Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini

KANUNIZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 9

0 Voti 00.0 / 5

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA

WAJIBU WA MWANAMUME

Sehemu ya tisa

MSIMAMIZI WA FAMILIA

MRIDHISHE NA MLIWAZE MKE WAKO

Pia mwanamke, kama ilivyo kwa mwanaume, hupata mabadiliko ya hisia kubwa. Huhisi furaha, hasira, huzuni na kadhalika. Huchoka kutokana na kazi za nyumbani na inawezekana akaudhiwa na watoto.

Watu wengine wanaweza kumtibua kwa shutuma zao. Inawezekana akaingia kwenye mashindano na wengine. Kwa ufupi, mwanamke hukabiliana na matatizo mengi ambapo mengine miongoni mwa hayo humuathiri sana hivyo kwamba anaweza kukata tamaa kwa kiwango ambacho kitasababisha atoe Majibu yasiyofaa hata kwa mambo madogo.

Hususan mfano huu ni wa upande wa wanawake, kwa sababu wao ni wepesi sana na hutoa Majibu kwa umakini zaidi kwa Matukio yasiyopendeza ikilinganishwa na waume.

Wanawake ambao hupata matatizo huhitaji kutulizwa. Wanaume lazima wawafariji kwa sababu ni wenzi wao na wao ndiyo wanaoaminiwa na wake zao.

Mpendwa bwana! Unapomuona mke wako katika huzuni na hasira basi jaribu kuelewa hali yake. Kama ukiingia nyumbani kwako na hakusalimu, wewe mtolee salam.'  Tendo hili halitakudhalilisha wewe. Ongea naye ukiwa katika tabasamu. Epuka ukali. Msaidie kazi za nyumbani. Uwe mwangalifu usimuudhi kwa namna yoyote. Usimtanie. Kama hajisikii kuzungumza, basi muache. Usiseme: Unasumbuliwa na nini?

Kama anayo hali ya kutaka kuzungumza, msikilize na mliwaze. Jifanye unahusika zaidi na tatizo lake kuliko yeye. Mruhusu akwambie malalamiko yake kwako. Halafu, kama vile baba mwema au mume mwenye huruma jaribu kumsaidia apate ufumbuzi wa tatizo lake.

Mpe moyo wa kuwa mvumilivu. Kwa busara na mantiki mfanye ayaone matatizo yake kama madogo. Imarisha tabia yake na msaidie kushinda sababu ya hasira yake, uwe mvumilivu na mtendee kufuatana na mantiki yako. Kwa hakika utaona, msaada wako kuwa unafaa na maisha yatarudi katika hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi kwenu nyinyi wote.

Kinyume chake, ukimwendea isivyo Sahihi, inawezekana ukasababisha matesa zaidi kwake. Pia wewe utateseka na inaweza kusababisha ugomvi mkubwa mno ambao utawapa usumbufu wote wawili.

Fuatana nami Sehemu ya kumi kanuni za ndoa na maadili ya familia

Toa maoni yako

Maoni ya watumiaji

Hakuna maoni
*
*

Site ya Al-Imaamaini Al-Hassanaini (A.S) ya usambazaji wa utamaduni wa Kiislamu na mafunzo ya Kidini