Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KUFUNGUA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA 3

0 Voti 00.0 / 5

KUFUNGUA SAFARINI KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNAH

Sehemu ya tatu

QUR-ANI TUKUFU NA SAUMU YA RAMADHANI SAFARINI

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga saumu, kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu." 2:183

يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون.

Siku maalumu za kuhesabika. Na ambaye alikuwa katika nyinyi ni mgonjwa au yuko safarini basi yampasa alipe idadi yake katika siku nyingine. Na wale waiwezayo kwa mashaka yawapasa fidia kumlisha masikini. Na ambaye atafanya kheri, basi kheri yake mwenyewe na mkifunga ni kheri kwenu, ikiwa mnajua." 2:184

أياما معدودات فمن كان منكم مريضاً أو على سفر فعدة من أيام أخر وعلى الذين يطيقونه فدية طعام مسكين فمن تطوع خيراً فهو له وأن تصوموا خير لكم إن كنتم تعلمون.

Ni mwezi wa Ramadhani iliyoteremshwa Qur-ani kuwa muongozo kwa watu, na dalili zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi mwenye kushuhudia mwezi huu na aufunge, na ambaye alikuwa mgonjwa au yuko safarini basi itampasa idadi katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu huwatakieni yaliyo mepesi wala hawatakieni yaliyo mazito, na mtimize hesabu na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongozeni na ili mpate kushukuru." 2:185

شهر رمضان الذي انزل فيه القران هدى للناس وبينت من الهدى والفرقان فمن شهيد منكم الشهر فليصمه ومن كان مريضاً أو على سفر فعدة من أيام أخر يريد الله بكم اليسر ولا يريد بكم العسر ولتكملواالعدة ولتكبرو الله على ما هداكم ولعلكم تشكرون.

Hakika Aya hizi tukufu zimebeba hukumu za makundi manne baada ya kuwa zimehimiza kuwa Saumu ni kati ya mambo yaliyolazimishwa kwa Waumini kama ilivyolazimishwa kwa wale wa kabla yao.

Mara nyingi tamko kulazimishwa ni alama ya kufaradhishwa na kuwajibishwa, na wala mukallafu haruhusiwi kuacha, hivyo Mwenyezi Mungu anawaambia Waumini wote: "Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga saumu, kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu."2:184

يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون

Hivyo Saumu imelazimishwa kwa mwanadamu kwa namna tofauti bila kutofautisha kati ya mzima mwenye afya, mgonjwa, msafiri na mwenye kuweza kwa mashaka. Lakini utekelezaji wake unatofautiana kulingana na kila hali ya mukallafu, kwa sababu kulingana na hali ni kuwa mukallafu amegawanyika katika makundi manne na kila kundi lina hukumu yake.

Mwanachuoni bora wa Sheriah ni yule anayepokea ufahamu wa Qur-ani na Sunnah, sawa iwe ufahamu huo unaafikiana na madhehebu ya Imamu wake anayemfuata au unatofautiana naye.

Isipokuwa wafasiri wengi katika kutafsiri Aya hizi wamejaribu kuzioanisha na madhehebu ya maimamu wao bila ya kuzamisha mtazamo ndani ya misamiati ya Aya na sentence zake ili watoe matokeo ya aina moja bila kutofautiana. Na bila shaka umeshajua kauli zao huko nyuma (Sehemu ya pili)

Hivyo tunasema:

Aya zilizotangulia zinabainisha hukumu ya makundi manne ambayo tayari umeshajua anuani zake. Hivyo kifuatacho ni upembuzi kuhusu kinachopatikana ndani ya Aya hizi kuhusu haki ya makundi haya manne.

Fuatana nami Sehemu ya nne katika upembuzi kuhusu kinachopatikana ndani ya Aya hizi kuhusu haki ya makundi haya manne.

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini