Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 3

0 Voti 00.0 / 5

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 3

MWENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA

AAMILU NI NINI KATIKA KAULI YAKE (WA-ARJULAKUM )?
Kwa hakika Aya ya wudhu ni dalili iliothibitishwa juu ya kuwajibika kwa wudhu na namna yake. Nayo ni Aya iliyo wazi iliteremka ili kubainisha nini lazima kwa mwenye kuswali kabla ya Swala. Na hali ya mambo yalaz- imu Aya maalumati zake ziwe wazi.
Dalili yake iwe thabiti, bila ya kuzungukwa na (maana) ya jumla jumla au utata, amesema (s.w.t.):
Na kuainisha moja kati ya kauli mbili kati ya kupaka miguu miwili au kuiosha kwafungika kwenye kumpambanua Aamilu katika tamko Ufafanuzi wake: Kwa kweli katika Aya tukufu kuna Aamilu wawili na vitenzi viwili, kwa mtazamo wa kwanza (utaona) kila moja yafaa iwe ndio Aamilu katika kauli yake: , isipokuwa maneno yapo katika kuain- isha Amilu ni nini kwa mujibu wa usafi wa kiarabu?
Na Aamilu hao wawili ni:
Lau tukisema: Kwa hakika Aamilu ni wa kwanza itakuwa wajibu miguu miwili ioshwe. Na kama tutasema Aamilu ni yule wa pili itakuwa wajibu ipakwe. Hivyo basi kiwajibishi ni kimoja kati ya hao Aamilu wawili walio kizuwizi cha kumuainisha Aamilu katika
Bila shaka mtazamo makini katika Aya, pamoja na kuweka kando fikra ya kila rai zilizopita na kitendo kilichoenea kati ya Waislamu, wathibitisha kuwa wa pili, yaani ndio Aamilu wala sio wa kwanza wa mbali. Ukipenda waweza sema: Kwa hakika Imeungwa juu ya (ma’amulu) wa karibu, yaani vichwa sio juu ya wa mbali, nakusudia: nyuso, na twafafan- ua hilo kwa mithali ifuatayo:
Endapo tutamsikia msemaji akisema:
(Nampenda Zaid na Omari, na nimempita Khalid na Bakari, bila ya kutia irabu kwa kusema: kwa nasbu (litamkwe Bakaran) au kwa jarri (Bakarin), tutahukumu kuwa (Bakari) ameungwa (Khalid). Na msababishaji wake ni kitenzi cha pili, na wala si hajaungwa (Amri) ili ahesabike Aamilu kuwa ni kitenzi cha kwanza.
Wanavyuoni wa Kiarabu wamesema kuwa haki ya kiunganish8 iwe kwa wa karibu sio wa mbali, na hiyo ndio asili na kuiacha (asili hii) ishara yahi- tajika katika usemi, kama si hivyo pengine husababisha utata na kuchanganya lililokusudiwa na lisilokusudiwa.
Hebu tufanye mfano: Raisi atoe agizo kwa mhudumu wake. Mkirimu Zaid na Amri na mpige Bakari na Khalid. Yeye atapambanua kati ya jumla mbili, na ataona kuwa (Amru) ameungwa na (Zaid). Na kuwa (Khalid) ameungwa (Bakari) wala fikrani mwake halitozunguka wazo kinyume na hilo.
Ar-Raziy amenena:
Inajuzukuwa itenganishwa Aamilu wa nasbu katika kauli yake: (arju- lakum) ile kauli yake:
(imsahuu) na inajuzu iwe kauli yake (fagh’siluu) lakini Aamilu wawili wakikutana kwa maamuli mmoja huwa kumtendea kazi Aamilu wa karibu ndio bora.
Kwa ajili hiyo imekuwa wajibu awe Aamilu wa nasbu katika kauli yake (arjulakum) ni kauli yake (wamsahu).
Maelezo: Kwa ajili ya wasomaji wetu wasiopitia lugha ya Kiarabu: Aamilu ma’amulu katika kiarabu neno au jina herufi yake ya mwisho huwa inaka- biliwa na mabadiliko kwa mfano jina Muhammadun wakati mwingine huja Muhammadan na mwingine Muhammadin.
Na hupatikana mabadiliko haya kwa sababu. Hivyo basi msababishaji aliyelifanya hilo jina lipate haya mabadiliko ndiye aitwaye Aamilu. Na maamulu ni: Ni lile jina lililokubali mabadiliko.
Katika jumla ya kwanza tamko Muhammadu limeishia du kwa dhumma kwa sababu ya kutanguliwa na kitenzi Akala, kwa hiyo akala ndio Aamilu.
Jumla ya pili: Ra’aytu Muhammada hapa limekuwa na fat’ha kwa sababu ya kutanguliwa na kitenzi Ra’aytu. Hivyo basi Ra’aytu ndio Aamilu.
Mfano wa tatu: Marartu bi Muhammadi. Muhammadi hapa limekuwa na kasra kwa sababu ya kutanguliwa na bi kwa hiyo bi ndio Aamilu.
Ma’amulu: Ni aliyetendewa, mfano wa jumla hii: Ra’aytu Muhammada, hivyo basi Ra’aytu: ni Aamilu, Muhammada: ni Ma’amulu .
Kwa hiyo imethibiti kuwa kauli yake: (wa arjulakum) kwa kunasibisha laamu yaani kutia fat’ha kwawajibisha mas’hu (kupaka)9
Hali ikiwa kama hivyo haifai kutoka nje ya utaratibu katika mifano ya busara, maneno ya Bwana Mwenye enzi ni bora mno yawe hivyo. Wala mfano hauishii kwenye mfano tulioutaja, bali wewe waweza kuleta mifano mbali mbali ilimradi tu iwe yashabihiana na ulio katika Aya.
Lau utaileta Aya hii kwa Mwarabu halisi aliyejiweka nafsi yake mbali na madhehebu anayojiambatanisha nayo, na umuulize kuhusu dalili ya Aya atakujibu: Kuna viungo ambavyo ni wajibu kuviosha, navyo ni nyuso na dhiraa, na kuna viungo ambavyo ni wajibu vipakwe, navyo ni vichwa na miguu.
Lau utamgeuza mtazamo wake aangalie kwenye kanuni za lugha ya Kiarabu utamuona hatangitangi (kusema) kuwa Aamilu wa (ru’usi) vichwa na (arjuli) miguu ni kitu kimoja nayo ni kauli yake: (famsahuu) wala haitozunguka mawazoni mwake fikira ya kutenganisha kati ya (ru’usu) vichwa na miguu, awe Aamilu katika vichwa ni kauli yake: (fagh’siluu).
Na endapo dalili ya Aya itakuwa wazi kuihusu mojawapo kati ya kupaka na kuosha, hatutahitajia kitu kingine, kwa kuwa atakayeafiki atatilia nguvu madhumuni ya Aya, na atakaye khalifu atajaribu aina ya njia ambazo iliyo bora katika hizo ni kuwa imenasikhiwa na Kitabu.
QIRA’A MBILI NA KUPAKA JUU YA MIGUU
Kwa kweli kutofautiana kwa wasomi katika tamko (wa arjulakum) kwa fat’ha na jarri hakuathiri kitu kuhusu dalili ya Aya kuwa yawajibisha kupaka, kwa kuwa aina hizi mbili za usomaji zinaafikiana na kauli ile (ya kupaka) bila ya mushkeli wowote.
Ufafanuzi wa hilo: Kwa hakika Naafiu na Ibin Aamiru na Aaswimu wameisoma kauli yake (s.w.t.) (katika riwaya ya Hafsa: (wa arjulakum) kwa nasbu – fat’hah - na huu ndio usomaji ulio maarufu ambao upo ndani ya misahafu iliyoenea katika kila zama na kila kizazi.
Na Ibin Kathir, Hamzah na Abu Amri na Aaswimu wameisoma katika riwaya ya Abu Bakr kwa jarri.- kasra.
Na sisi tunasema: Kwa kweli usomaji aina mbili unawiana na kauli ya kupaka bila ugoigoi wala kutaradadi.
Ama ya pili, yaani usomaji wa jarri – kasra - nayo ni ushahidi wenye nguvu wa kuwa miguu imeungwa juu ya kauli yake: (biru’usikum) kwa kuwa soma hii ya jari - kasra haina sababu ila ni kuwa imeungwa na (tamko) la kabla yake.
Na hapo miguu inakuwa imehukumiwa kupakwa bila ya shaka. Ama usomaji wa nasbu sababu katika hilo ni kuwa kuunga kwa kufuata mahali pa (biru’usikum) kwa kuwa ni mansubu mahalan yaani mahali pa maf ’uli kwa kauli yake: (wamsahu) kwa hiyo miguu pia inahukumiwa kupaka tu. Na kuatifia mahali ni jambo lililoenea katika lugha ya Kiarabu, na pia imekuja katika Qur’an tukufu.
Ama kuhusu Qur’an amesema (s.w.t.):
“Kwa hakika Mungu ni mwenye kuepukana na washirikiina na Mtume wake - mwenye kuepukana nao” kwani usomaji (warasuluhu) kwa dhumma ni usomaji ulio maarufu ulioenea, na hakuna sababu ya kuisoma kwa dhumma ila ni kwa kuwa imeungwa kwa kufata mahali pa ismu inna. Nakusudia: Laf ’dhuljalalah katika kwa kuwa ni mubtadau.
Maswala ya kuunga kwa kufuata yamejaza vitabu vya irabu, kiasi kwamba Ibn Hisham amefanya mlango mahususi wa atfu alal’mahali na ameeleza sharti zake.
Ama katika fasihi ya kiarabu ielezee - atfu alal’mahali- hapana taabu. Msemaji amesema:
Hivyo basi usemi wake (walalhadiida) kwa nasbu at’fu ala mahali kwa kuwa ni khabari ya laysa katika usemi wake (falasna). Kwa hiyo tumefikia natija ifuatayo: Kwa kweli kutofautiana kwa usomaji huu wa namna mbili hakuathiri kitu kuainisha kauli ya kupaka, somo la usomaji huu wa namna mbili litaku- fikia kikamilifu kuihusu kauli ya kuosha.
Kisha ni kwamba kundi la wanataaluma wajulikanao wa Kisunni wamesema wazi kuwa Aya yajulisha kupaka, wakisema kuwa kauli yake (s.w.t.) (wa arjulakum) imeunganishwa na Aamilu wa karibu sio wa mbali, na kwamba Aamilu hapa ni (famsahu).
Na twataja baadhi ya maneno hayo:
Ibn Hazmi amesema: Ama kauli yetu kuihusu miguu miwili kwa kweli Qur’an imeshuka na kupaka, amesema (s.w.t.): (wamsahu biru’usikum waarjulakum), sawa iwe imesomwa kwa kutia kasra lamu au kwa kuitia fat’ha, hali yoyote iwayo ikiwa imeungwa na ru’usi itakuwa ima ni kufuata tamko au kufuata mahali, wala si kuhusu kinyume na hivyo.10
Ar-raziy amesema: “Ama usomaji wa jarri kasra walazimu miguu iwe imeungwa na vichwa, kwa hiyo kama ilivyowajibika kupaka kichwani basi ni hivyo hivyo miguuni. Ama usomaji wa nasbi, pia wamesema wawajibisha kupaka.
Hivyo ni kwa sababu kauli yake: (wamsahu bi ru’usikum) iko mahali pa nasbi, ila tu imekuwa na kasra kwa sababu ya kuingiwa na ba’u, kwa hiyo miguu kuiunganisha na vichwa itakuwa ruhusa katika miguu kuwa na nasbi ikiwa imeungwa kwa kufuata dhahir, na huu ni mwendo wa wananahau mashuhuri.
Na Sheikh Sindiy al-Hanafiy amesema: baada ya kukata shauri kuwa kwa kweli dhahiri ya Qur’an ni kupaka - na hii ndio tamko lake:
Kupaka kumekuwa ndio dhahiri ya Qur’an, kwa kuwa usomaji wa jarri ni dhahiri katika hilo - la kupaka - na usomaji wa nasbu yachukuliwa kwa kuifanya kuunganisha kwa kufuata mahali.11
Na huenda kadiri hii ya nukuu yatosha kubainisha kuwa usomaji wote wa namna mbili zote utatilia mkazo kupaka tu na kuambatana nako bila ya mushikeli.
USOMAJI WA NAMNA MBILI NA KUOSHA MIGUU
Kwa kweli umejua kuwa tofauti ya usomaji katika kauli yake: (wa arju-lakum) haiathiri usemi wa kupaka miguu miwili sawa tuisome kauli yake (wa arjulakum) kwa nasbu yaani fat’ha au tuisome kwa jarri-kasra, soma hizo mbili zote zinatilia nguvu wajibu wa kupaka, na yafuatia kuwa Aamilu katika kauli yake: (arjulakum) ni ile kauli yake: (famsahuu) na tamko (wa arjulakum) limeungwa na (biru’usikum) aidha kwa tamko au mahali.
Maneno yapo katika uwezekano wa kuitekeleza kauli ya kuosha kulingana na usomaji wa namna mbili uliyo maarufu na kadiri ya kulingana kwake na soma hizo na kanuni za lugha ya kiarabu.
Na itabainika kupitia somo hili kuwa kulazimisha kuosha kwa mujibu wa Aya hii ni ukiukaji ulio dhahiri wa kanuni za kiarabu, na ubainifu unakujia:
KUOSHA NA USOMAJI WA NASBU (FAT’HA)
Ikiwa tutasema Aya ni dalili ya kuosha miguu, hapana budi Aamilu atakuwa kauli yake katika jumla iliyotangulia (fagh’silu) na iwe imeungwa na kauli yake: (wujuhakum) na hii yalazimu kutenganisha kati ya ma’atufu ambaye ni (wa arjulakum) na maatufu alayhi (wujuhakum) na jumla ngeni nayo ni (wamsahu biru’usikum) hali ikiwa hatenganishwi kati ya maatufu na maatufu-alayhi hata na (tamko la) neno moja sembuse jumla mzima ngeni! Wala haijasikika katika maneno ya Kiarabu fasaha msemaji aseme: kwa kuunga (Umaran ala Zaidan).
Ibn Hazmi amesema:
Haifai kuiunga arjulakum na wujuhakum, kwa sababu si ruhusa izuilike kati ya ma’atufu na maatufu-alayhi na jambo lingine jipya12
2-Abu Hayyani amesema: Na mwenye kusema kuwa usomaji wa nasbu katika (arjulakum) kuwa ni kuunga kwa kufuata kauli yake: (fagh’silu wujuhakum wa aydiyakum) na akatenganisha kati yao na jumla hii ambayo ni kauli yake: (wamsahuu biru’usikum) ni mbali, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuweka mtengano kati ya at’fu na ma’atufu -alayhi na jumla ya insha13
3-Sheikh Al-Halabiy kuihusu tafsiri ya Aya hii amesema: Nasbu (wa arju- lakum) ni kwa ajili ya mahali na jarri yake ni kwa ajili ya tamko. Na wala si ruhusa iwe nasbu kwa ajili ya kuunga juu ya wujuhakum kwa sababu ya mwanya kati ya maatufu na maatufu-alayhi kwa jumla ngeni nayo: (wamsahu biru’usikum), na kimsingi wasitenganishwe kati yao hata kwa neno moja sembuse jumla. Wala haijasikika katika lugha fasaha mfano wa:
Nimempiga Zaid na nimempita Bakari na Amri kwa kumuunga Amri na Zaid!14
Na Sheikh As-Sindiy amesema: “Na kuichukulia kisomo cha nasbu kwa kuunga kwa kufuata mahali ni karibu mno kwa sababu ya kufuatana kwa matumizi ya (atfu alaa-mahali) juu ya mahali, pia matumizi hayo yana sababu ya kujiepusha kuingiza mwanya wa neno geni kati ya, maatufu na maatufu-alayhi, kwa hiyo imekuwa dhahiri ya Qur’an kupaka.
Na15 yasiyo kuwa hayo miongoni mwa maneno yanayobainisha kuwa usomaji wa nasbu na kuelewa kuwa wajibu ni kuosha unalazimu kukiuka kanuni ya sarufi ya kiarabu.
Kuosha Na Usomaji Wa Kasra
Kwa kweli wanaosema kuosha miguu wamehalalisha usomaji wa nasbu kwa sura ambayo umeujua udhaifu wake, na kutokuwa na uwiano na sarufi ya Kiarabu.
Lakini waliposimama juu ya usomaji wa jarri, na kwamba wenyewe wajulisha wajibu wa kupaka sio kuosha wameduwaa katika kuhalalisha na kuuelekeza itolewe kauli ya kuosha, kwa kuwa usomaji wa jarri uko wazi kuwa tamko (waarjulikum) limeungwa na ( bi ru’usikum) kwa hiyo hukumu yake inakuwa hukumu ya ru’usi), hapo basi walinepa, ‘kulia kushoto’ ili wapate kwa ajili ya usomaji wa jarri pamoja na kauli ya kuosha kihalalishi, nacho si kingine ila usemi wa kuwa hiyo jarri ni kwa sababu ya jiwari yaani ukaribu.
Na matokeo: kuwa tamko lake(wa arjulakum) limehukumiwa nasbu kulin- gana na sarufi kwa kuwa limeungwa juu ya kauli yake: (wujuhakum), laki- ni limejipatia irabu ya jarri kutokana na kauli yake: (biru’usikum) kwa sababu limekuwa pembezoni mwa tamko ambalo ni majururu na hii ndio isemwayo (aljarru biljiwari) yaani tamko lililoambukizwa jarri kwa sababu ya ujirani, nako ni kuliacha tamko mbali na irabu yake ya asili na kuchukua irabu ya tamko la jirani yake.
Na wametolea mfano kwa kauli yao:kwa kuwa kauli ni khabari ya kauli ya: lakini limesomwa kwa jarri kwa sababu ya kuwa kwake pembezoni mwa kauli kwa kuwa ni maj’ruru kwa kuwa ni mudhwafu ilayhi.
Na kwa kuwa jarri ya ujirani kawaida huwa haiwi katika lugha fasaha, na endapo itakuwa kwa mfano, huwa ni kwa kutimiza sharti, na hapa sharti zimekosekana. Tutatoa ufafanuzi katika mlango ufuatao.
KUTIA KASRA KWA UKARIBU KUSIHI NA SHARTI ZAKE
Madamu wasemaji wa kuosha miguu wanatafsiri usomaji wa jarri kwa ujirani, hapa tunatoa maneno ya wanazuoni wa fasihi ili ieleweke umbali wa kufaa kwa matumizi ya jarri ya ujirani, na lau itakuwa sahihi, ni zipi sharti zake?
Az-Zujaju amesema: “Huenda ikasemwa kuwa (wa arijulikum) ni majruru kwa ajili ya ujirani, yaani kwa sababu ya kuwa pembezoni mwa arru’usi iliyo majruru, mfano wa kauli ya msemaji: Juh’ru dwabi kharbi, kwani (kharbi) ni khabari ya (al’juh’ru) kwa hiyo ni lazima iwe mar’fuan, lakini imekuwa majruru kwa ajili ya ukaribu. Hivi, halafu amepingwa kwa kauli yake: Na hiyo sio sahihi, kwa sababu ya kuafikiana wanazuoni wa lugha ya kiarabu kuwa irabu ya ukaribu ni irabu isio ya kawaida na ni ya nadra. Na (irabu) ambayo hali yake huwa hivi haifai kuichukulia Qur’an bila ya dharura inayolazimisha hilo.
Alaud-Diini Al-Bugh’dadiy amesema ndani ya tafsiri yake iitwayo ‘Al- Khazinu’: “Ama mwenye kuifanya laamu iwe na kasra katika (al’arjuli) kwa sababu ya ukaribu wa tamko sio hukumu. Na wamelitolea dalili kwa kauli yao: (Juhru dwabbi kharbi) na akasema: Alkharbu ni sifa ya Al’juhru sio ya Adwabbi, ila tu imechukua irabu ya Adwabbi kwa ukaribu, si sahihi kwa sababu mbili:
a. Kwa kuwa kasra ya ukaribu hutumika kwa sababu ya dharura ya kiushairi, au hutumika unapopatikana usalama wa kutochanganya (maneno), kwa kuwa Alkharbi haiwezi kuwa sifa ya dwabbi – fisi - bali ni ya Aljuh’ru (shimo).
b. Na kwa sababu kasra ya ukaribu huwa bila ya wau ya kuunga, ama pamoja na wau ya kuunga Waarabu hawajasema.16
Asyrafiy na Ibni Jiniy wamepinga kasra ya ukaribu na wameifanyia taawili kauli yao (kharbi) kwa jarri - yaani kasra, kwa kuwa ni sifa ya Adwabbi, fisi. Na mwenye kutaka ufafanuzi na arejee Al-Mugh’niy.17
Ibn Hisham amesema: “Jarri ya ukaribu haiwi pamoja na herufi ya kuunga kwa sababu herufi ya kuunga inazuwia kukurubiana.”
Muhtasari wa maneno ambayo tumeyanakili kwa ufupi ni mambo yafuatayo:
Kwanza: Kuwa kasra ya ukaribu haijathibiti katika usemi fasaha.
Pili: Kuwa kasra ya ukaribu endapo itathibiti kwa mfano, itakuwa aidha kwa sababu ya dharura ya kiushairi au kwa sababu ya kufanya uzuri chapa inayofanana kati ya matamko mawili yaliyo karibu. Na sababu mbili hizi hazipo kwenye maudhui hii. Hapa hakuna dharura ya kiushairi wala kuifanya vizuri chapa katika kulitoa tamko (wa arjulikum) mbali na irabu yake halisi na kulipatia irabu ya jirani yake.
Tatu: Kuwa kuunga kwa ukaribu kunafaa mahali ambapo kuna usalama wa kutogubikwa na tuhuma kama ilivyokuja katika mfano ulio maarufu kwa kuwa (kharbi) ni sifa ya shimo sio ya fisi japo itiwe kasra, kinyume na mahali hapa kwa kuwa usomaji wa jarri wasababisha tuhuma, lau ingekuwa miguu kwa ukweli imehukumiwa kuoshwa, kwa hiyo kuitia jarri kwa ujirani kwaleta tuhuma kuwa miguu imehukumiwa kupakwa na kwamba yenyewe imeungwa na vichwa bila ya msemeshwa kuwa na wazo la kuwa jarri hii ni ya ukaribu, hapana haja ya kuifanya aina hii ya jarri ambayo dhahiri yake inapingana na makusudio ya msemaji.
Nne: Jarri ya ukaribu haijathibiti ila katika sifa, badali, na mfano wake sio katika kiungwa kama ilivyo katika Aya .

Kutokana na utafiti huu imedhihiri kuwa usemi wa kupaka unaambatana na kila moja ya soma hizi mbili bila ya hata chembe ya tafsir wala taabu, hii ni tofauti na kauli ya kuosha, kwani kauli hiyo haiwiani si na usomaji wa nasbi-(fat’ha) wala ya jarri (kasra).

ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini