Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA NNE) A

0 Voti 00.0 / 5

KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA NNE) A
MLANGO WA 3: KANUNI MUHIMU ZA KIFIQHI -1 KWA WAWILI WALIOOANA NO: 1

HALI YA JANABA

Janaba ni kunajisika kiibada kunakosababishwa na kutokwa na manii au kwa kujamiiana, na yule mtu ambaye anawajibika kuoga Ghusl al- Janaabat anajulikana kama Mujnib.
MAMBO AMBAYO NI MAKRUH KWA MWENYE JANABA

MAMBO AMBAYO NI MAKRUH KWA MWENYE JANABA1

1. Kula

2. Kunywa

Hata hivyo, kama mtu huyu aliyeko kwenye hali ya janaba akiosha mikono yake, uso na kinywa, halafu akala na kunywa, katika hali hiyo haitakuwa makruh. Ni rahisi kwa hiyo basi kwa mtu kutawadha.

3. Kulala

Hata hivyo, kama mwenye janaba hana maji, au kwa sababu ya kutoku- patikana maji, anaweza kufanya tayammam badala ya Ghusl al-Janabat.

4. Kugusa sehemu yoyote ya kitabu, jalada, pambizo au ukingo wa Qur’ani Tukufu au ile sehemu katikati ya mistari yake.

5. Kufanya tendo la kujamiiana wakati mtu yuko kwenye hali ya Ihtilam (yaani aliyetokwa na manii usingizini).

6. Kuweka nywele henna.

7. Kupaka mafuta mwilini mwake mtu.

8. Kuchukua au kukaa na Qur’ani Tukufu.

9. Kusoma zaidi ya aya saba za Qur’ani, mbali na zile ambazo sijdah ya wajibu hutokea (kuzisoma aya hizo ni haram).

DOKEZO: Udhahiri wa ‘Makruh ya Ibada’ ni tofauti na kanuni ya jumla ya makruh, ambayo ni kwamba, ni bora kwamba mtu asilifanye tendo hilo. Kwa mfano, ni makruh kwa msafiri kuswali swala ya Dhuhri, al-Asr, na Ishaai nyuma ya mtu ambaye sio msafiri na kinyume chake,2 au ni makruh kusoma Qur’ani ndani ya sajidah.3

Hii ‘Makruh ya Ibada’ haina maana kwamba ni bora mtu asilifanye tendo hilo, bali hasa ina maana kwamba kama ukikifanya kitendo hicho, basi kiwango cha malipo yake yanayopatikana ni cha chini kulinganisha na kile cha kawaida.
MAMBO AMBAYO YANAKATAZWA KWA MTU MWENYE HALI YA JANABA

MAMBO AMBAYO YANAKATAZWA KWA MTU MWENYE HALI YA JANABA4

1. Kugusa kwa kiungo chochote cha mtu huyo, maandishi ya Qur’ani Tukufu, au jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa lugha yoyote ile iwayo. Ni bora vilevile kwamba yale majina 14 ya Ma’suumin (a.s.) pia yasiguswe katika hali hiyo.

2. Kuingia ndani ya Masjidul-Haraam au Masjidun-Nabii.

3. Kukaa au kusimama katika misikiti mingine yote, na hali kadhalika katika msingi wa tahadhari ya wajib kukaa katika maquba ya Maimam watukufu ni haram pia. Hata hivyo, hakuna madhara iwapo mtu atapita au kukatisha msikiti, kwa kuingia kupitia mlango mmoja na kutokea kwenye mwingine.

4. Kuingia msikitini kwa lengo la kunyanyua kitu au kuweka kitu ndani yake.

5. Kusoma aya za Qur’ani tukufu ambazo ndani yake kuleta sajidah kunakuwa ni wajibu

6. Surat ‘Alif Lam Mim Sajdah (32:15), Surat Haa Mim Sajdah (41:38), Suratun-Najm (53:62) na Surat al-Alaq (96:19).
JOSHO LA JANABA-(GHUSLUL-JANAABAH)
NYAKATI AMBAZO GHUSLUL-JANAABAH INAKUWA NI WAJIB:

1. Wakati mwanaume anapomuingilia mwanamke mpaka kwenye ile sehe- mu ya kutahiriwa kwake au zaidi, hata kama kumwaga manii hakuku- tokea, josho la janaba linakuwa ni wajibu kwao wote.5

2. Kama baada ya kujamiiana mwanaume hakufanya Istibraa (kujikamua) kwa ajili ya kutoa manii (ambayo ni kiasi cha kukojoa tu) na kisha akachukua josho, na baada ya hapo akaona utokwaji na kitu na hakuweza kutambua kama ni manii au hapana (yaani mkojo) itachukuliwa kwamba ni manii na kwa hiyo Ghusul-Janaabah itakuwa ni wajibu kwake tena.6

3. Kama mwanaume anatokwa na manii kwa kupitiwa usingizini.7
NYAKATI AMBAZO GHUSL AL-JANAABAT HALIWI WAJIB

1. Kama mtu anatia shaka kwamba dhakari yake imeingia mpaka sehemu aliyotahiriwa ama laa, hapo josho la janaba haliwi wajib kwao wote.8

2. Yale maji, unyevunyevu ambao unatolewa na mwanaume wakati wa kunyegereshana unaitwa Madhii na ni masafi kiibada. Yale majimaji yanayotoka baada ya kumwaga manii yanaitwa Wadhii, nayo ni masafi kiibada. Ule uoevu ambao wakati mwingine hutoka baada kukojoa unaitwa Wadii, ni msafi kiibada (isipokuwa ukikutana na mkojo) na hakuna mojawapo kati ya haya linalohitajia Ghusl. Iwapo mtu atafanya Istibraa baada ya kukojoa na kisha akatoa uoevu na akatia shaka kwamba ni mkojo au moja kati vioevu vilivyotajwa hapo juu, uoevu huo ni msafi kiibada.9

3. Kama mtu anashughulika katika kujamiiana mara moja na akataka kujishughulisha tena mara moja au mbili katika usiku mmoja, josho sio wajibu kwa kila mara baada ya kila tendo moja.

4. Kama mtu amemwaga manii katika usingizi wake na angependa kushughulika na kujamiiana, sio wajibu kwake kuoga josho kisha ndipo ashiriki katika tendo hilo. Ni makruh hata hivyo kujishughulisha katika tendo hilo katika wakati wa hali hiyo.10
KANUNI MUHIMU ZA JOSHO (GHUSL)
TARATIBU ZA JOSHO (CHINI YA BAFU YA MANYUNYU)

a.) Mtu kwanza ni lazima alete nia ya Ghusl na kisha aoshe kichwa na shingo halafu mwili mzima.

Ni bora kuosha upande wa kulia kwanza na kisha upande wa kushoto. Mwili hauwezi kuoshwa kabla ya kichwa11

b.) Hakuna madhara kama wakati wa kuosha shingo mtu akaosha sehemu kidogo ya upande wa kulia wa mwili wake.12

c.) Kama sehemu ya mwili imenajisika, sio muhimu kwanza kuifanya tohara ndipo uchukue Ghusl; bali wakati unapooga josho sehemu hiyo inaweza kutoharika.13

d.) Endapo sehemu yoyote ya mwili imeachwa na ukavu (hata kwa ukubwa wa kichwa cha sindano) josho hilo linakuwa ni batili.14

e.) Tofauti na wudhuu, katika Ghusl ni sawa kutochunga muwaalaat, yaani, baada ya kuosha kichwa na shingo, mtu halafu anafanya kitu kingine (kwa mfano, kuupaka mwili sabuni), ni sawa kwake kurudi tena kuosha mwili baada yake; sio lazima kwa josho hilo kuanzishwa upya kuanzia mwanzo kabisa.15

f.) Shuruti zote ambazo zinatengua wudhuu, vilevile zinatengua Ghusl.

g.) Kama mtu atatokea kukojoa wakati wa josho au kutokwa na ushuzi, sio lazima kwa josho kuanza upya; josho hilo hilo linaweza kumaliziwa. Hata hivyo, kama mtu atataka kuswali, basi kwa mujibu wa tahadhari ya wajib, wudhuu lazima uchukuliwe hapo kwani hairuhusiwi kuswali kwa tohara ya josho hilo hilo.16

h.) Ghusl yenye nia nyingi kama inavyohitajika, mustahab na wajib, kwa mfano, Ghusl ya sunna ya Ijumaa inaweza kufanywa wakati mmoja na Ghusl ya Janaba.17

i.) Baada ya Ghusl ya Janaba kufanyika, mtu lazima atawadhe kwa ajili ya Swala. Hii ndio hali kwa majosho yote ya wajibu. Kama nia nyingi zitaingizwa, kwa mfano nia ya mustahab na wajib, hapo tena wudhuu sio lazima.18
TAYAMMUM
NYAKATI AMBAZO TAYAMMUM INAWEZA KUTENDWA BADALA YA GHUSL

Kuna hali namna sita ambapo tayammam inaruhusiwa badala ya Josho, ambazo kwamba zifuatazo zinatumika sana kwa wanandoa:
1. WAKATI HAYAWEZI KUPATIKANA MAJI YA KUTOSHA JOSHO

Kama mtu anaishi kwenye sehemu yenye makazi ya watu wengi, anapaswa kufanya juhudi ya kutosha katika kupata maji kwa ajili ya Josho, mpaka wakati ambapo huenda matumaini yote yatakapopotea.19

Kwa hiyo endapo mtu atahitaji kufanya Ghusl ili aweze kuswali, na kwa wakati huo hakuna maji yanayoweza kupatikana, bali mtu akawa na hakika kwamba kabla swala hiyo haijawa qadhaa maji yatapatikana, basi ni lazima mtu asubiri hadi yatakapopatikana maji ili Josho liweze kufanyika.

Tayammam haiwezi kufanyika katika hali hii hata kama muda wa swala (wa fadhila) utakuwa umeingia au kama swala ya jamaa inaswaliwa.20

Hata kama kuna dalili kidogo tu kwamba maji yatapatikana kabla ya wakati wa swala, mtu hawezi kufanya tayammam na kuswali mpaka labda mtu atakapopoteza matumaini kabisa kwamba maji hayatapatikana kabisa kabla ya swala hiyo kuwa qadhaa.21

Hata hivyo, kama mtu ana uhakika kabisa kwamba maji hayatapatikana kabla ya qadhaa, basi hapo mtu anaweza kufanya tayammum na kuswali kwa wakati wa mapema iwezekenavyo.22
2. WAKATI INAPOKUWA NI KARIBU KUWA WAKATI WA QADHAA

Mtu anapaswa kufanya tayammum pale wakati uliobakia kwa swala hiyo kuwa qadhaa ni mdogo sana kiasi kwamba kama mtu atafanya Ghusl, hakutakuwa na muda uliobakia kwa kutekeleza swala hiyo.23
Hata kama mtu atakuwa na mashaka kwamba kutakuwa na muda wa kutosha au laa utakaokuwa umebaki kwa ajili ya swala kama akichukua josho au wudhuu, anapasika kufanya tayammam.24
3. HATARI KWA AFYA

Kama mtu akihofia kwamba endapo atatumia maji ataugua maradhi fulani au madhara ya kimwili, au ugonjwa ambao tayari anaugua utaendelea kwa muda mrefu, au utakuwa mkali zaidi au ugumu mwingine zaidi utaweza kujitokeza, basi anapaswa kufanya tayammam. Kwa mfano, kama mtu ana ugonjwa wa macho ama sindano mahali ambapo maji hayaruhusiwi juu yake kwa masaa 24, tayammam inapaswa kufanyika. Hata hivyo, endapo mtu anaweza kuyaepuka madhara hayo kwa kutumia maji ya vuguvugu, aandae maji ya vuguvugu kwa ajili ya Josho.25

REJEA:

    1. Islamic Laws – Shari’ah ya Kiislam; Kanuni ya 362
    2. Islamic Laws, Kanuni ya 1499
    3. Islamic Laws, Kanuni ya 1101
    4. Islamic Laws, Kanuni ya 361
    5. Islamic Laws, Kanuni ya 355
    6. Islamic Laws, Kanuni ya 354
    7. Islamic Laws, Kanuni ya 351
    8. Islamic Laws, Kanuni ya 356
    9. Islamic Laws, Kanuni ya 74
    10. Islamic Laws, Kanuni ya 362
    11. Islamic Laws, Kanuni ya 367
    12. Islamic Laws, Kanuni ya 369
    13. Islamic Laws, Kanuni ya 378
    14. Islamic Laws, Kanuni ya 380
    15. Islamic Laws, Kanuni ya 386
    16. Islamic Laws, Kanuni ya 392
    17. Islamic Laws, Kanuni ya 395
    18. Islamic Laws, Kanuni ya 397
    19. Islamic Laws, Kanuni ya 655
    20. Islamic Laws, Kanuni ya 723
    21. Islamic Laws, Kanuni ya 723
    22. Islamic Laws, Kanuni ya 723
    23. Islamic Laws, Kanuni ya 686
    24. Islamic Laws, Kanuni ya 686
    25. Islamic Laws, Kanuni ya 677

ITAENDELEA MAKALI IJAYO

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini