Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 4

0 Voti 00.0 / 5

UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 4

MWENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA

IJITIHADI KUIKABILI TAMKO LA KISHERIA
Kwa kweli maafa ya fiq’hi ni kushikamana na itibari na sababu za mapendekezo ili kulikabili tamko la kisheria, kwa kuwa yakinza madhehebu ya taabudiy - kujitoa. Kwa kuwa Muislamu anaitii (Nassu) tamko la kisheria - afikie afikako - haitangulizi rai yake mbele ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Kitabu na Sunnah ndio tako la kisheria, na Sunna sahihi za Mtume wake(s.a.w.w.) (ndio Nassu pia), na hiyo ni alama ya kusalimu amri kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake na Kitabu chake na Sunna zake. Amesema (s.w.t.):
Yaani msitangulie mbele ya Mungu na Mtume wake kwa kulazimisha rai zenu kwa Mtume na umma wa kiislamu. Kwa sababu kutanguliza sababu za mapendekezo mbele ya tamko rasmi ni kutangulia mbele ya Mungu na Mtume wake. Yenye neema ni yale aliyoyasema Imamu Shafiy:
“Mwenye kufuata mapendekezo atakuwa amefanya sheria”.
Si mmoja katika masunni walio mashuhuri waliofahamu kuwa dhahiri ya Aya au uwazi wake ni kupaka miguu miwili, na hilo wamelitambua kwa dhamira zao au kwa ndimi zao na kalamu zao. Lakini kutii madh’habu za maimamu wanne na wengine kumewazuwia wasiichukuwe malengo ya Aya. Hivyo basi wakafuata madh’habu zilizorithiwa badala ya kuifuata Qur’an Tukufu.
Lau wao wasingekulia na fikra hii tangu uchanga wa kucha zao, wasingezitanguliza maoni yao mbele ya Kitabu kitukufu cha Mungu kijulishacho kupaka, na wangezikomboa fikra zao kutoka vifundo vya ufuasi. Kwako kinakujia namna ya kitu fulani kutoka maoni kama haya ambayo akili hairidhiki wala dhamiri iliyo huru.
KUOSHA KWAINGIZA NDANI YAKE KUPAKA
Al-Jaswasu amedhania kuwa Aya ya wudhu ina maana ya jumla hivyo basi hapana budi hadhari (ih’tiati) ifanywe, nayo ni kuosha ambako ndani yake kuna kupaka pia, kinyume na kupaka, kwa kuwa ndani yake hakuna kuosha, kisha ameondoa kitendawili cha Aya kwa madai ya kuafikiana wote kuwa lau akiosha atakuwa faradhi ameitekeleza.18
Izingatiwe Kwanza ni kwamba vipi ameisingizia Aya kuwa ina maana ya ijmalu hali ikiwa na dalili ya wazi, kwa kuwa iko katika kubainisha nini wajibu juu ya wanaoswali wote wakati wanapotaka kuswali, katika mfano kama huu inabidi iwe yenye kubainisha mradi wa Aya, isiyotazamiwa kuwa na maana ila moja. Isipokuwa tu kilichomfanya aseme ijimalu ni kuikimbia dhahiri ya Aya ijulishayo kuwa wajibu wa miguu ni kupaka sio kuosha.
Pili: Kwa kweli asemalo, eti kuosha ndani yake kuna kitu kupaka na wala si hivyo kinyume chake, kwa kuwa hakuna kuosha. (usemi) huu si sahihi, kwa sababu mradi wa kuosha katika maana yake ya maudhui ni kutiririsha maji juu ya kiungo, kama ambavyo mradi wa kupaka ni kupitisha mkono juu ya kiungo kwa umajimaji uliobaki mkononi, hapo basi kuosha na kupaka huwa faradhi mbili tofauti, kwa namna ambayo kila moja iko tofauti na nyingine, si kuosha imo ndani ya kupaka wala kupaka ndani ya kuosha.
Tatu: Madai ya kuondoa utata wa Aya kwa kuwa akiosha atakuwa ametekeleza faradhi yake kwa maafikiano ya wote ni mswada wa litakiwalo, kwa kuwa vipi anadai maafikiano juu ya hilo hali ikiwa wasemao kupaka kati ya Swahaba na Taabiina, majina yao yatakujia, si wachache kuwalinganisha na wasemao kuosha kama ambavyo Imamia nao ni robo ya Waislamu wote wanaona kuosha ni batili na kupaka ni lazima, sasa u-wapi huo muwafaka wa wote juu ya kuosha!
SUNNA KUKINASIKHI KITABU
Kuna ambaye aionaye Aya wazi yajulisha kupaka na yuaibatilisha kauli isemayo kuwa miguu yenu imeungwa juu ya kauli yake: (wujuhakum) na anasema: Haifai kabisa kuwe na kizuizi cha habari ambayo si ya maatufu kati ya maatufu na maatufu alayhi, kwa kuwa hivyo husababisha utata na kufunika na ni kupotosha si kubainisha. Huwezi ukasema:
(Nimempiga Muhammad na Zaid na nimempita Khalidi na Amri), hali ikiwa wewe kimsingi wataka kusema umempiga Amri aslan. Na Sunnah ilipokuja na amri ya kuosha miguu miwili imekuwa sahihi kuwa kupaka miguu kumeondolewa19
Izingatiwe kwanza: Kuwa haifai kuondoa hukumu ya Kitabu isipokuwa kwa Sunna iliothibiti, kwa kuwa Kitabu ni dalili iliyothibiti huku yake haiondolewi ila na dalili iliyothibiti mfano wake.
Ama hapa Sunna inayoonyesha kuosha inapingana na Sunna inayoonyesha kupaka. Vipi iwe yawezekana moja kati ya dalili mbili zinazopingana itan- guilizwe mbele kuliko Qur’an tukufu bila sababu yenye uzito?
Zitakujia riwaya zinazoungana mkono zionyeshazo kuwa Mtume (s.a.w.w.) na swahaba wake walikuwa wanapaka miguu badala ya kuosha.
Pili: Umma umeafikiana kuwa Sura ya Al-Maidah ni ya mwisho kuteremka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kuwa haikuondolewa hukumu hata Aya moja kutoka humo. Na riwaya zimepita na kauli nyingi za swahaba zionyeshazo hivyo.
Tatu: ilimlazimu Ibni Hazmi aifanye Aya iwe dalili ya haikuondolewa hukumu kwa Sunah, lau ingethibiti kuwa Mtume aliosha miguu yake muda fulani katika umri wake basi Aya ndiyo yenye kuondoa huku ya Sunna sio kuwa Sunna imeinasikh Qur’an.
ZINDUO KUWAJIBIKA KUWA MWANGALIFU WAKATI WA KUMWAGIA MAJI
Zamakhshari alifahamu kuwa usomaji wa jarri wamlazimisha mtu aipake miguu sio kuiosha, akawa katika lengo la kuizuia dalili, na kwamba miguu ingawaje imeatifiwa juu ya vichwa pamoja na hivyo uungaji unakosa dalili ya kuosha, alisema:
Jamaa wamesoma (wa arjulakum) kwa fat’ha ikawa imejulisha kuwa miguu ya kuoshwa.
Ukisema: Utafanya nini na usomaji wa jarri na huingia katika hukumu ya kupaka?
Nitasema: Miguu ni miongoni mwa viungo vitatu vya kuoshwa, huoshwa kwa kumiminia maji juu yake, kwa hiyo kukawa na dhana ya kufanya israfu iliyokatazwa, hivyo ikaungwwa kwenye kiungo cha tatu kinachopakwa sio kwa sababu ipakwe (miguu) bali kutanabahisha kuwa matumizi ya wastani ni wajibu wakati wa kumiminia maji juu yake, na imesemwa mpaka nguyu mbili
Izigatiwe kwanza: Kuwa sababu alizo zisema zitasihi tu ikiwa nukta ni ile ielewekayo na wasemeshwa wote katika waumini, mbali walioje na nukta hii ambayo Zamakh’shariy ameibuni akielekeza kwenye madh’hebu yake! Kwa ibara nyingine: Nukta aliyoisema itakuwa sahihi endapo itakuwa salama mbali na kugubikwa na utata, si katika nafasi ambayo haina usalama huo.
Na yafuatia lichukuliwe tamko la dhahiri kuwa kupaka ni wajibu, ighafilikiwe nukta adhimu ya Sheikh Zamakh’shariy!
Pili: Mikono pia ni mahali pa kudhaniwa israfu kama miguu, basi ni kwa nini hakutanabahisha wajibu wa matumizi ya wastani katika kumwagia maji mikono pia?!
Hayo yote yanadhihirisha kuwa sababu hizi ni njia ya kuwaelekeza watu kwenye madh’hebu ambayo Bwana wa Al-Kashaafu amekulia na kama si hivyo haingemjia moyoni mwake sababu hii.
URAHISI WA KUOSHA MIGUU MIWILI SI KAMA VILE NYWELE
Ibin Qudaama alipofahamu kuwa muktadha wa kuatifia al’arjuli ala ru’usi ni al’mas’hu kupaka, sawa isomwe kwa nasbu au kwa jarru, hapo akaan- za kuleta falsafa na kufanya jitihada kuikabili dalili iliyo thabiti na akasema: “Kuna tofauti kati ya kichwa na mguu, na kwa mujibu huo hai- wezekani viwili hivyo vihukumiwe hukumu moja, na sababu ni:
1. Kinachopakwa kichwani ni nywele ambazo huwa taabu kuziosha, na miguu miwili ni kinyume na hivyo kwa hiyo hiyo yashabihiana mno na vioshwavyo.
2. Kwamba miguu miwili ina mpaka huishia hapo kwa hiyo yashabihiana na mikono miwili.
3. Kwamba miguu miwili iko kwenye hatari ya kuchafuka kwa kuwa hukanyaga kwayo ardhini kinyume na kichwa.
Izingatiwe: Kuwa ni ijitihadi binafsi katika kulikabili tamko rasmi la sheria na kutia falsafa katika hukumu.
Ama (hoja) ya kwanza: Hivi kuna mashaka gani katika kuosha nywele endapo kioshwacho kikiwa sehemu ya hizo nywele, kwa kuwa ndio wajibu katika kupaka, basi na iwe hivyo wakati wa kuosha.
Ama ya pili: Kushikilia hoja ya kushabihiana ni hoja dhaifu sana kwa kuwa vingi vilioje vishabihianavyo vyatofautiana katika hukumu. Na sababu ilio fasidi mno kuliko hiyo ni ile ya tatu, kwa kuwa miguu miwili kuwa kwake katika hatari ya kuchafuka hailazimu kuainishiwa kuosha, kwa kuwa ase- maye kupaka anasema kuwa ni wajibu miguu iwe tohara kisha ipakwe.
Kwa umri wangu, hakika sababu hii na iliyotangulia ya Zamakhshariy ni kuichezea Aya kwa lengo la kuyaunga mkono madhehebu. Linalopendeza kwa mwana fiq’hi mwerevu ni kuifanyia kazi Aya, sawa iafikiane na mad- hehebu ya Imamu wake au hapana. Na bwana wa tafsiri Al-Manar ana neno la maana sana kuwahusu hawa wanaotanguliza fatwa za maimamu kuliko Kitabu kitukufu na Sunna sahihi, asema: “Kwa kweli kufanya amali kwao ni kwa kulingana na kauli za vitabu vyao mbali na kitabu cha Mungu na Sunna za Mtume wake.
Kuwafuata (wanazuoni) waliopita katika kuosha
Ibin Taymiyya alipofahamu kuwa usomaji wa kasra yalazimu kuiunga miguu na (hukumu ya) vichwa na italazimu kuipaka miguu miwili sio kuiosha, alikimbilia kulifanyia tafsiri ‘tamko rasmi la kisheria, na akasema: “Na mwenye kusoma kwa kasra, maana yake si (wamsahu arjulikum) pakeni miguu yenu) kama wanavyodhania baadhi ya watu, kwa sababu kadhaa, moja yake:
Kwa kweli waliosoma hivyo katika salafu,-walio tangulia -walisema: amri limerudi kwenye kuosha.”20
Izingatiwe: Kuwa endapo yatakuwa sahihi aliyoyasema italazimu isemwe kuwa Salafu waliiacha Qur’an nyuma ya migongo yao na wakayachukuwa yasiyoafikiana na Qur’an. Lau kurejea kwao kutakuwa kwa ajili ya kuon- dolewa hukumu ya Kitabu, umekwishajua kuwa hukumu ya Qur’ani haindolewi na khabari ya Aahadi. Na hata tukikubali kuwa kuinasikhi ni jaizi, haijaondolewa hukumu yoyote kutoka katika Sura ya Al-Maidah.
Na miongoni mwa ajabu ni kuwa Ibni Taymiyya amejikinza mwenyewe, amesema katika sababu ya saba, hii ndio nassu ya usemi wake: Arabic text (inna tayammuma juila badalan minal wudhui indal haadja fahudhifa shatru a’adhwail’wudhui wa khufa ash shatru thaani, wadhalika fainnahu hudhifa ma kana mamsuhan wa musiha makana magh’sula.)21
(Kwa kweli tayammamu imefanywa badala ya udhu wakati wa haja, hivyo basi vimefutwa nusu ya viungo vya udhu na kufanywa wepesi nusu ya pili, na hivyo vimefutwa vilivyokuwa vikipakwa na kupakwa vilivyokuwa vikioshwa).
Kama tayammamu msingi wake utakuwa kufuta kilichokuwa kikipakwa itakuwa hukumu ya miguu imefutwa katika tayammamu, hivyo italazimu hukumu yake iwe kupaka ili iwe sahihi kuifuta, na lau itakuwa hukumu yake ni kuosha itakuwa haikufutwa, itabaki kama uso na mkono na hupakwa!
KUIWEKEA MPAKA AYA YA KUOSHA
Kwa hakika mfasiri maarufu kwa jina la Sheikh Ismail Haqiy Al- Burusawiy ameunga mkono kauli ya
kuosha kwa sababu kupaka hakujaeleza mpaka ila tu kuwekewa mpaka kumekuja katika viungo vioshwavyo.
Kwa maneno yake haya anakusudia kuwa miguu imewekewa mpaka wa ka’abu mbili kwa hiyo kuosha ka’abu mbili kumeshabihiana na mikono iliyowekewa mpaka wa viwiko. Kwa hiyo yahukumiwa kuoshwa kwa hukumu ya ushirika katika kuwekewa mpaka.
Izingatiwe: Kuwa kila moja kati ya vioshwavyo na vipakwavyo katika Aya vimekuja na mpaka na bila ya mpaka. Kwa hiyo nyuso katika Aya huoshwa wala haukuwekwa mpaka, na mikono huoshwa na mpaka umewekwa kwa kauli yake: (ilalmarafiqi) hivyo basi yajulikana kutokana na hali hiyo kuwa kuosha pengine huwa na mpaka na pengine bila ya mpaka, hivyo basi mpaka sio dalili ya kuwajibika kuosha wala kukosa mpaka sio dalili ya kuwajibika kupaka, na hali ni hiyo kwenye kiungo kipakwacho, kwani miguuu kulingana na ilivyochaguliwa - hupakwa na huwa na mpaka, ni mpaka kwenye kaabu mbili, na kichwa hupakwa nacho.
UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA
hakina mpaka. Hivyo basi kuifanya mipaka ndio alama ya kuosha yafanana mno na kuifanya a’am kuwa ni dalili ya akhasu.
Na alilosema kuwa katika kupaka haukuja mpaka wowote, maneno ameyafanyia ta’awili ni sawa na kuyafanya madai ndiyo dalili.
Lau tukisema kwa kuzizingatia pendekezo kama hizi, kwa mujibu wa uzuri wa lugha yalazimu miguu iwe yenye kupakwa si kuoshwa.
Al’Murtadha amesma: “Kwa hakika ndani ya Aya muna utajo wa kiungo cha kuosha kisichowekewa mpaka nacho ni uso, na kime’atifiwa au kuungwa na kiungo cha kuoshwa chenye mpaka nacho ni mikono miwili, kisha ikaanzwa kutajwa kiungo kipakwacho kisicho kuwa na mpaka nacho ni kichwa, basi ni wajibu miguu iwe ya kupakwa nayo imewekewa mpaka na imeungwa si viungo vingine, ili jumla mbili zikabiliane katika kuungwa kinachooshwa chenye mpaka juu ya kioshwacho kisicho kuwa na mpaka, na katika kuungwa kipakwacho chenye mpaka juu ya kipakwacho kisicho na mpaka22
REJEA NI SUNNA ENDAPO AINA MBILI ZA USOMAJI ZITAPINGANA
Madh’habu ya Alusiy ni kuwa aina mbili za usomaji zilizozagaa zenye kupingana zinakuwa kama Aya mbili zinazopingana, na asili ifuatwayo katika mfano kama huu ni kuzidondosha zote mbili na kurejea kwenye Sunna!
Amesema: “Kwa hakika aina mbili za usomaji zilizozagaa kwa ijimai ya makundi mawili, bali kwa itifaki ya Waislamu wote, na miongoni mwa kanuni za Usuli kwa makundi mawili kuwa aina mbili zilizozagaa za usomaji endapo zitapingana katika Aya moja, zitakuwa na hukumu ya Aya mbili, hapana budi kwetu tufanye juhudi na kujitahidi kwanza kuziowanisha kwa kadiri iwezekanavyo. Kwa sababu asili ya dalili ni kuzitendea kazi sio kuzitelekeza kama ilivyokubalika kwa wana usuli, baada ya hapo tutafute ya kuitilia uzito kati ya mbili hizo, na endapo haikutuwia wepesi kuitilia uzito tutaziacha na kuelekea kwenye dalili zingine katika Sunna.
Izingatiwe: Ni miongoni mwa ajabu kujalia visomo viwili kuwa zinapingana baada ya hapo tufanye juhudi kuondoa upinganaji kwa njia ambazo msemaji amezisema, kwa sababu kujaalia mfano wowote wa kupingana kati ya aina mbili za usomaji ni rehani ya kuzusha dhehebu katika Qur’an na kulitendea kazi, kama si hivyo basi visomo viwili havina upingano wala (hakuna cha) kudondoshwa, hivyo vyote viwili zinalenga jambo moja nalo ni kupaka miguu miwili, kwa kuwa kauli yake (s.w.t.): (wa arjulakum) visomo hivyo vyote viwili vimeungwa na tamko moja nalo ni kauli yake: (ru’usikum) lakini ima ni atfu juu ya mahali kwa hiyo hufanywa nasbu yaani fat’ha au kuungwa kwa kufata tamko kwa hiyo hufanywa jarri kasra.
KUOSHA NI NYONGEZA YA MTUME (S.A.W.W.)
Jamalud Dini Al-Qasimiy anasema kuwa Aya iko wazi kuwa fardhi ni kupaka kama alivyosema Ibnu Abbas na wengine, lakini kuitilia maanani kuiosha miguu miwili katika Ma’athur ni kuizidisha katika fardhi na kuipanua kulingana na kawaida yake, kwa kuwa yeye amefanya katika kila faradhi Sunna inayoiunga na kuipa nguvu katika Swala, Zaka, Saumu, na Hijja.
Na miongoni mwa yajulishayo kuwa wajibu wake – miguu - ni kupaka ni kule kufanywa kwa sheria ya kupaka juu ya khofu mbili na socksi, nalo halina sanadi ila ni Aya hii. Kwa kuwa kila Sunna asili yake ni ndani ya Kitabu cha Mungu kwa matamshi au kwa inavyofahamika. Jua hivyo na hifadhi na Mungu ndio mwongozi.23
Izingatiwe: Mtume (s.a.w.w.) ameepukana na sifa ya kuzidisha au kupun- guza katika faradhi, bali yeye amefuata wah’yi na kaulimbiu yake ilikuwa:
(Qul innama atabiu maa yuhaa ilayya min Rabbiy) (Al’A’araf: 203).
(Sema: Mimi ni mwenye kufuata wahyi tu kutoka kwa Mola wangu) na kauli yake:
(Qul ma yakunu liy an ubadilahu min tilqai nafsiy in atabiu ila maa yuuha ilayya) 10:15
(Sema sikuwa niibadilishe itakavyo nafsi yangu sifuati isipokuwa wahyi ufikao kwangu).
Lau azidishe (kitu) katika swala ni kwa amri kutoka kwa Mungu (s.w.t.).
Kisha lau atazidisha azidishacho huzidisha ambacho kimethibiti asili yake kwa Sunna, sio kwa Kitabu kitukufu kama kuongeza rakaa mbili kwenye swala za rakaa nne na rakaa katika swala ya rakaa tatu.
Muslim ametoa (habari) kutoka kwa Ibin Abbas, alisema: Mungu alifarad- hisha Swala kupitia ulimi wa Mtume wenu (s.a.w.w.) nyumbani rakaa nne na katika safari rakaa mbili. (Sahih Muslim, juzuu ya 2, uk.143) Babu Swalatul-Musafiriyna.
Lau tufanye mfano kuwa faradhi ilikuwa kupaka si kuosha na kwamba Mtume (s.a.w.w.) amezidisha kwenye faradhi kwa hukumu ya riwaya zina- zoamrisha kuosha, lakini tutafanyaje sasa na riwaya zinazoamrisha kupa- ka, nazo ni riwaya sahihi nyingi kama itakavyokujia kikamilifu, je hapa kuna kimbilio baada ya kupingana ila ni Kitabu kitukufu?!
Na maneno haya yote yanabainisha kuwa wafuasi wa riwaya hizi walichukuwa msimamo mapema mukabala wa Aya zinazoeleza na zenye dalili za wazi, na kulazimisha madhehebu yao juu yake (hizo Aya), jambo ambalo limewaingiza katika mbabaiko, matatizo na katika azma, na waligonga milango yote ili watoke humo na walijiangika na sababu za mapendekazo yasiyofaa.
KUSHIKAMANA NA MASILAHI.
Bwana wa ‘Manaar’ alipotambua kuwa maana dhahiri ya Aya ni kupaka juu ya miguu kwa mkono uliolowa kwa maji, alijaribu kuitoa Aya mbali na maana yake ya dhahiri kwa kushikamana na maslahi, na alisema: “Haiingii akilini hekima yoyote kuwajibisha kupaka juu ya unyayo kwa mkono uliolowa, bali ni kinyume na hekima ya wudhu, kwa sababu kulowana kiasi kidogo kukiingia juu ya kiungo ambacho kina vumbi au uchafu kwazidisha uchafu, na mkono wa mpakaji unapata sehemu ya uchafu huo.
Izingatiwe: Alilosema ni miongoni mwa mapendekezo, hayategemewi ikiwa tamko la kisheria lipo, wala hapana shaka kuwa hukumu za kishe- ria zinafuata maslaha ya kweli, wala si wajibu juu yetu kujuwa undani wake. Hivyo (kwa mtizamo wetu kibinadamu) kuna masilahi gani katika kupaka juu ya kichwa hata kwa kadiri ya kidole au vidole viwili, kiasi kwamba mpaka (Imamu) Shafiy amesema:
(Idha masahar ra’asa bi’iswibain wahidatin au baadhi iswibain au ba’a- tini kaffihi, au amara man yamsahu lahu, ajza’ahu dhalika ?!-
(Endapo atapaka kichwa kwa kidole kimoja au baadhi ya kidole au kwa sehemu ya ndani ya kitanga cha mkono wake, au akamuamuru atakayem- paka litamtosha hilo!
Na kuna neno la maana la Imamu Sharafud-dini Al’Musawiy, twalileta tamko lake hapa. Amesema: “Sisi tunaamini kuwa mfanya sheria mtakatifu aliwaangalia waja wake katika kila alichowakalifisha nacho miongoni mwa hukumu zake za kisheria, wala hakuwaamuru isipokuwa lenye maslahi kwao. Na wala hakuwakataza ila ambalo lenye ufisadi na ndani yake lina uovu kwao.
Lakini yeye (s.w.t.) pamoja na hayo hakujaalia chochote miongoni mwa uwezo wa kutambua hukumu hizo uwe umepimwa kulingana na maslahi na uovu kwa mujibu wa rai za waja, bali kutii kwao kuwe kwa dalili zenye nguvu alizowaainishia, hakuwafanyia mwanya wa kuelekea kingine.
Na ya kwanza miongoni mwa dalili hizo za hekima ni Kitabu cha Mungu Mtukufu, naye amepitisha hukumu ya kupaka vichwa na miguu katika udhu, hivyo hakuna upenyo wa kuacha kukiri hukumu yake. Ama usafi wa miguu kwakuwa mbali na uchafu hapana budi uhifad- hiwe kabla ya kupaka juu yake kulingana na dalili mahsusi zilizojulisha kuwa tohara ni sharti kwenye viungo vya wudhu kabla ya kuanza wudhu.24
KUINGIA KATI JUMLA: (FAMSAHU..) NI KWA AJILI YA KUBAINISHA UTARATIBU
Kwa hakika kufanya mwanya kati ya herufi ya kiungo “na” “??” kwa kauli (famsahu biru’usikum) ni kwa ajili ya kubainisha kutangulia kupaka kabla ya kuosha miguu.25
Izingatiwe: Msemaji ana nafasi ya kukusanya kati ya kuitaja taratibu na uwazi wa kubainisha kwa kukariri kitenzi kwa kusema:
Kwa hiyo yanakuwa maneno yake yamejengeka kulingana na makusudio yake na wakati huo huo yako safi bila ya utata.

ITAENDELEA KATIKA MAKALA IJAYO.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini