Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 3

0 Voti 00.0 / 5

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA

WAJIBU WA MWANAMUME

Sehemu ya tatu

MSIMAMIZI WA FAMILIA

MPENDE MKEO. 2

Angalia takwim zifuatazo. Mahitaji ya saikolojia ya mapenzi, uzembe wa waume kuhusu matakwa ya wake zao na kutozingatia umuhimu wa hadhi ya kiakili ya wanawake, ni vipengele ambavyo vimekuwa sababu ya kesi nyingi za kutalikiana.

Mnamo mwaka 1969 miongoni mwa kesi za kutengana 10372, katika kesi 1203 wanawake walionesha sababu ya kutaka kutalikiana kuwa ni kuvunjwa moyo kimaisha, kujihisi hathaminiwi na upungufu wa waume kutojali matakwa na hisia kubwa za wake zao."

Mwanamke alisema mahakamani; "Nipo tayari kuacha mahari yangu na hata kumlipa mume wangu fedha ili akubali kunipa talaka. Mume wangu anawapenda zaidi kasuku wake ndio sababu sitaki kuishi naye zaidi ya sasa."

Mapenzi na urafiki wa familia ni thamani kubwa zaidi kuliko chochote na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu ameiona hiyo kama mojawapo ya alama za uwezo na neema kubwa ambayo mwanadamu amepewa. Qur-ani Tukufu inasema:

ومن ءآيته أن خلق لكم من أنفسكم أزواجا لتسكنوا إليها وجعل بينكم مودة ورحمة إن في ذلك لأيت لقوم يتفكرون.

"Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wenza kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri. 30:21."

Imamu Ja'afar Sadiq alisema: Yeyote ambaye ni ni rafiki yetu huonesha wema zaidi kwa mke wake."

Mtukufu Mtume saww alisema: "Jinsi mtu anavyozidi kuwa mwaminifu ndivyo anavyozidi Kuonyesha wema kwa mke wake."

Imamu Ja'afar Sadiq as alisema: "Mmojawapo ya sifa bainifu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu ni kwamba wote ni wema kwa wake zao."

Mtukufu Mtume saww alisema: "Maneno ya mwanaume anayemwambia mke wake; "Ninakupenda kweli" kamwe hayaondoki moyoni mwake."

Kama ambavyo yalivyo, mapenzi na huba lazima yawe halisi na kuvutia kwenye moyo wa mwingine, lakini hata kupenda sana kwa mtu haitoshi, kwa kuwa ni muhimu Kuonyesha huba. Kwa Kuonyesha hisia zako kwa maneno na vitendo vyako, mapenzi unayoonesha, yatapata jibu zuri kutoka kwa mkeo na nyoyo zenu zitaimarisha muungano wa mapenzi.

Uwe wazi na udhihirishe mapenzi yako bila kusita. Wakati yupo au hayupo, msifie. Mwandikie barua (massage) unapokuwa safarini na mtaarifu kwamba kutokuwa karibu naye unajihisi mpweke sana. Mara kwa Mara mnunulie kitu kama zawadi. Mpigie simu unapokuwa ofisini au shughuli zako na umuulize hali yake.

Kitu kimoja cha muhimu sana kwenye akili ya mwanamke ni namna hizi za Kuonyesha mapenzi kwake.

Bibi mmoja wakati analia kwa masikitiko alisema: "Niliolewa na mume wangu usiku mmoja wa majira ya kupukutika kwa majani. Tuliishi pamoja kwa amani kwa muda fulani. Nilihisi kuwa nilikuwa mwanamke mwenye bahati kubwa sana hapa duniani. Niliishi kwenye nyumba yake ndogo kwa miaka sita.

Nilihisi ninayo furaha mara mia moja nilipogundua kwamba nilikuwa mja mzito. Nilipomtaarifu mume wangu alidondokwa na chozi la furaha wakati amenikumbatia mikononi mwake. Alilia sana hivyo kwamba karibu angeshindwa kujizuia.

Halafu akatoka nje na akaninunulia mkufu wa almasi kwa fedha yake ya akiba. Alinipa mkufu na akasema: "Ninatoa hii kwa mwanamke bora kuliko wote ambao nimewaona hapa duniani." Lakini (cha kusikitisha) baada ya muda mfupi alikufa kwenye ajali ya gari.

إن لله وإن إليه راجعون.

Fuatana nami Sehemu ya nne ya kanuni za ndoa na maadili ya familia

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini