) na maana yake ni kuwa lau imetokea kwa Mtume muda fulani katika maisha yake, akipaka juu ya khofu mbili, Kitabu kimekuja kinyume chake kikiinasikhi Sunna kiliposema: yaani pakeni juu ya ngozi sio juu ya viatu wala si juu ya khofu wala soksi .5
3. DOLA KUENEZA KUOSHA
Watawala walikuwa wameng’ang’ania kuwa miguu ioshwe mahali pa kupaka na walikuwa wanawalazimisha watu hivyo badala ya kupaka kwa sababu ya uchafu wa chini ya nyayo mbili, na kwa kuwa kiasi kikubwa miongoni mwao walikuwa waendao miguu mitupu bila viatu, wakapenda nafsini mwao kubadilisha kupaka kwa kuosha. Na hilo lajulishwa na baadhi ya habari zilizokuja ndani ya matamko rasmi.
Ibn Jariri alieleza kutoka kwa Hamid, alisema: “Musa bin Anasi alisema hali sisi tuko kwake: Ewe Abu Hamza, kwa hakika al’Hujaaju alituhutubia akiwa Ah’wazi hali sisi tu pamoja naye akasimulia kuhusu tohara, akasema: Osheni nyuso zenu na dhiraa zenu na pakeni baadhi ya sehemu ya vichwa vyenu na sehemu ya miguu yenu, kwani hapana kitu kwa mwanadamu kilicho karibu mno na uchafu wake kuliko nyayo zake mbili, hivyo basi osheni chini yake na juu yake na kano zake mbili.
Anasi akasema:
(Mungu amesema kweli na al’Hujaju amedanganya, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema: (na pakeni baadhi ya vichwa vyenu na baadhi ya miguu yenu na kano zake mbili. Alisema: Na Anasi alikuwa akipaka nyayo zake mbili akizilowesha.
Na linaloweka wazi kuwa propaganda za dola zilikuwa zinaunga mkono kuosha, na humuadhibu asemaye kupaka, kiasi kwamba wasemaji wa kupaka walikuwa na hadhari kudhihirisha itikadi zao, walikuwa hawasemi waziwazi bali kwa kujificha, (dalili juu ya hilo) riwaya ya Ahmadi bin Hambali kwa sanadi yake kutoka kwa Abu Maliki al’Ash’ariy kuwa aliiambia kaumu yake: “Jikusanyeni nikuswalisheni Swala ya Mtume wa Mungu (s.a.w.w.)”
Na walipokusanyika, alisema: “Je katika ninyi kuna mmoja yeyote ambaye si katika ninyi:?” Wakasema: “Hapana, isipokuwa mtoto wa dada yetu.” Akasema: “Mwana wa dada wa kaumu ni katika wao.” Akaagiza bakuli ndani yake mna maji, alitawadha na akasukutuwa na kupandisha maji puani, aliosha uso wake mara tatu na dhiraa zake mbili mara tatu tatu, na akapaka sehemu ya kichwa chake na juu ya nyayo zake mbili, hatimaye alisali.”
Hii ni mitazamo mitatu yawezekana kwayo kuosha kukahalalishiwa mahali pa kupaka pamoja na Kitabu kitukufu kujulisha kupaka. Na wa karibu mno ni wa pili kisha wa tatu.

ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini